Uchakachuaji huu wa kanuni za Bunge uliofanywa na CCM haukubaliki popote | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchakachuaji huu wa kanuni za Bunge uliofanywa na CCM haukubaliki popote

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Watanzania, Feb 9, 2011.

 1. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2011
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kabla hata hatujasahau uchakachuaji wa kura za uraisi wa JK, kura za wabunge wa CCM, umeya wa jiji la Arusha, CCM sasa wameendeleza kufuru ya uchakachuaji wa waziwazi wa kanuni za Bunge. Ukisoma kanuni za kuunda kambi rasmi ya upinzani bungeni huwezi kuja na tafsiri ya kambi rasmi eti maana yake ni vyama vyote vya upinzani kama alivyosikika Anna Makinda akitamka uchakachuaji huo.

  Kanuni za bunge za kuunda kambi ya upinzani lazima zijitosheleze bila ya kujipinga zenyewe. Tangu mwanzo kanuni inaanza kwa kutoa mwongozo kuwa kambi rasmi ya upinzania itaundwa pale ambapo vyama vya upinzani vimefisha asilimia 12.5 ya wabunge wote. Na kwamba chama cha upinzania hakitakuwa na haki ya kuunda kambi ya upinzania hadi kiwe na wabunge wasiopungua asilimia 12.5. Na kwamba kama vyama viwili vinawabunge waliofikia asilimia 12.5, basi kile chenye wabunge wengi ndicho kitakachochagua kiongozi wa kambi ya upinzani na naibu wake. Kanuni inaeleza wazi kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani ndiye mwenye uwezo wa kuchagua wabunge wa chama chake au kambi rasmi ya upinzania kuwa wasemaji wa wizara.

  Tafsiri ya kambi rasmi ya upinzani haiwezi kuwa ya vyama vyote ikiwa kuna chama kinajitosheleza kwa wabunge kuunda kambi ya upinzani. Tafsiri hii inaweza kutumika pale tu ambapo hakuna chama cha upinzani kina wabunge wanaofikia asilimia 12.5, ambapo vyama vinalazimika kujiunga pamoja na kufikisha asilimia 12.5. Lakini kama kuna chama cha upinzani kimefikisha aslimia 12.5 na kimevipita vyama vingine kwa idadi ya wabunge ndicho chenye haki ya kuunda kambi rasmi ya upinzani bungeni. Si haki, na uchakachuaji huu wa makusudi wa CCM na spika wa bunge Anna Makinda haukubaliki kabisa na ni juu ya Chadema na Watanzania kupinga kwa nguvu zote uzandiki huu wa kulichezea bunge la Tanzania. Kutafsiri kanuni ya bunge kwa kupotosha wakati kanuni zinajieleza wazi ni uhaini mkubwa sana.

  Chadema na Watanzania tuchukue hatua za haraka sana za kisiasa, kisheria n.k. leo hii na si kesho ili kulinda na kurudisha heshima ya bunge letu.

  Kanuni za Kuunda kambi ya upinzania
  14.
  -(1) Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni atachaguliwa
  chini ya utaratibu ulioainishwa kwenye fasili za Kanuni hii
  zinazofuata.
  (2) Wabunge wote wa Upinzani wanaweza kuunda Kambi Rasmi
  ya Upinzani iwapo idadi yao itakuwa si chini ya asilimia kumi na
  mbili na nusu ya Wabunge wote.
  (3) Chama cha Upinzani hakitakuwa na haki ya kuchagua
  Kiongozi wa Upinzani Bungeni, isipokuwa tu kama kina idadi ya
  Wabunge wasiopungua asilimia kumi na mbili na nusu ya Wabunge
  wote.
  (4) Endapo kutakuwa na Vyama vya Upinzani zaidi ya kimoja
  ambavyo kila kimoja kina Wabunge asilimia kumi na mbili na nusu
  au zaidi, basi Chama chenye idadi kubwa zaidi ya Wabunge kuliko
  vingine ndicho kitakuwa na haki ya kuchagua Kiongozi wa Kambi
  Rasmi ya Upinzani Bungeni, lakini, ikiwa kutakuwa na vyama viwili
  au zaidi vyenye idadi sawa ya Wabunge ambao ni zaidi ya asilimia
  kumi na mbili na nusu, Wabunge wa vyama vinavyohusika
  watachagua Kiongozi wa Upinzani Bungeni chini ya utaratibu
  watakaokubaliana wenyewe.
  15
  .-(1) Chama chenye haki ya kumchagua Kiongozi wa Kambi Rasmi
  ya Upinzani Bungeni kinaweza pia kuchagua Naibu Kiongozi wa
  Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.
  (2) Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni atateua
  Wabunge wa Chama chake au Wabunge wa Kambi Rasmi ya
  Upinzani Bungeni ambao watakuwa wasemaji wakuu wa Kambi ya
  Upinzani kwa Wizara zilizopo za Serikali.
   
 2. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #2
  Feb 9, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nchi yetu sasa imefikia mahali pabaya kwa habari ya msimamo. Watu wanaweza kutafsiri kama haina kichwa. Kila mara ule uadilifu wa kusimamia maneno yao umeondoka. Endapo hali itaendelea hivi basi imani kwa serikali itakuwa imekwisha. Nawashauri viongozi wa serikali na viongozi wa vyama vya siasa kusimamia maneno yao. Je sio Spika huyu huyu ambaye alisikika akisema juu ya kanuni kuwa haiwezekani kwa kambi ya upinzani kuwa na kambi mbili. Je kama spika akianza hivi na mapema imani ya wananchi kwa bunge itakuwaje?
  Ni vizuri maslahi ya Taifa yakawa juu kuliko ya vyama. Unahitajika umakini katika kuisimamia serikali. Hakuna sababu ya kuhofu kwa chama cha upinzani makini kuwa viongozi wa kamati za bunge endapo maslahi ya tiafa niyo yaliyo juu.
   
 3. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,067
  Trophy Points: 280
  Kwa bahati mbaya mimi bado sijaelewa athari za mabadiliko ya tafsiri yaliyofanywa katika muktadha wa kanuni zenyewe. Mabadiliko hayo ya tafsiri yatainyima(yataipunguzia) CDM nini hasa yakisomwa pamoja na kanuni zenyewe?
   
 4. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #4
  Feb 9, 2011
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu uchakachuaji huu wa makusudi unataka kuwalazimisha Chadema bila hiari yao wawajumuishe vyama vingine kwenye kambi ya upinzani kinyume na kanuni zenyewe. Kwa kuwa Chadema wana asilimia 12.5 na imevipita vyama vingine, kanuni za bunge zinawaruhusu kuunda kambi ya upinzani bila kushirikisha vyama vingine. Lakini tafsiri ya CCM na Anna Makinda inapingana na kanuni zote.
   
 5. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #5
  Feb 9, 2011
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tatizo ni kwamba kanuni inachakachuliwa kwa manufaa ya CCM. Haikubaliki tafsiri ipingane na kanuni zingine
   
 6. cabhatica

  cabhatica JF-Expert Member

  #6
  Feb 9, 2011
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 1,074
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Angalizo: Hili suala la vyama lina walakini. Tanzania ya watu milioni 40, walio wanachama wa vyama vya siasa vyote hawafiki robo (yaani mil 10). Waheshimiwa wabunge wetu wajue wamechaguliwa na watanzania na watanzania wanataka maendeleo. Kwa mwendo huu nashawishika kuamini kwamba tunahitaji wagombea binafsi sasa ili kuondoa hili ombwe na jinamizi la uchama. Katiba mpya ikichelewa, misri inanukia.

  Imezoeleka sasa kwamba kanuni au tafsiri zinaletwa sio kwa nia ya kusukuma maendeleo ya taifa bali kulinda aina fulani ya mfumo wanaotaka watawala....Chadema msikubali kuyumbishwa....kuna watu wenye akili timamu wanafuatilia kwa karibu...msichoke kusimama kwenye haki...siku moja watz watawakumbuka kama Mwalimu
   
 7. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #7
  Feb 9, 2011
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Zamani nilifikiri bunge ndo mahali pekee pa kupatia haki za wananchi, i was so wrong. they are self centred sana na wako kufanya lolote kwa maslahi yao tuu, kweli duniani hakuna haki. niko so demoralized.
   
 8. H

  Haika JF-Expert Member

  #8
  Feb 9, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  inashangaza!!
   
 9. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #9
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  ".........Ukisoma kanuni za kuunda kambi rasmi ya upinzani bungeni huwezi kuja na tafsiri ya kambi rasmi eti maana yake ni vyama vyote vya upinzani kama alivyosikika Anna Makinda akitamka uchakachuaji huo....."

  Huyo mama hawatendei haki akina mama wengine wanaowakilishwa na jinsia yake maana ana-paint picha kwamba
  1. akina mama ni watu wa kukurupuka na kutoa maamuzi wakipewa nafasi kubwa kitu macho si kweli..

  2. Anatoa picha kwamba akina mama si watumakini kitu ambacho si kweli hasa ukizingatia kazi na majambozi ya Mdee...

  3. Anatoa picha kwamba akina mama kazi yao kubwa ni kuwafurahisha akina baba ili wasiendelee kugombana na kusahu kwamba kazi aliyopewa ina nafasi ya kumpa uraisi kama (God Forbid) raisi wa nchi akifariki gafla...
  4. Anapingana na kauli yake mwenyewe kwamba jambo ambalo halina maslahi kwa taifa halipaswi kuchukua muda wa bunge maana ni sisi tax payers tunaowalipa siku zote kwa kazi za kipuuzi kama hizi za kutafsiri kanuni na taratibu zilizopitishwa na zililokubalika na bunge la 9

  5. Labda atuambie tangu lini sisi wapiga kura tuliwatuma kwenda kubadlisha kanuni na sio kutunga sheria na za kuwabana mafisadi?

  Akina mama popote pale mlipo amkeni na mkemeeni kama shetani anavyokemea na akina kakobe vinginevyo mama huyo anaiwekea jinsia yenu matatani katika kushika nyadhifa kubwa kama akina Tibaijuka... MSIPOAMUKA siku mkitaka kugombea uraisi tutawapinga kwa sababu ya mambo ya akina makinda..
   
 10. MADAM T

  MADAM T JF-Expert Member

  #10
  Feb 9, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 3,653
  Likes Received: 937
  Trophy Points: 280
  Nashindwa hata kuelezea nilivyokerwa na jambo hili, najiuliza kila mara kwanini CCM hawana aibu kiasi hicho na kwanini wanatudharau namna hiyo? Wanafikiri watanzania wote ni bendera fuata upepo kama wanachama wao? kwamba hatuna uwezo wa kufikiri au ni ulevi wa madaraka ndio unawasumbua... hivi hii idea kwanini hawakuitoa wakati CHADEMA ina wanawabunge wachache, nawaunga mkono kwa 100% CHADEMA kwa walichokifanya ila sijui nitoe mchango gani kuhakikisha CCM hawafanikiwi kwa walichopanga. Sijui lini na sisi tutakuwa majasiri kama wenzetu wa Tunisia na Misri...
   
 11. g

  gidytitus JF-Expert Member

  #11
  Feb 9, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 332
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Wakati tuliokuwa tukiusubiri kuona CCM wanavyojarbu kuupiga vita upinzani mahiri wa CHADEMA ni sasa, nadhani watanzania wale wote wanaotaka kufahamu nyendo na matendo yanayotendwa na CCM kila siku, jana wameshuhudia ni kitu gani kimeanza, Mimi nachoomba kwa wana JF na watanzania wote kufaham ni kwamba madai yote yanayotafutwa na CCM kutaka vyama vyote pinzani kujiunga si kwa nia nzuri, wamejaribu hata kuchakachua na kuongeza kanuni ambazo hata hazikuwepo wakidhania kuwa CHADEMA hawatoona. Na tufahamu kuwa CCM na CUF ni kitu kimoja mpaka sasa kwa hiyo wanajaribu kuingiza mashushu na wasaliti kupitia shati la Upinzani, Chonde chonde CHADEMA kataeni hiyo sumu!!!!, hata kwa kuandamana mjengoni huko huko, bunge ni la kwetu wananchi na wala si la CCM na CUF, pigeni ngumi hizo meza mpaka zipasuke lakini kieleweke!!!,. Wasomeni machoni mwao kuna tabasam la kinafiki! huo urafiki wa kutaka kutujengea uadui ndani yetu hatuutaki hatuutaki!!, Halafu kwa nini wanatudharau kiasi hichoo? wapuuzi kweli!, hivi wanadhania kuwa mpaka tukaamua kufanya hivyo tulikuwa hatujui kuwa tunazuia nini na ni kwa sababu gani, mi nawashauri CCM wajinge na CUF kwani ni ndugu tayari useme tu walikuwa hawajafahamiana coz dingi yao alichelewa kuwatambulisha!!, ni vyama viwili tayari vilivyoko madarakani, wakifanya hivyo watuache, kisha CHADEMA itajiunga na vyama pinzani vingine viliyobaki. kama si hivyo CHADEMA endelei kuwa CHADEMA hivyo hivyo, ukizingatia si nyie bali ni umma mkubwa wa watanzania uliopo nyuma yenu, tafadhrini sana CCM na CUF waacheni hao wawakilishi wetu, la sivyo wote tutaingia bungeni coz mmeshindwa kuwasikiliza na kuwatii wao.CHADEMA kuweni makini na huyo mama, naye ni kibaraka wa ccm na CUF, kwani hatumwamini kuwa ataisimamia haki kama inavyotakiwa, lakini kwa muundo wa Tundu Lisu, atajiuzuru ngazi hiyo wakati akienda kutibiwa PRESHA hukoooo!! Big up Tundu, tunakukubali, endelea kupiga hizo meza, but kuwa makini coz ipo day waweza kushtakiwa kuwa umeua kwa kumsababishia presha huyo mama!!, coz hayuko fresh kiafya, lakini usijali coz kayataka mwenyewe!! RAi yangu kwa vyama vingine tofauti na hivi vyama viwil tawala ni kwamba anakayetaka kwenda nasi na auvue na kuupiga vita huo uovu kwanza!!.
   
 12. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #12
  Feb 9, 2011
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyu mama anashangaza sana. Hajui umuhimu wa nafasi yake ya kulinda hadhi ya bunge na ofisi ya Uspika. Mimi hata sijui CCM na Anna Makinda wametumia ufahamu wa kutoka sayari gani. Yaani chama ambacho hakina haki ya kuunda kambi rasmi ya bunge eti kijumuishwe kwenye kambi hiyo kinyume cha kanuni ni ajabu kabisa. Iweje chama chenye wabunge pungufu ya asilimia 12.5 kijumuishwe kwenye kambi rasmi ya bunge wakati kanuni zinakataa? CCM sasa mnaipeleka nchi wapi hata kuchezeachezea bunge?
   
 13. J

  Jenifa JF-Expert Member

  #13
  Feb 9, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  chadema mliamua kubagua sasa mmebaguliwa. mizee mizima hovyo

  nimelipenda hilo la waturudi kwenye posho wana madeni benki
   
 14. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #14
  Feb 9, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ahsante sana ndugu yagu. lakini kumbuka Pia Spika ana nafasi nzito katika kubalisha kanuni za Bunge.

  Pitia kanuni ya Kifungu cha 152 (3) ambacho kinasema bayana kuwa Spika akishauriana na kamati ya kanuni za Bunge atakuwa na madaraka ya kuzifanyia marekebisho au mabadiliko, nyongeza za kanuni za bunge kulingana na mahitaji ya wakati, kadri atakavyoona inafaa.


  Kwa msingi huo Sasa ni wakati muafaka kuondoa Hilo neno RASMI ili kuwepo na uakilishi mahiri wa upinzani bungeni Pindi wapinzani wanaposhindwa kukubaliana tena kwa hoja hafifu.

  Inasikitisha sana kuona chadema wanaposema CUF sio chama cha Upinzani kwa sababu tu wameungana kuunda serikali ya mseto zanzibar. Lakini wanasahau kuwa Serikali inaanzia katika ngazi za mitaa na kuendelea mpaka kwenye halmashauri, manispaa na majiji.

  sasa vipi huko kwenye ngazi za wilaya wao wanaungana na CCM kuunda mabaraza ya madiwani. kwanini wasijitoe na huko.

  Uroho tu na ukabila, udini umewajaa.

   
 15. M

  Mwan mpambanaji JF-Expert Member

  #15
  Feb 9, 2011
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 468
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Niliiwahi kusema na narudia tena,haki haiombwi,na kwa kadri tunavyozidi kunyamaza ndivyo ccm wanatake advantage,swala la haki nchini si la chadema ni la watu wote,ndugu zangu tuingie mitaani tukomeshe uhuni huu.
   
 16. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #16
  Feb 9, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  haya yooooote kwa Chadema ni DHAMBI YA UBAGUZI wa kidini, Kikanda na bado msipoangalia dhanbi hii itawamaliza wenyewe.
   
 17. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #17
  Feb 9, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Huhitaji kuwa mtaalamu wa hermeneutics kuelewa hizo kanuni zinaeleza nini. Kanuni hizo zipo wazi na hazihitaji maelezo zaidi au vifungu vingine vya kanuni.
   
 18. K

  Ki tochi Member

  #18
  Feb 9, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  kweli hesabu ugonjwa wa taifa!!!!!!!!!
  ukiambiwa idadi si chini ya 12.5% .... Maana yake wawe 12.5% au zaidi.

  CDM wako 12.5% kwa nini wasianzishe kambi yao?
  CCM wako zaidi ya 12.5% ndo maana wako wenyewe.

  Hivi kweli kama Spika hapa umeshindwa kuelewa hili,
  KATIBA SI NDO TUTAPELEKWA CHAKA LA HATARI.


   
 19. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #19
  Feb 9, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,163
  Likes Received: 1,122
  Trophy Points: 280
  naomba mfano wa halmashauri ambapo CDM wameungana na CCM kuunda baraza la madiwani? if you do not have any, delete this shit of yours!!
   
 20. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #20
  Feb 9, 2011
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapa tatizo ni kwamba, tafsiri ya kuchakachua ya CCM inapinga kanuni za msingi zinazoelekeza kuwa chama cha upinzania kinapata haki ya kuunda au kuwa katika kambi rasmi ya upinzani ikiwa kimefikisha asilimia 12.5 ya wabunge wote. Kama vyama vyote havina idadi hiyo ndio vinaungana kupata asilimia 12.5 na kuunda kambi rasmi. Chadema inajitosheleza kuunda kambi rasmi, na vyama vingine kulingana na kanuni havina haki ya kuwemo katika kambi rasmi ya upinzani. Hivyo kulingana na kanuni Chadema yenye wabunge wengi hailazimiki kuingiza wabunge wa vyama vingine kwenye kambi rasmi ya upinzani. Hiyo tafsiri ya kuchakachuwa ya CCM si halali kwa namna yeyote ile na haikubaliki. Inadhalilisha bunge na kuwa kama kilabu cha pombe.
   
Loading...