Elections 2010 Uchakachuaji huu usipodhibitiwa utalitumbukiza taifa kwenye mapinduzi ya kiraia

Membensamba

Senior Member
Nov 4, 2010
157
10
Mahali popote yalipowahi kutokea mapinduzi ya raia, ukiangalia sana utagundua kuwa nyuma ya mambo kulikuwa na historia ya raia kunyimwa haki zao za msingi au serikali ilikiuka maadili ya utawala bora kwa kiwango kisichovumiliwa. Haki ya raia kujichagulia viongozi wake ni ya msingi, na raia wakiona wananyang'anywa haki hiyo mara kwa mara uwezekano mkubwa ni kufanya mapinduzi ya kiraia ambayo huweza kuleta maafa makubwa (Mungu apishe mbali).

Tanzania hizi sasa inashuhudia matukio yenye harufu kali ya uchakachuaji wa kura kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika october 31. Dalili zimeonekana wazi kuwa wananchi wamekerwa na uchakachuaji huu kiasi cha kufanya ghasia, ikiwa ni pamoja na kuchoma na kuharibu mali.

Matukio haya hakuna mtu angeamini kuwa yanaweza kutokea Tanzania inayojulikana kama kisiwa cha amani. Tumefikaje hapa? Kilichotufikisha hapa ni wananchi kutishiwa kunyimwa haki yao ya msingi ya kujichagulia viongozi kwa njia ya kubadilishwa matokeo ya uchaguzi kwa njia ya rushwa, au kununuliwa washindi wa uchaguzi, au kuibiwa kura.

Leo tumesikia mgombea uraisi Mhe. Dr. Slaa akilalamikia hilo hilo. Hali hii isipokemewa, iko siku tutajikuta tumo katikati ya mapinduzi ya kiraia. Watu wamekamatwa na mihuri ya tume, wengine karatasi za kura, lakini wahusika wako kimya wala hakuna kemeo lolote kutoka tume ya uchaguzi wala serikali. HII NI HATARI.
 
Back
Top Bottom