Uchakachuaji huu usipodhibitiwa utalitumbukiza taifa kwenye mapinduzi ya kiraia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchakachuaji huu usipodhibitiwa utalitumbukiza taifa kwenye mapinduzi ya kiraia

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Membensamba, Nov 4, 2010.

 1. M

  Membensamba Senior Member

  #1
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 157
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mahali popote yalipowahi kutokea mapinduzi ya raia, ukiangalia sana utagundua kuwa nyuma ya mambo kulikuwa na historia ya raia kunyimwa haki zao za msingi au serikali ilikiuka maadili ya utawala bora kwa kiwango kisichovumiliwa. Haki ya raia kujichagulia viongozi wake ni ya msingi, na raia wakiona wananyang'anywa haki hiyo mara kwa mara uwezekano mkubwa ni kufanya mapinduzi ya kiraia ambayo huweza kuleta maafa makubwa (Mungu apishe mbali).

  Tanzania hizi sasa inashuhudia matukio yenye harufu kali ya uchakachuaji wa kura kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika october 31. Dalili zimeonekana wazi kuwa wananchi wamekerwa na uchakachuaji huu kiasi cha kufanya ghasia, ikiwa ni pamoja na kuchoma na kuharibu mali.

  Matukio haya hakuna mtu angeamini kuwa yanaweza kutokea Tanzania inayojulikana kama kisiwa cha amani. Tumefikaje hapa? Kilichotufikisha hapa ni wananchi kutishiwa kunyimwa haki yao ya msingi ya kujichagulia viongozi kwa njia ya kubadilishwa matokeo ya uchaguzi kwa njia ya rushwa, au kununuliwa washindi wa uchaguzi, au kuibiwa kura.

  Leo tumesikia mgombea uraisi Mhe. Dr. Slaa akilalamikia hilo hilo. Hali hii isipokemewa, iko siku tutajikuta tumo katikati ya mapinduzi ya kiraia. Watu wamekamatwa na mihuri ya tume, wengine karatasi za kura, lakini wahusika wako kimya wala hakuna kemeo lolote kutoka tume ya uchaguzi wala serikali. HII NI HATARI.
   
Loading...