Kuna watu wanaonekana kushabikia au kumlaumu mpiganaji Slaa kwa kusema kuwa kura zake zinachakachuliwa. Nia ni kupunguza idadi ya viti maalumu kwa upande wa Chadema ili CCM iweze kuingiza wanawake wao ambao waliwateua kwa wingi wakidhani kuwa upinzani usingekuwa na nguvu. Ni vizuri pia tukajua mapema formula watakayotumia NEC kuteua wabunge wa viti maalumu ambao mwaka huu ni asilimia 40 ya wabunge wote wa kuchaguliwa. Kila kura ya slaa ina umuhimu katika kuamua ni wabunge wangapi itapata katika mgao wa viti maalumu. Hivyo ni vizuri Tume isichukulie jambo hili kijuujuu!