Elections 2010 Uchahakachuaji wa Matokeo ya Slaa na Viti Maalumu

Jobo

JF-Expert Member
May 15, 2008
586
43
Kuna watu wanaonekana kushabikia au kumlaumu mpiganaji Slaa kwa kusema kuwa kura zake zinachakachuliwa. Nia ni kupunguza idadi ya viti maalumu kwa upande wa Chadema ili CCM iweze kuingiza wanawake wao ambao waliwateua kwa wingi wakidhani kuwa upinzani usingekuwa na nguvu. Ni vizuri pia tukajua mapema formula watakayotumia NEC kuteua wabunge wa viti maalumu ambao mwaka huu ni asilimia 40 ya wabunge wote wa kuchaguliwa. Kila kura ya slaa ina umuhimu katika kuamua ni wabunge wangapi itapata katika mgao wa viti maalumu. Hivyo ni vizuri Tume isichukulie jambo hili kijuujuu!
 
Well written!

I hope Dr. Slaa has already submitted to NEC his complains and supporting documents for votes rigging.
 
kwa taarifa yenu hilo ndio lengo kubwa la Dr Slaaa, maana anajua kumtoa aliye madarakani ni kazi sana, ila kama CCM wamepata 52% na Dr Slaa apewe haki yake ya 43% anayostahiii,
 
Well written!

I hope Dr. Slaa has already submitted to NEC his complains and supporting documents for votes rigging.

Superman, unaweza kuniambia wabunge wa viti maalumu wanapatikanaje? Ni kura za rais au majimbo?
 
Vinapatikana kutokana na asilimia ya kura za Urais.

Sasa hivi idadi ya majimbo ya uchaguzi ni: 239

Bunge lililopita lilikuwa na viti 323 Kikatiba. Yameongezeka majimbo 7 na kufanya jumla ya viti kuwa 330. majimbo ya Uchaguzi mwaka huu ni 239. Rais ana viti 10 vya kuteua. Hivyo vinabaki viti 81. Hivi vinagawanywa kwa % ya wingi wa kura za urais.

Mfano kama JK akipata 64% then CCM watapewa viti: 52
Kama Slaa akipata say 26% then CHADEMA watapata viti 21. n.k
 
Na ndio maana Slaa anataka kura zake kama vile wananchi walivyopiga, na kimsingi huo ndo ulikuwa mpango wa kwanza wa CHADEMA kupata wabunge wengi wa kuchaguliwa na kura nyingi za urais kupata viti maalum vingi Bungeni. Uwezekano wa kupata Urais hata wao naamini alijua si rahisi kwao.

Kama kweli tunataka bunge zuri tuwe upande wa Dr Slaa kudai kura za urais zilizoporwa na hao wanaojiita ma jiniaz wa IT wa Kikwete
 
nadhani siyo kweli superman. Viti maalum mwaka huu ni 105, vimeongezeka toka 75 vya 2005.

Viti maalum vinatokana na asilimia ya kura za wagombea ubunge kwa ujumla

Tanzanian general election, 2005 - Wikipedia, the free encyclopedia

pia asilimia ya kura za Rais, Wabunge na madiwani kwa pamoja zinachangia kwenye kufanya mahesabu kwa ajili ya RUZUKU pesa ambayo ni muhimu kwa ujenzi wa chama, kulipa watendaji, kuendesha kampeni, mikutano, kujenga miundombinu ya chama na kufanya maandalizi kwa ajili ya Uchaguzi ujao.

Jambo la kujivunia kwa chadema ni kwamba ruzuku waliyokuwa wakipata ilikuwa ni asilimia 6% ya ruzuko yote lakini wameshinda kwa zaidi ya asilimia 20%. maana yake ni kwamba kama wakipata hiyo asilimia 20% ya Ruzuku yote basi watapata mafanikio zaidi uchaguzi ujao.... freedom is coming
 
Ni kweli. Kwa mantiki hii Chadema itapata nafasi nyingi tu hasa ukizingatia kwamba walipata ushindi kwenye majimbo yenye wapiga kura wengi.
 
its a ,mess to think CCM will ever change the Tanzanians life...hatari zaidi kwani ni ushindi wa CCM nikigezo tosha kuwa watanzania wengi ni mbumbu na hao ni wale wote waliokichagua chama cha mapinduzi
 
nilisahau kuongeza pia kura za madiwani zinatoa nafasi kwa madiwani wa viti maalum pia.

kwa hiyo sehemu nyingi walizochakachua CHADEMA imeshika nafasi ya pili hasa kwenye wapiga kura wote, mfano kura alizopata Slaa Ubungo pekee ni zaidi ya kura za kikwete zanzibar yote
Kura alizopata Myika Ubungo pekee ni zaidi ya kura za wabunge wote wa CUF zanzibar ambao wanachaguliwa kwa kura 3500 wakati JJ Mnyika kagonga over 60,000
 
Superman uteuzi hautegemei kura ya urais. Kura ya urais haina nafasi katika kuchagua wabunge kwa kuwa inahusisha asasi mbili tofauti (Concept ya separation of powers between the legislature na executive). Idadi ya Wabunge wa viti maalum inategemea agregate vote ya kura za wabunge wote baada ya kujumlishwa na kugawanywa na ndio maana CHADEMA ilipata viti 6 maalum mwaka 2005 wakti ilikuwa na wabunge watano wa kuchaguliwa. kwa mantiki hiyo CUF pia itapata viti vichache sana maana kura za ubunge za cuf ni ndogo sana (ukizingatia walikoshinda sana yaani Zanzibar kura ni 5000 kwa jimbo).

CHADEMA wanatarajiwa kupata wabunge kama 25 wa viti maalum.

Vinapatikana kutokana na asilimia ya kura za Urais.

Sasa hivi idadi ya majimbo ya uchaguzi ni: 239

Bunge lililopita lilikuwa na viti 323 Kikatiba. Yameongezeka majimbo 7 na kufanya jumla ya viti kuwa 330. majimbo ya Uchaguzi mwaka huu ni 239. Rais ana viti 10 vya kuteua. Hivyo vinabaki viti 81. Hivi vinagawanywa kwa % ya wingi wa kura za urais.

Mfano kama JK akipata 64% then CCM watapewa viti: 52
Kama Slaa akipata say 26% then CHADEMA watapata viti 21. n.k
 
Kuna watu wanaonekana kushabikia au kumlaumu mpiganaji Slaa kwa kusema kuwa kura zake zinachakachuliwa. Nia ni kupunguza idadi ya viti maalumu kwa upande wa Chadema ili CCM iweze kuingiza wanawake wao ambao waliwateua kwa wingi wakidhani kuwa upinzani usingekuwa na nguvu. Ni vizuri pia tukajua mapema formula watakayotumia NEC kuteua wabunge wa viti maalumu ambao mwaka huu ni asilimia 40 ya wabunge wote wa kuchaguliwa. Kila kura ya slaa ina umuhimu katika kuamua ni wabunge wangapi itapata katika mgao wa viti maalumu. Hivyo ni vizuri Tume isichukulie jambo hili kijuujuu!

Jobo,

Lakini unajua kwamba kura za kupata viti maalumu hazitokani na kura za mgombea urais?

Kura za urais zinaingia pale tu ambapo chama hakina mgombea ubunge kwenye jimbo husika. Kura zinazotumika ni zile za wagombea ubunge.

Kwa mfano jimbo ambalo CHADEMA hawakuweka wagombea ubunge basi kura alizopata mgombea urais kwenye hayo majimbo zitatumika.

CHADEMA iliweka wagombea karibu 180 katika majimbo 239. Majimbo mengi ambayo hawakuweka ni pamoja na Zanzibar ambako Dr. Slaa kama mgombea urais hana kura nyingi. Pia majimbo mengi ya vijijini ambako nako hana kura nyingi.

Tuelewe katiba inasema nini kabla ya kuja na tuhuma kama hizi.
 
Vinapatikana kutokana na asilimia ya kura za Urais.

Sasa hivi idadi ya majimbo ya uchaguzi ni: 239

Bunge lililopita lilikuwa na viti 323 Kikatiba. Yameongezeka majimbo 7 na kufanya jumla ya viti kuwa 330. majimbo ya Uchaguzi mwaka huu ni 239. Rais ana viti 10 vya kuteua. Hivyo vinabaki viti 81. Hivi vinagawanywa kwa % ya wingi wa kura za urais.

Mfano kama JK akipata 64% then CCM watapewa viti: 52
Kama Slaa akipata say 26% then CHADEMA watapata viti 21. n.k

Mkuu Superman,

Naona hapa hujawa superman ha haaaa!!! Inabidi usome tena somo la uraia.

Viti maalumu vya wabunge vinatokana na kura za wagombea ubunge. Viti maalum vya madiwani, vinatokana na kura za madiwani.

Kura za urais zinaingia pale tu ambapo chama hakina mgombea wa ubunge au udiwani.

Effect ya kura za Slaa kwenye mgawo wa viti maalum itakuwa ndogo sana.
 
nadhani siyo kweli superman. Viti maalum mwaka huu ni 105, vimeongezeka toka 75 vya 2005.

Viti maalum vinatokana na asilimia ya kura za wagombea ubunge kwa ujumla

Tanzanian general election, 2005 - Wikipedia, the free encyclopedia

pia asilimia ya kura za Rais, Wabunge na madiwani kwa pamoja zinachangia kwenye kufanya mahesabu kwa ajili ya RUZUKU pesa ambayo ni muhimu kwa ujenzi wa chama, kulipa watendaji, kuendesha kampeni, mikutano, kujenga miundombinu ya chama na kufanya maandalizi kwa ajili ya Uchaguzi ujao.

Jambo la kujivunia kwa chadema ni kwamba ruzuku waliyokuwa wakipata ilikuwa ni asilimia 6% ya ruzuko yote lakini wameshinda kwa zaidi ya asilimia 20%. maana yake ni kwamba kama wakipata hiyo asilimia 20% ya Ruzuku yote basi watapata mafanikio zaidi uchaguzi ujao.... freedom is coming

Hesabu ya viti maalum inakakatuliwa ifuatavyo:

1. Bunge litakuwa na wabunge 326, at least 30% inatakiwa wawe wanawake, namba ambayo ni kama wabunge 98.
2. Lakini kuna wabunge wanawake wameshinda majimboni, katika hiyo 98 toa hiyo namba. Kwa mfano kama wameshinda majimboni wanawake 10, basi namba inapungua na kuwa 88.

3. Hiyo 88 ndiyo vyama vinagawana kulingana na kura za wabunge ambazo kila chama kimepata. Mimi nahisi CCM watapata viti kama 50, CHADEMA 20 na vinavyobaki watagawana CUF, NCCR UDP na TLP.
 
Hapana, wabunge wanawake wa majimbo hawapunguzwi katika ile 30%. Asilimia hii iko fixed. Ndiyo maana wachambuzi walisema kama wanawake wakijitokeza wengi kwenye majimbo, kuna uwezekano wa kufikia asilimia 50:50.
 
Back
Top Bottom