Uchaguzi Zambia: Hakainde Hichilema anaongoza dhidi ya Rais Edgar Lungu

Ss Jr

JF-Expert Member
Jan 15, 2018
577
450
Rais wa Zambia, Edgar Lungu

MGOMBEA upinzani nchini Zambia, Hakainde Hichilema, ameongoza katika matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais, uliofanyika tarehe 12 Agosti 2021, dhidi ya Edgar Lungu, anayetetea kiti hicho kwa muhula wa pili. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea ).

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa mapema leo Jumamosi, tarehe 14 Agosti 2021 na Tume ya Uchaguzi Zambia (ECZ), Hakainde aliyegombea kupitia Chama cha UPND, anaongoza kwa kura zaidi ya 60,000 dhidi ya Lungu.

Ambapo amepata 171,604, huku mpinzani wake wa karibu Lungu wa Chama Tawala cha Patriotic Front, akipata 110,178. Kura hizo ni matokeo ya majimbo 15 kati ya 156 ya Taifa hilo, lililoko Kusini mwa Afrika.

Wakati zoezi la kuhesabu kura likiendelea, kupitia ukurasa wake wa Twitter, Hakainde alitoa wito kwa watu wanaohesabu kura, kutenda haki wakati zoezi hilo linafanyika.

“Jua linapochomoza kwa ajili ya siku ya hatima ya Zambia, ujumbe wetu kwa wale wanaohusika na kuhesabu kura ni rahisi, haki. Haki pekee ndiyo mnayotakiwa kuifuata, ili mpate kuishi na kumiliki nchi ambayo Bwana Mungu wenu amewapa,’ ameandika Hakainde.

Wakati Hakainde akioa wito huo, Lungu kupitia ukurasa wake wa Twitter, alilalamika akidai kwamba mchakato wa uchaguzi huo haukuwa huru na wa haki.

Rais huyo wa Zambia anayemalzia muda wake, alitoa shutuma hizo baada ya mauaji ya Mwenyekiti wa chama chake katika Mkoa wa Kaskazini Magharibi, Jackson Kungo.

Lungu amedai wapinzani wake wameufanya uchaguzi huo kuwa vita, kufuatia mauaji ya Kungo.
Hii ni mara ya pili kwa miamba hao wa siasa nchini Zambia,kuchuana katika kinyang’anyiro cha urais.

Kwa mara ya kwanza, walichuana kwenye Uchaguzi Mkuu uliofanyika 2016, ambapo Lungu alitangazwa mshindi wa kiti hicho, baada ya kupata ushindi mwembamba dhidi ya Hakainde.

Screenshot_20210814-161239.jpg
 
Tunamtakia kila lililo jema ili atawale kwa haki kwa maendeleo ya Zambia na majirani zake.
 
Asante sana kwa taarifa hii, kwa chaguzi za Africa ni kawaida wapinzani kuongoza mwanzoni, matokeo ya maeneo ya mijini, sasa subiria matokeo ya vijijini na matokeo ya mwisho yatakayo tangazwa, utashangaa!.
P
 
Hakainde Hichilema... Atakuwa mchaga wa Machame Nkarungo au...? 🤔 :oops:
 
Asante sana kwa taarifa hii, kwa chaguzi za Africa ni kawaida wapinzani kuongoza, sasa subiria matokeo ya mwisho yatakayo tangazwa, utashangaa!.
P
Exactly mkuu hii ni cancer kwa chaguzi nyingi hapa Africa,President Lungu atashinda tena na kisa itakua kura za vijijini!na hizi tume za uchaguzi zote zinafanyaga hivi kwa chaguzi hapa dark continent.
 
Haiwezekani Malawi, Zambia, Botswana,, Ghana, Senegal, nk. Wabadilishane madaraka kupitia sanduku la kura! Halafu jambo hilo hilo lionekane kama ni dhambi kwa nchi kama Tanzania.
Kwa Tanzania sio dhambi bali ndio ukweli wenyewe.

P
 
Uchaguzi huu liwe fundisho kwa watanzania wanaodhulumiwa na serikali ya CCM lakini bado wameingangania.
Mkuu comment yako imenisitua mno, najiuliza nimekoment muda gani kumbe majina yanakaribia kufanana mkuu
 
Ingekuwa walau 90% ya kura zote hii Ingekuwa habari.

"This is not News!"
 
Asante sana kwa taarifa hii, kwa chaguzi za Africa ni kawaida wapinzani kuongoza mwanzoni, matokeo ya maeneo ya mijini, sasa subiria matokeo ya vijijini na matokeo ya mwisho yatakayo tangazwa, utashangaa!.
P
Kama ulikuwemo kwenye akili yangu Pascal Mayalla. Ni mapema mno kuongelea habari ya HH kuwa mshindi ktk uchaguzi huu. Lungu atafanya yake kwenye majimbo yaliyobakia mpk watu washangae.
 
Kwa Tanzania sio dhambi bali ndio ukweli wenyewe.

P
Ukweli wa kubaka uchaguzi kama alivyofanya mwendazake 2020?
 
Huyo ni Muwemba asilia, nakumbuka sekondari kulikuwepo na mwalimu kutoka Zambia akijulikana kwa jina la; Kachingwe Kaselenge.
Hapana..HH ni mtonga from southern province of Lusaka central..kabila kubwa lenye utajiri wa Ng,ombe .Mwalimu Kachingwe Kaserenge of Mwanalugali school ni mmambwe wa south Lake Tanganyika. Huyu bila shaka ametokea border ya Mbala na Sumbawanga.
 
Asante sana kwa taarifa hii, kwa chaguzi za Africa ni kawaida wapinzani kuongoza mwanzoni, matokeo ya maeneo ya mijini, sasa subiria matokeo ya vijijini na matokeo ya mwisho yatakayo tangazwa, utashangaa!.
P
Vipi huko, kura za vijijini zinasemaje?
Bado huamini kuwa vyama tawala vimechokwa mjini na vijijini?
Bado umekariri?
 
Back
Top Bottom