Uchaguzi wanukia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi wanukia

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by mshairi.mtangan, Jun 16, 2009.

 1. m

  mshairi.mtangan New Member

  #1
  Jun 16, 2009
  Joined: Nov 12, 2008
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zichungeni shilingi,bajeti inazotoa,
  Matapeli wako wengi, wanazifuatilia,
  Msibumbwawe kwa wingi,tumboni zitaishia,
  Na kitakachobakia, uchaguzi wanukia!

  Twabeba nizigo mingi, hakuna wa kutuhurumia,
  Anzia na mashangingi,mitaani yakizagaa,
  Hayaingizi shilingi, bali zinaangamia,
  Na kitakachobakia, uchaguzi wanukia!

  Chungeni kila shilingi, sasa itakayoingia,
  Na wekeni na vigingi, kila watakayoitoa,
  Udhbiti ni msingi, fedha vema kutumia,
  Na kitakachobakia, uchaguzi wanukia!

  Kwa sasa walaji wengi,waletaji wapungua,
  Mezani msongemangi, wanajua kutumia,
  Bongo zao hazigongi, vipi nasi tutajaa,
  Na kinachobakia, uchaguzi wanukia !

  mshairi
   
 2. S

  Sammy Sr. Member

  #2
  Jun 17, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uchaguzi wanukia

  Haya, haya nyie wenye njaa,
  Uchaguzi unanukia,
  Kaa mkao wa kufaa,
  Wamwagaji waingia!

  Matajiri wenye njaa,
  Kofia mbili kuvaa,
  Wasioishiwa tamaa,
  Hadi mauti kuingia!

  Wanakuja kuzinunua,
  Shahada mtazopewa,
  Hesabu wajipangia,
  Kila mtu kumnunua.

  Haya, haya wenye njaa,
  Mnaotaka kuvaa,
  Kanga, vitenge mtapewa,
  Mradi utu wenu kuua!

  Haya, haya wenye njaa,
  Pombe mnaozitumia,
  Mtakunywa na kukojoa,
  Mradi makuwadi kuwa!

  Haya, haya wenye njaa,
  Mtageuzwa dagaa,
  Funika kombe mkiwa,
  Kafiri kukusafiria!

  Moja mnayochukua,
  Milioni yeye hutwaa,
  Miaka kumi kitmia,
  Wenye njaa mwajifia!

  Au wazee mmekuwa,
  Hamna mnayemfaa,
  Wawaache kwenye mataa,
  Nyuma, mbele hamtojua!

  Nani kakuambia,
  Mtu huyu anafaa?
  Wewe umemwangalia,
  Vizuri ukamchungua ?

  Uoza mkichagua,
  Na nchi hujiozea,
  Wazinzi mkiteua,
  Nanyi mwafa kwa zinaa!

  Na Mungu huhuruhimia,
  Wale wanaojihurumia,
  Afueni huwapatia,
  Juhudini wanaokaa!

  Vinginevyo mnapewa,
  Yule tu anayewafaa,
  Hata punguani akiwa,
  Nyie bado mtamsifia!

  Kuna siku atawaambia,
  Sumu ni dawa muruwa,
  Mtakunywa mtajiua
  Na yeye atabakia!

  Vipi unaaminia,
  Mwingine kukufikiria,
  Akilini linaingia,
  Hili kweli kuwa likawa?

  Si chama ninakwambia,
  Wala mtu pia kuwa,
  Kila mmoja na yake njaa,
  Yako hatoiangalia!

  Nadra atakayekufaa,
  Kwa kura yako kununua,
  Chambua tena chaambua,
  Chama cha kukipigia!

  Wenye udini kataa,
  Mkiristo akiwa
  Na Mwislamu naye pia,
  Rwanda wanatutakia,
  Na baa na mabalaa!

  Lila na fila tambua,
  Ya Mungu kutanzua,
  Kaizari kumwachia,
  Yale anayostahilia!

  Viongozi wamepotea,
  Dini wanazichezea,
  Na watakaokujalia
  Ni sisi Watanzania!
   
Loading...