singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
Nchi nyingi zimeingia kwenye machafuko baada ya uchaguzi Mkuu wa nchi husika. Hii ni kutokana na hulka ya kibinadamu kuwa anayeshindwa hakubali kushindwa na anayeshinda humkejeli aliyeshindwa. Siasa za nchi si sawa na upinzani wa Simba na Yanga. Siasa ndiyo hutoa mustakabali wa taifa husika. Siasa ikienda fyongo, hakuna kitakachonoga.
Tunapoelekea kwenye Uchaguzi wa Zanzibar ambao umepangwa kufanyika Machi 20, mazingira ya uchaguzi huo si mazuri. CCM wamejipanga kisawasawa kushiriki uchaguzi huo. Chama Kikuu cha upinzani CUF wamejipanga kisawasawa kususia uchaguzi huo. Hapa CUF wamehiari kuwa nje ya siasa za Zanzibar kwa miaka 5 ijayo. Haijajulikana ni aina gani ya siasa watakayoshiriki hasa kutokana na kuwa nje ya serikali na bunge. CCM itakuwa inajitanua katika maeneo yote kwa asilimia 100. Uwakilishi pekee wa CUF ni kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambako naamini ndiko CUF watakakopenyezea mambo yao.
Wito wangu kwa Wazanzibari ni kwamba, ZEC wametangaza tarehe ya Uchaguzi. Hakuna chombo chenye mamlaka ya kutengua maamuzi hayo ya ZEC isipokuwa ZEC wenyewe. Waliotangaza kushiriki naamini kuwa wamefanya hivyo bila ya shinikizo kutoka upande wowote. Na wale waliosusia, naamini kuwa wamefanya hivyo bila ya kushawishiwa na upande wowote. Kutokana na hali hiyo, nawaasa pande zote kuwa watakaoshiriki uchaguzi huo washiriki kwa amani na wanaosusia wasusie kwa amani. Fanyeni mfanyayo ila mtuachie amani yetu. Amiri Jeshi Mkuu ametangaza kuimarisha amani na utulivu kote nchini. Ni wajibu wetu kujiepusha na yale yatakayovuruga amani yetu.