Uchaguzi 2020 Uchaguzi wa wazi na haki kama CCM maoni, ungetutibu sote

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,811
35,802
Amani ya nchi hii ilikuwa ya thamani mno kiasi kumtaka kila mmoja wetu kufanya yote yawezekanayo kuhakikisha kuwa hatutetereki lilikuwa si jambo la kupuuzwa.

Tume kwa kuendesha uchaguzi wa wazi na wa haki tu kungefanya mamlaka zote (hasa za kutumia mabavu) kubakia likizo.

Walishindwa waziwazi kina Makonda kina Pascal Mayalla, Katambi, Mwakyembe nk kwenye kura za maoni kiroho safi, wala hakukuwa na kelele wala msuguano.

Tume nendeni "the remaining extra mile" kwa mustakabala wa amani yetu. "It is never too late."

Bado mnaweza kukubaliana na vyama hivi namna iliyo bora zaidi tunayoweza kukubaliana na kuaminiana sote.

Sisi sote ni ndugu. Tunaweza fanya uchaguzi kindugu kwa kuhakikisha uwazi na haki tu.

Eeh mola wetu ukatujalie busara kidogo kutuepusha na dhoruba hili la wazi linalotunyemelea.
 
Kuwa fair tu, kinachoombwa ni kidogo sana:

"Tujiridhishe sote kuwa uchaguzi huu ni huru na wa haki. Uwazi uliotumika na CCM kwenye kura zao za maoni ni mwalimu mzuri mno."

Kama kuwapo nje ya 100m kutawafanya wapiga kura kujiridhisha kuwa pana haki imetendeka kwanini iwe haramu?

Bila hivyo wana JF, binafsi natangulia kuaga:
 
NEC watoe nakala za matokeo kwa mawakala kwenye kila kituo. Kipindi hiki Lisu anashinda asubuhi na mapema tu.

Sijapanda daraja mwaka wa 7 huu kazini. Nahitaji Rais atakayeheshimu Haki, Uhuru na Sheria.

Kama kuhesabu pesa hata kama ni10m/- hakuwezi kuchukua masaa 2, basi kuhesabu kura zisizofika 200,000 kwenye kituo kimoja hakuwezi kuchukua masaa 2.

Matokeo yatangazwe mbele ya hadhara kituo kwa kituo punde tu baada ya kumaliza kuhesabu.

Kusiwe na visingizio vyovyote vya ucheleweshaji.
 
Amani ya nchi hii ilikuwa ya thamani mno kiasi kumtaka kila mmoja wetu kufanya yote yawezekanayo kuhakikisha kuwa hatutetereki lilikuwa si jambo la kupuuzwa...
Wapinzania watauza nchi. Tusifanye makosa Oktoba 28. Chagua Magufuli ✅
 
Kuwa fair tu, kinachoombwa ni kidogo sana:

"Tujiridhishe sote kuwa uchaguzi huu ni huru na wa haki. Uwazi uliotumika na CCM kwenye kura zao za maoni ni mwalimu mzuri mno."....
Mkuu unaenda wapi Kama watz bado tunakuitaji mkuu tafadhali
 
Mkuu unaenda wapi Kama watz bado tunakuitaji mkuu tafadhali

Mkuu kwani hata ni kutaka kwenda mahali? Mtu anayepanga kupindisha haki ana nia ya kuwafanya wengine waidai.

Nina uhakika nitakuwapo Tahrir square baada ya ctct 28 pamoja na vitisho vyao. Si kwa kulazimishwa na mtu bali kupinga ghiliba na uchaguzi huu. Solo peke yangu na hatuko wachache.

Tulirudi salama JKNIA pia kutoka kiluvya. Sina hakika Oct 28 itakuwa vipi kwani pana watu wanaonekana kuwa na nia ovu sana na huu uchaguzi.

Kwanini haki haitakiwi kuhakikishwa? Ni maajabu ya Firauni.
 
Mkuu kwani hata ni kutaka kwenda mahali? Mtu anayepanga kupindisha haki ana nia ya kuwafanya wengine waidai..
Mkuu hiki ni kipindi kigumu ,japo watu wanakichukulia poa,na nashangaa Sana, lazima nec ,na baadhi ya vyombo vyetu nyeti kufanya mahamuzi magum,yasioangalia sura,cheo,Wala matakwa ya mtu Bali kuangalia tz kwanza kwa haya yafuatayo:

1. kuanza Sasa mchezo wowote wa chama kimoja kutaka kuhujum chama kingine kwa mbinu chafu wakemee bila kuangalia mtu.

2. Kura Sasa, vituo vyote 81 na point ziesabiwe wazi chini ya mawakala wa vyama nakutoa nakala ya matokeo kwa ushaidi wa badae ili apatikane mchawi Kama Kuna malalamiko.

3. wapo watu wanatanganza maneno mabaya Sana majukuani,kisa viongozi na yakutisha sijui sindano fyuu,wachukuliwe hatua bila kujali ni Nani, Tanzania kwanza.

4. kusimamia mshindi wa chama chochote kwa ushindi halali anatangazwa, Tanzania kwanza

Mwisho
Hatuna sababu yakuingiza mgogoro wa nchi kisa uchaguzi,wakati siku zipo,wazee mpo,na njia za kuepuka fika huko zipo wazi Kama nilivyobainisha hapo juu, why??? Haya ni Mambo muhim kikilipuka hapa hakiangalii we unachama au huna chama wote ni waanga ,mama zetu,baba zetu, Bibi zetu huko vijijini wapo pia,
 
Mkuu hiki ni kipindi kigumu ,japo watu wanakichukulia poa,na nashangaa Sana, lazima nec ,na baadhi ya vyombo vyetu nyeti kufanya mahamuzi magum,yasioangalia sura,cheo,Wala matakwa ya mtu Bali kuangalia tz kwanza kwa haya yafuatayo:
Mkuu umeandika mambo mazito sana. Umenisoma kuchukua muda kutafakari zaidi.

Sababu ipi ya kuliingiza taifa kwenye dhahama? Sababu hiyo haipo! Kila mtu na aachwe ashinde mechi zake na tutapita kipindi hiki salama.

Wagombea wote ni wana wa nchi hii. Hayupo mmoja mwenye kujifanya yeye ndiye mzalendo zaidi. Mgombea mmoja asijifanye yeye ndiye anatupenda sana.

Chema chajiuza mbona chajiuza?

ZEC muda bado upo tafrani hii ya 27 na 28 tuimaluze sasa, vinginevyo kama mnataka kututumbukiza matatizoni tu.

Kwanini kama mnataka siku tofauti basi yote ya ZEC yasifanyike na kwisha 27 na ya NEC yasifanyike na kwisha 28? Kwa nini mnalazimisha? Kwanini msiwasikilize wananchi, wapiga kura na vyama vinasema je? Busara nayo je?

Sababu zenu za wana usalama kupiga 27 kwa Zanzibar kwa ZEC hali bado watapiga tena 28 kwa NEC ni jambo la kukemewa.

Mko wapi viongozi wa dini? Mko wapi wenye busara zenu? Mko wapi wenye dhamana?
 
Ajabu na kweli ni kuwa kuna watu wakisikia au kuona title zinazozungumzia uchaguzi huru na wa haki wanafura kwa hasira.

Kwa nini hawataki uwazi kama uliomnyoosha gwa'jima, Pascal Mayalla,, makonda, silinde au hata Mwakyembe?
 
Tume ishirikiane na vyama vyote ione namna ya kuufanya uchaguzi ule huru na haki. Ili kulinda amani yetu.

Kura zipigwe wazi uwanjani na zihesabiwe wazi uwanjani kila mtu aone zoezi la kura yake inavyohesabika ili haki itendeke, panapo haki mgombea yeyeto atakaeleta vurugu kwa kushindwa kihalali tutamdhibiti sisi wenyewe wananchi.

Wakurugenzi msipindishe haki mkajiponza wenyewe au familia zenu.
 
Back
Top Bottom