Uchaguzi wa Umeya Mwanza leo: CHADEMA yateua wagombea wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi wa Umeya Mwanza leo: CHADEMA yateua wagombea wake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by n00b, Sep 28, 2012.

 1. n00b

  n00b JF-Expert Member

  #1
  Sep 28, 2012
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 952
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 60
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


  KAMATI za Utendaji za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Wilaya ya Nyamagana na Ilemela katika vikao tofauti kwa kushirikiana na kamati za madiwani katika kila wilaya husika, zimekamilisha mchakato wa kupata wagombea wa nafasi za umeya na naibu meya, Halmashauri ya Jijila Mwanza na Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.

  Kamati ya Utendaji ya Wilaya pamoja na madiwani wa CHADEMA Wilaya ya Nyamagana walimteua aliyekuwa Naibu Meya kabla, Diwani waKata ya Maina, Charles Chibara kuwa mgombea wa Umeya Halmashauri ya Jiji laMwanza.

  Kwa upande wa Ilemela, kikao cha Kamati ya Utendaji pamoja na madiwani wa wilaya hiyo walimteua Diwani wa Kata ya Nyamanoro, Abubakar Kapera kuwa mgombea wa Umeya Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.

  Kikao hicho cha Utendaji na madiwani wa CHADEMAWilaya ya Ilemela, pia kilimteua Diwani wa Kirumba, Danny Kahungu kuwa mgombea wa nafasi ya Unaibu Meya Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.

  Vikao hivyo tofauti vya uchaguzi vilivyoketi kwa mujibu wa katiba, kanuni na taratibu za chama chini ya usimamizi wa Ofisi yaKatibu Mkuu wa CHADEMA, vilihusisha wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Wilaya na madiwani katika eneo husika.

  Itakumbukwa kuwa katika kutafuta namna bora ya kusimamia vyema utendaji wa chama katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza ambayo ilikuwa ni halmashauri pekee nchini iliyokuwa ikihusisha wilaya mbili, yaani Nyamagana na Ilemela, Baraza Kuu la CHADEMA liliamua kuwa masuala yote yanayohusu jiji hilo yasimamiwe na Ofisi ya Katibu Mkuu.

  Utekelezaji wa maamuzi hayo ya kikatiba, ulianza siku nyingi, ikiwemo kusimamia uchaguzi wa Meya wa Jiji la Mwanza mapema baadaya uchaguzi mkuu mwaka 2010.

  Wakati huo huo Kamati ya Utendaji ya Wilaya Nyamagana imekubali kumwachia kugombea nafasi ya Unaibu Meya wa Halmashauri ya Jijila Mwanza, Diwani wa Mirongo Daudi Mkama, katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Septemba 28, 2012.

  Aidha, kutokana na vurugu zilizosababishwa na kundi la watu waliovamia na kuvuruga kikao cha uteuzi wa mgombea wa Umeya na Naibu Meya wa Manispaa ya Ilemela hivi karibuni, uongozi wa CHADEMA Wilaya umefungua kesi polisi kwa jalada lenye namba MZN/RB/8226/2012, kwa ajili ya hatua za kisheria.

  Imetolewa na Ofisa Habari wa CHADEMA

  Septemba 27, 2012,
  Dar es Salaam

   
 2. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #2
  Sep 28, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,515
  Likes Received: 1,685
  Trophy Points: 280
  Huyo anayegombea unaibu meya mwanza ni wa chadema?
   
 3. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #3
  Sep 28, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo Chadema na CUF wamefunga ndoa Mwanza.
   
 4. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #4
  Sep 28, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kama angekuwa CDM, wasingetumia neno "wamemwachia" kugombea.
   
 5. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #5
  Sep 28, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,142
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  Nimesikia kuwa Jiji la mwanza limegawanywa na kupata halimashauri mbili tofauti. Halimashauri moja Itakuwa ya ILEMELA Na ya pili itakuwa ya NYAMAGANA. Leo ni uchagzi wa viongozi wa halimashauri hizo, naona wapiganaji wako mkao wa kazi.

  Naomba MUNGU haki itendeke ili kuepuka umwagikaji wa damu.
   
 6. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #6
  Sep 28, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  sioni tatizo, siasa ni maelewano jamani,

   
 7. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #7
  Sep 28, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Leo hii mkuu?
   
 8. h

  hans79 JF-Expert Member

  #8
  Sep 28, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Kumwachia sio mseto au ndoa, we vp mbona upo kimagumashi zaidi?
   
 9. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #9
  Sep 28, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  chezeya mtaji weye?
   
 10. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #10
  Sep 28, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Hivi wewe unadhani sie watoto? Wamemuachia wapi Chadema na Cuf wamefanya makubaliano, wakatae kuwapa CUF Naibu Meya waone kama Meya hajatoka CCM.
   
 11. O

  Original JF-Expert Member

  #11
  Sep 28, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 326
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Chadema kamwe hawawezi kushirikiana cuf.
   
 12. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #12
  Sep 28, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,152
  Likes Received: 1,248
  Trophy Points: 280
  Strategies mkuu, si unajua kila kitu kujipanga kwa akili
   
 13. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #13
  Sep 28, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Katika siku ya leo ya tarehe 28 septemba 2012 panafanyika uchaguzi wa meya wa halmashauri ya jiji la mwanza na ilemela.

  Katika chaguzi ya halmashauri ya jiji la mwanza CDM wamemuweka mgombea wa Meya na kukubaliana na Cuf kuwaachia nafasi ya unaibu meya kwa ndg. Daudi Mkama. Hii yote ni kwa ajili yakupata kura za madiwani wa Cuf ili CDM iweze kushinda kwani bila hivyo kwa idadi ya madiwani wa CDM katu hawawezi kushinda. Mlisikia kuna uzi jana ulipita kwa Dr slaa kuonekana mwanza, nia na madhumuni hasa ya ujio huu ni kuweka makubaliano na Cuf yakuachiana nafasi hizo ili CDM iweze kushida, kwa kifupi twaweza sema kufunga ndoa.

  Kwa mintarafu hii basi, yaonyesha wazi cdm na cuf wamefunga ndoa , sasa swali la kujiuliza ndoa hii ni ya dhati yakutoka moyoni au ni ya kimagumashi? kwani tumesikia kauli nyingi za cdm wakiituhumu cuf kuwa ni ccm b nk
   
 14. C

  CUF Ngangari JF-Expert Member

  #14
  Sep 28, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 273
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  uchaguzi umeishamalizika meya katoka CCM na naibu meya katoka CUF.
   
 15. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #15
  Sep 28, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Ukiona hivyo ujue Ritz analia kiutu uzima kwakuwa magamba walikuwa wamemuahidi pepo diwani wa mirongo lakini baada ya Chadema kushitukia chezo na kumuachia nafasi ya unaibu meya wamebaki wanalia na kusaga meno.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #16
  Sep 28, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Vipi umepata matokeo ya Meya Nyamagana? Kama umepata naomba uni-PM.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...