Uchaguzi wa ufaransa: Somo kwa tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi wa ufaransa: Somo kwa tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mark Francis, May 10, 2012.

 1. Mark Francis

  Mark Francis Verified User

  #1
  May 10, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 605
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tarehe 6/5/2012 Jumapili iliyopita, watu wa Ufaransa walifanya uchaguzi wao ambao tulishuhudia ukimfanya François Gérard Georges Hollande (Socialist Party) kuwa Rais wa 24 wa Ufaransa tokea mwaka 1848 ambapo Napoleon III alikua Rais wa kwanza. Uchaguzi huo ambao ulikua na ushindani mkubwa kati ya Hollande na Sarkozy ulimalizika salama kwa Sarkozy kukubali kushindwa na kumpongeza mshindi.

  Mojawapo ya sifa za Hollande ni kuwa aliachana na mkewe Segolene Royal mnamo mwezi Juni 2007, hana uzoefu na siasa za kimataifa na hivyo hana umaarufu kimataifa na pia hajawahi kukaa katika ofisi za serikali. Kutokana na uchaguzi huo, Watanzania tunaweza kujifunza yafuatayo;


  1. Kuheshimu demokrasia kunaepusha nchi na machafuko na vifo visivyo vya lazima. Tumeshuhudia katika nchi yetu machafuko ambayo yalisababisha vifo katika chaguzi mbalimbali tokea mwaka 1995 kutokana na matumizi ya mabavu kwa lengo la kuwaweka watu wasiopendwa na wananchi. Tukijifunze kutoka Ufaransa ambao wamemchagua wanaempenda bila kuingiliwa na mtu yeyote na wale wachache ambao mtu wao hajachaguliwa wameheshimu maamuzi ya wengi.
  2. Kutokua na mke sio sababu ya mtu kukosa urais. Hollande kachaguliwa kuwa Rais wa Ufaransa akiwa hana mke kufuatia kuachana na mke wake tokea mwaka 2007. Kwa hapa Tanzania mtu asipokua na mke anachukuliwa kama mtu asiefaa wakati kazi ya Urais haina uhusiano wowote na kuwa au kutokua na mke au kuvunjika kwa ndoa.
  3. Kutokua na uzoefu na siasa za kimataifa sio kigezo cha kumnyima mtu nafasi ya kuwa Rais wa nchi yetu. Hollande kachaguliwa akiwa hana uzoefu za siasa za kimataifa, lakini kaaminiwa na kapewa nchi kuongoza. Hapa kwetu, mtu kama Dr. Slaa hakuaminika kwa baadhi ya watu kwa sababu hana uzoefu za kimataifa kitu ambacho hakina uhusiano na uongozi wa nchi.
  4. Kutokuwahi kufanya kazi katika ofisi za serikali hakumzuii mtu kuwa Rais wa Tanzania. Imekua ni kawaida kwa nchi yetu kwa viongozi kuwa na uzoefu mkubwa serikalini na ndipo wapate Urais, isipokua kwa hayati Mwl. Nyerere, hicho sio kigezo sahihi na ndio maana tunaishia kupata viongozi wasio bora. Tunajifunza sasa kuwa hata wasiokuwa na uzoefu na ofisi za serikali wapewe urais kwa sababu wanaweza kuwa na mchango mkubwa wa mawazo kuliko hao walio na uzoefu na ofisi za serikali.

  Hayo ni baadhi tu ya yale tunayoweza kujifunza kutokana na uchaguzi huo wa Jumapili iliyopita. Kwa waliofatilia uchaguzi huo wanakaribishwa kuongeza mengine ambayo Watanzania tunaweza kujifunza kutokana na uchaguzi huo.
   
Loading...