Uchaguzi wa Udiwani Kata 16......... Upinzani 1 CCM 0

Zitto

Former MP Kigoma Urban
Mar 2, 2007
1,562
10,879
Kama mnavyofahamu hivi sasa kampeni za uchaguzi wa udiwani zinaendelea nchi nzima. Chaguzi hizi ndogo zinatokana na waliokuwa wakishikilia viti hivo ama kufariki dunia au kupoteza sifa za uanachama wa vyama vilivyowadhamini.

Wakati siku ya uchaguzi ni tarehe 28 oct tayari kambi ya upinzani imekwisha weka kibindoni kiti kimoja katika Kata ya Nankukwe, halmashauri ya Wilaya ya Chunya kule Mbeya.

CCM walikosa mgombea katika hiyo baada ya wananchi kuona kuwa hata wakigombea watashindwa tu. Mpaka ilipofika saa kumi jioni ya tarehe 2 Oct, mgombea wa upinzani Bwana Lula ndie alikuwa mgombea pekee aliwasilisha fomu za utezui na hivyo kutangazwa kuwa Diwani wa kata hiyo...........

Hii ni habari njema sana kwa wapenda mabadiliko wote nchi hii. Kama CCM wameshindwa kupata mgombea wa udiwani, chama chenye mtandao nchi nzima, tusubiri tuone Ubunge 2010.........

http://ippmedia.com/ipp/nipashe/2007/10/11/100215.html
 
Binafsi nadhani wapinzani wanaweza kabisa kuzoa zaidi ya nusu ya viti vinavyogombewa ili kuionesha CCM kuwa watu hawatanii...
 
Mhe. Zitto naungana na wewe kufurahia habari hiyo, lakini sikubaliani kwamba hicho ni kipimo kizuri cha kutambua uwezo wa mageuzi kijamii. Nadhani kipimo kizuri ni kwa wagombea wote kujitokeza na kuruhusu demokrasia ya walio wengi kuchukua nafasi yake. Huo ndio ushindi wa heshima ambao mwisho wa siku hauna visingizio.

Ukweli siasa nchini imeanza kubadilika na wananchi wanatambua nini wanachokihitaji, lakini ni vema uelewa huo ujidhihirishe kwa kura ya wazi. Na hii itawafundisha 'watawala wa kudumu' kuwa sasa upepo umebadilika maana hata sasa hawana habari!
 
nina uhakika hawa wazwagi hawatashinda hata kata moja,ndio maana vikao vya CC havikatiki,nasikia wanampango wa kununua wapiga kura ili kuonesha chama bado kimeshika hatamu..
nawasihi tena na tena wana wa Watanzania msiwachague hawa Mafisadi na wanaotetea Rushwa.atakayekupa pesa ili umchague muweke hadharani
 
Mhe. Zitto naungana na wewe kufurahia habari hiyo, lakini sikubaliani kwamba hicho ni kipimo kizuri cha kutambua uwezo wa mageuzi kijamii. Nadhani kipimo kizuri ni kwa wagombea wote kujitokeza na kuruhusu demokrasia ya walio wengi kuchukua nafasi yake. Huo ndio ushindi wa heshima ambao mwisho wa siku hauna visingizio.

Ukweli siasa nchini imeanza kubadilika na wananchi wanatambua nini wanachokihitaji, lakini ni vema uelewa huo ujidhihirishe kwa kura ya wazi. Na hii itawafundisha 'watawala wa kudumu' kuwa sasa upepo umebadilika maana hata sasa hawana habari!

Kalumanzira (sio kalimanzira)

Mwaka 2005, CCM ilishinda bila kupingwa viti 9 vya Ubunge. Mwaka 2000 walishinda viti 20. Mchakato wa demokrasia ni pamoja na kupita bila kupingwa. Nchini Uingereza na Canada, kuna historia ya maspika wa bunge ambao wameongoza vikao vya Bunge bila ya upendeleo wa kisiasa kuachiwa viti vyao bila kupingwa.

Jambo la Msingi hapa ni kuwa CCM, chama chenye mtandao mkubwa kimeshindwa kupata mgombea udiwani Chunya! Narudia Chunya!

MwanaKijiji,
Tumegawana Kata kwa vyama. Tunajitahidi kuhakikisha kuwa tunahinda Kata nyingi tuwezavyo. CHADEMA mpaka sasa imejiweka vizuri sana katika Kata 4- Majengo-Songea, Katazi, Kabwe na Namanyere kule Rukwa. TLP wameshapata kiti kimoja na wana uhakika wa kushinda kule Moshi Vijijini na Arusha. CUF wana uhakika wa kushinda kule Tunduru katika kata moja. Tunaweza kupata kata kumi. Tunajitahidi
 
CUF wana uhakika wa kushinda kule Tunduru katika kata moja. Tunaweza kupata kata kumi. Tunajitahidi

Wilayani Lushoto Tanga, CUF wana madiwani wengi pia. Nadhani wakitumia vyema turufu hii, basi wapinzani wanaweza kufanya maajabu zaidi ifikapo mwaka 2010.
 
Mhe. Nashukuru kwanza kwa 'kupendezesha' jina langu, nimeamini kweli wewe ni 'mbantu' wa kweli. Pili sikatai wazo la mgombea kupita bila kupingwa, wasiwasi wangu ni kwa ccm kuja baadaye kudai kuwa hawakuona sababu ya kuweka mtu! Hoja hiyo unaweza kuona ya kitoto lakini kwa mwananchi wa kawaida anaweza kudhani ni hoja.

Ukifuatilia hoja zao (maana wewe unawajua zaidi) mara nyingi hazivuki mipaka ya masikio ya tafakari, na wanaelewa kuwa hiyo ndiyo lugha ya kuongea na 'watanzania' wakaeleweka.
 
Yaani ccm imekoswa mgombea wa udiwani,it looks like a joke,but it sounds very good to me,leo nitapata usingizi mnono maana hizi ni dalili njema za kushinda vitani.Lakini bado nahofia je huu uchaguzi hautafanyiwa mizengwe,maana i know these nyang'aus(ccm) can invest billions of money ili wapate hivi viti,ni wasiwasi sana na hilo.
Ingelikua jambo la mbolea kama viti vyote vingeenda upinzania,halafu ccm ipate zero(0).
 
I like this statement.................Upinzani 1 CCM 0............now guys you are talking....keep on good spirit ya umoja

Nakubaliana na Mh. Zitto.............i mean, it can be any other place......but Chunya is something else....lazima Upinzani wafurahie
 
Kabla hujaweza kushinda vikubwa lazima ushinde vidogo! Ndiyo maana timu yetu ya Taifa ikicheza na vitimu vidogo vidogo ikihangaika tunajua hata kuwa kwa kubwa itahenya! Katika mapambano ya vita kabla hujaichukua Baghdad, lazima uanze pembezoni mwake!! Tatizo linakuja ukiichukua Baghdad utaweza kuitawala?
 
Zitto,

Mbona mnakuwa vigeugeu? upande mmoja mnapinga uchaguzi upande mwingine mnakubali ushindi wa chee!

Inaelekea zile juhudi za kupinga uchaguzi mmeziacha maana sasa mpo ktk kampeni! usanii wa upande wa ushindani huu.

Mwaka huu tutaona vituko vingi tu.
 
Masatu

Kinachoongelewa hapa ni kwamba bao tayari limeisha ingia zidi ya chama tawala. Ukiona unaanza kukosa wangombea nawe ndiye mtawala ujue umekwisha. Kwa maana rahisi huko hawana lao. Tusubiri tena ubunge kuanzia Bongo mwaka 2010 wataanza kukimbia wenyewe.Nawashauri hata mawaziri wakagombee mikoani maana aibu ya ufisadi/Buzwagi wataiweka wapi? Aibu tu.

Maana CCM wanachemsha mafuta na kujikaanga wenyewe wakisaidiwa na mwenyekiti wao anyeongoza jahazi la kujikaanga.
 
Zitto,

Mbona mnakuwa vigeugeu? upande mmoja mnapinga uchaguzi upande mwingine mnakubali ushindi wa chee!

Inaelekea zile juhudi za kupinga uchaguzi mmeziacha maana sasa mpo ktk kampeni! usanii wa upande wa ushindani huu.

Mwaka huu tutaona vituko vingi tu.

Linywe hilo chloroquin bila maji tumia soda maana ni hatari tulikuwa hatukuzoea haya. Ndipo serikali ya JK na wasanii wenzake walipotufikisha. Ukivaa kandambili zikianza kukatika katika unatupa na kununua mpya.
 
Kabla hujaweza kushinda vikubwa lazima ushinde vidogo! Ndiyo maana timu yetu ya Taifa ikicheza na vitimu vidogo vidogo ikihangaika tunajua hata kuwa kwa kubwa itahenya! Katika mapambano ya vita kabla hujaichukua Baghdad, lazima uanze pembezoni mwake!! Tatizo linakuja ukiichukua Baghdad utaweza kuitawala?

Mkjj,
Hapo sasa ndio inabidi uwe "prince" aliyesoma historia na kuielewa.
Anywayz upinzani/wanamabadiliko wanahitaji hizo diwani nyingi, siku itakapoanza miji yetu kuwa na mameya ambao si CCM basi ujue mwisho wao ndio umefika!!!!!. Bwana Buraza K, ushindi ni ushindi uwe wa kuchaguliwa au wakuteuliwa....wanaweza kuspin vyovyote watakavyo lakini mwisho wa siku "sie" tunajua kwamba ni wao ndio wameweka mpira kwapani, ligwaride limewashinda huko Chunya!!!!!.
 
Zitto,

Mbona mnakuwa vigeugeu? upande mmoja mnapinga uchaguzi upande mwingine mnakubali ushindi wa chee!

Inaelekea zile juhudi za kupinga uchaguzi mmeziacha maana sasa mpo ktk kampeni! usanii wa upande wa ushindani huu.

Mwaka huu tutaona vituko vingi tu.

'satu,
Hamna ambiguty hapo bro!!!!!! wewe mwenyewe tu unaji-mix kwa makusudi.......tuliza misuli na jaribu kuelewa nini hoja hapa, kukurahisishia ni kwamba "CCM WAMEANZA KUKOSA WATU WA........" unaweza kumalizia.
 
wanaweza kuspin vyovyote watakavyo lakini mwisho wa siku "sie" tunajua kwamba ni wao ndio wameweka mpira kwapani, ligwaride limewashinda huko Chunya!!!!!.

YIM, wenzako wako mahakamani wanasimamisha uchaguzi sasa sijui nani anaweka mpira kwapani hapo!

Mpira dk 90 umepata goli dk ya kwanza unaanza ngebe! tusubiri dk 90 au 120 if not penalt shoot out tuone who has the last laugh

Teh teh teh..
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom