Uchaguzi wa Udiwani Kata 16......... Upinzani 1 CCM 0

Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Jul 5, 2007
5,192
0
YIM, wenzako wako mahakamani wanasimamisha uchaguzi sasa sijui nani anaweka mpira kwapani hapo!

Mpira dk 90 umepata goli dk ya kwanza unaanza ngebe! tusubiri dk 90 au 120 if not penalt shoot out tuone who has the last laugh

Teh teh teh..

inaonekana kimekuuma sana kukosa mgombea kwenye udiwani..

mwaka huu utakula nyembe kwa hasira na wivu...

kwi kwi kwi kwikiiiiii kwi
 

Msanii

JF-Expert Member
Jul 4, 2007
8,670
2,000
.... Mpaka ilipofika saa kumi jioni ya tarehe 2 Oct, mgombea wa upinzani Bwana Lula ndie alikuwa mgombea pekee aliwasilisha fomu za utezui na hivyo kutangazwa kuwa Diwani wa kata hiyo...........

Hii ni habari njema sana kwa wapenda mabadiliko wote nchi hii. Kama CCM wameshindwa kupata mgombea wa udiwani, chama chenye mtandao nchi nzima, tusubiri tuone Ubunge 2010.........

http://ippmedia.com/ipp/nipashe/2007/10/11/100215.html

Zitto
Naungana na wapenda mabadiliko wenzangu kwa kutoa mkono wa pongezi za ushindi. Naamini kuwa kama vyama vingi vitaendelea kuonesha uaminifu ktk nafasi hizi, sisi wapiga kura tutawaamini zaidi in next term ktk nafasi kubwa zaidi maana tuliowaamini wametukoma nyani giladi.

kuhusu 2010 natoa rai kuwa kazi ianze sasa kusaka kura maana mkingojea kipindi cha kampeni itakuwa vurugu maana nyie hamna magari yenye bendera za serikali kwa ajili ya kampeni zenu. haya mambo ya BOT, Buzwagi, orodha ya mafisadi yawe practicle zaidi kwani yanaongeza crediti ktk account ya uaminifu.

Tanzania bila CCM inawezekana.
 

YournameisMINE

JF-Expert Member
Aug 29, 2007
2,247
1,225
YIM, wenzako wako mahakamani wanasimamisha uchaguzi sasa sijui nani anaweka mpira kwapani hapo!

Mpira dk 90 umepata goli dk ya kwanza unaanza ngebe! tusubiri dk 90 au 120 if not penalt shoot out tuone who has the last laugh

Teh teh teh..

'satu
Kuomba kuharisha tarehe ya mchezo ni tofauti na kutotokea uwanjani, Kwani goli la msumbiji lilifungwa dakika ya ngapi pale 'uwanja mpya'??Msee huo ni mmomonyoko kwa upande wenu, kwani ni lini mara ya mwisho sisiemu ilikosa mgombea wa udiwani?
 

Mkandara

Verified Member
Mar 3, 2006
15,536
2,000
Zitto,
Ndugu yangu samahani kidogo naomba somo hapa. Kama nimekuelewa vizuri, umesema kuna uchaguzi mdogo wa diwani 16 unaendelea, Hizi diwani ni zipi nakuomba utupe majina ya hizo kata zinazogombewa na pia ningependa kuelewa kama uchaguzi huu mdogo umefuata taratibu za kalenda kulingana na katiba ama imetokana na sababu ulizozitaja ambazo hazikupewa ibara na kifungu maalum ktk katiba.
 

Masatu

JF-Expert Member
Jan 29, 2007
3,281
1,195
'satu
Kuomba kuharisha tarehe ya mchezo ni tofauti na kutotokea uwanjani, Kwani goli la msumbiji lilifungwa dakika ya ngapi pale 'uwanja mpya'??Msee huo ni mmomonyoko kwa upande wenu, kwani ni lini mara ya mwisho sisiemu ilikosa mgombea wa udiwani?

Hivi baada ya lile goli la msumbiji mpira uliisha palepale eeh... Vipi ile mechi ya Kirumba na Senegal baada ya goli la Nizar.. second half ikawaje....

Suala hapo mkuu sio kuakhirisha mchezo, bali ni kuwa kuna timu inaamini kuwa wachezaji wake hawajasajiliwa na inaomba wasajiliwe kwanza ili watie timu uwanjani, lakini kwa upande mwingine wakiambiwa wameshinda ktk usajili uliopo wapo tayari kukubali ushindi!
 

Masatu

JF-Expert Member
Jan 29, 2007
3,281
1,195
inaonekana kimekuuma sana kukosa mgombea kwenye udiwani..

mwaka huu utakula nyembe kwa hasira na wivu...

kwi kwi kwi kwikiiiiii kwi


Hapana, nimefurahi kama ulivyofurahi wewe!

Kula wembe kwa ushindi wa udiwani! I dont think so.... u must b joking!
 

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Apr 27, 2006
12,668
0
CCM 5.... ... Upinzani 1,


MAPAMBANO YA KIFIKRA HAYA....


Uchaguzi wa Udiwani Kata 16......... Upinzani 1 CCM 0

Kama mnavyofahamu hivi sasa kampeni za uchaguzi wa udiwani zinaendelea nchi nzima. Chaguzi hizi ndogo zinatokana na waliokuwa wakishikilia viti hivo ama kufariki dunia au kupoteza sifa za uanachama wa vyama vilivyowadhamini.
Wakati siku ya uchaguzi ni tarehe 28 oct tayari kambi ya upinzani imekwisha weka kibindoni kiti kimoja katika Kata ya Nankukwe, halmashauri ya Wilaya ya Chunya kule Mbeya. CCM walikosa mgombea katika hiyo baada ya wananchi kuona kuwa hata wakigombea watashindwa tu. Mpaka ilipofika saa kumi jioni ya tarehe 2 Oct, mgombea wa upinzani Bwana Lula ndie alikuwa mgombea pekee aliwasilisha fomu za utezui na hivyo kutangazwa kuwa Diwani wa kata hiyo........... Hii ni habari njema sana kwa wapenda mabadiliko wote nchi hii. Kama CCM wameshindwa kupata mgombea wa udiwani, chama chenye mtandao nchi nzima, tusubiri tuone Ubunge 2010.........


Pigo Kubwa Kwa Upinzani. Kabuye Ang'olewa Ubunge.

taarifa zilizonifikia hivi punde ni kuwa mbunge wa jimbo la Biharamulo mh.mzee Phares Kabuye , ameng'olewa kwenye kiti chake cha ubunge asubuhi hii ya leo.
Mahakama kuu kanda ya Kagera imetoa uamuzi kuwa ameshindwa kesi ya uchaguzi iliyokuwa imefunguliwa na mgombea wa ccm na hivyo kutangaza kuwa amekosa sifa za kuendelea kuwa mbunge wa jimbo hilo.

Unajua hakuna kitu kibaya katika siasa kama unazi wa vyama, na kwa kawaida hufanywa na wanachi wasiokuwa na uchungu na taifa, kwa sababu kama kutogombea udiwani wa Chunya, ni dalili za kushindwa kwa CCM in the future kwenye taifa, Je kuondolewa kwa mbunge wa upinzani na mahakama ni dalili za nini kwenye taifa?

Diwani wa Chunya, na mbunge wa taifa nani ni more effective kisiasa? Chunya iko wapi Tanzania? Wazee taifa letu linadidimia na hizi siasa za unazi, uchaguzi wa mwisho wa udiwani kuna kata moja kule Lushoto, wagombea wote kuanzia upinzani mpaka CCM, waliamua kumuachia mgombea wa CCM, ambaye alionekana kuwa ndiye the best kwa interest ya tarafa, sasa kweli unaweza kusema kuwa hiyo ilikuwa ni dalili ya nini kwenye taifa?

I understand, kuwa kushinda makubwa ni lazima uanzie padogo, lakini kama Chunya ndio the best sign ya uchaguzi ujao wa taifa, basi kweli Freeman ndiye the next president maana hizi dalili za Chunya ni nzito sana,

Tunahitaji ku-grow up na kuzipita hizi siasa za unazi, tumewapeni heshima sana kwenye Mafisadi, it was a home run,

lakini za Chunya Pleeeeease you can have it!, Mheshimiwa Zitto, jina lako sasa ni kubwa mno than hizi siasa kata na madiwani wa Chunya, start living up to your name please, tunakuheshimu mno mkuu!
 

Masatu

JF-Expert Member
Jan 29, 2007
3,281
1,195
Mkuu ES safi sana! hawa so called washindani wanaishi kwa matumaini tu yaani all these fuss ni kwa sababu ya Kata moja? Dar Es Salaam yenye kata 52 haina diwani hata mmoja wa ushindani sembuse Mbunge.. lakini wanakwambia huo ndio mwisho wa CCM...

Haya ishini na fantasies zenu....
 

Masatu

JF-Expert Member
Jan 29, 2007
3,281
1,195
Wagombea CCM wapita bila kupingwa

NA MWANDISHI WETU

HALMASHAURI Kuu ya Taifa ya CCM imewapongeza madiwani wa kata za Mwandu, wilayani Kwimba na Lipumburu, wilayani Masasi, ambao wamepita bila ya kupingwa.
Hatua hiyo imeelezwa kuwa inadhihirisha kukubalika kwa Chama ndani ya umma.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Aggrey Mwanri, alisema pongezi hizo zilitolewa katika kikao cha halmashauri hiyo, kilichofanyika juzi.
Mwanri alisema kikao hicho, pamoja na mambo mengine kilipokea taarifa ya maendeleo ya maandalizi ya uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 16 za Tanzania Bara.
Katika hatua nyingine, alisema halmashauri hiyo imepongeza maandalizi yanayoendelea ya mkutano mkuu wa CCM wa Taifa, utakaofanyika Novemba 3 hadi 4, mwaka huu mjini Dodoma.
Alisema licha ya pongezi hizo, kikao kilipitia na kujadili mapendekezo ya mabadiliko ya Katiba na Kanuni za CCM, katika baadhi ya vifungu, ambayo yatawasilishwa katika mkutano mkuu.

Haya sasa kiko wapi? wako wapi wale waliosema tusome alama za nyakati... nadhani wanaweza kufuata ushauri wao wenyewe...

Sasa hata half-time bado goli limerudi na mshafungwa la pili na mechi ndio bado mbichiiiii.

Mtakufa na vijiba vya roho.....
 

Masatu

JF-Expert Member
Jan 29, 2007
3,281
1,195
Nadhani ipo haja ya kubadili jina heading ya thread na isomeke wapinzani 1 CCM 2

Teh teh teh!
 

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,172
2,000
watapitwa kama wamesimama, kwani kuuza chai huko!

nyie uzeni chai wenzenu wanachapa kazi
 

payuka

JF-Expert Member
Jun 17, 2010
829
0
Kalumanzira (sio kalimanzira)

Mwaka 2005, CCM ilishinda bila kupingwa viti 9 vya Ubunge. Mwaka 2000 walishinda viti 20. Mchakato wa demokrasia ni pamoja na kupita bila kupingwa. Nchini Uingereza na Canada, kuna historia ya maspika wa bunge ambao wameongoza vikao vya Bunge bila ya upendeleo wa kisiasa kuachiwa viti vyao bila kupingwa.

Jambo la Msingi hapa ni kuwa CCM, chama chenye mtandao mkubwa kimeshindwa kupata mgombea udiwani Chunya! Narudia Chunya!

MwanaKijiji,
Tumegawana Kata kwa vyama. Tunajitahidi kuhakikisha kuwa tunahinda Kata nyingi tuwezavyo. CHADEMA mpaka sasa imejiweka vizuri sana katika Kata 4- Majengo-Songea, Katazi, Kabwe na Namanyere kule Rukwa. TLP wameshapata kiti kimoja na wana uhakika wa kushinda kule Moshi Vijijini na Arusha. CUF wana uhakika wa kushinda kule Tunduru katika kata moja. Tunaweza kupata kata kumi. Tunajitahidi

haya mambo ya kupita bila kupingwa kumbe yameanza siku nyingi sana!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom