Uchaguzi wa Ubunge Ngorongoro kufanyika Desemba 11

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza uchaguzi mdogo wa Jimbo la Ngorongoro mkoani Arusha utakaofanyika Desemba 11 mwaka huu.

Siku hiyo pia utafanyika uchaguzi mdogo wa diwani wa kata ya Naumbu, Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, mkoani Mtwara.

Hatua hiyo imetokana na Tume kupokea barua ya Spika wa Bunge akiitaarifa kuwepo kwa nafasi wazi ya ubunge katika Jimbo la Ngorongoro halmashauri ya Wilayanya Ngorongoro mkoani Arusha.

Pia imepokea barua kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, ikitaarifu Tume juu ya uwepo wa nafasi wazi ya diwani.

Nafasi wazi ya ubunge imetokana na kufariki kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro, William Ole Nasha kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) aliyefariki Septemba 27 mwaka huu.
 
Naona siku hizi uchaguzi unakuwepo kati ya vyama rafiki tu, Chadema wakishiriki unageuzwa uchafuzi watu wanatafuta ushindi wa lazima.
 
Wameivuruga sana nchi yetu hawa wahuni. Nchi ambayo iliheshimika duniani sasa iko kundi moja na Burundi, Somalia etc.

Hakuna hajja ya kushiriki kwenye huu udhalimu tuwaache waendelee na utapeli wao. Kushiriki hizi chaguzi ni kubariki hizi hujuma.
 
Yaani hiii ni aibu kubwa mno...eti Tanzania kuna uchaguzi..ushuzi.
 
Back
Top Bottom