Elections 2010 Uchaguzi wa TZ vs uchaguzi wa Ivory Coast

nyasatu

Member
May 15, 2009
72
0
Katika kukua kwangu nimekua nikisikia sifa tofauti tofauti kuhusu wa tz,baadhi ya sifa izo ni kuwa wapole,wasio penda purukushani,wasiojua kudai haki yao,waungwana,watu wa yes sir etc.
Nikiwa ktk harakati zangu za kuangalia CNN wiki hii nzima kwa kiasi fulani nimefurahishwa na habri za uchaguzi wa ivory cost na mara moja habari hiyo imenifanya nikumbuke uchaguzi wetu wa Nov 31,ingawa kwa upande mwingine sifurahishwi na vitendo vya kuona maaskari(un+locals)wakiwa mitaani na mitutu na habari zinazidi sema kuwa yawezekana kukazuka ugomvi.

Sasa basi baadhi ya matukio(see below) yaliyonifanya nifurahi zaidi na kuanza kufikiria je yawezekana tokea hapa Tz na je mtu/watu wanaogopa nini kufanya ivyo au ndio ktk kudumisha mila ya kua wa tz ni waungwana,ni kama ifuatavyo
1)kuona mtu akimpokonya live muhusika wa uchaguzi makaratasi ya matokeo mbele ya waandish alipokua akitangaza matokeo na kuya destroy kwa kuonyesha kuyapinga.Hapa nliwaza siku wahusika wa NEC walipokua wakitangaza ''cooked data/results''zao lingetokea hili tukio ingekuaje?na hapa nazidi somehow prove that maybe tu wastaarabu mana walioonewa waliishia kutoa tu kauli za kumstopisha mtangazaji matokeao hata hivyo kauli hizo hazikuzaa matunda yeyote,wengine waliishia andika tu kwenye magazeti na hakukua na any sort of strike hata kupinga hayo matokeo.
2)Tukio la kuona despite all odds na vituko vya raisi aliekua madarakani lakini bado upinzani wameshinda,ila kinachonichekesha eti nao wamepinga matokeo.hapa nili assume siku ya siku ikifika na CDM ikashinda am sure CCM watapinga nao matokeo,ss hao CCM sitaki kujiuliza kama ni waungwana wa kuweza kukemea tu kwa maneno(kaa ilivyo ada ya wa tz)au nao wataingia msituni/mtaani?jibu la hili swali nahisi hadi ikifika wakati ndio nitajua kwa ss sina la kusema.....

all in all tuzidi waombea hawa wenzetu wawe na amani,mana vita sio jambo jema hata kidogo.

Nawasilisha
 
Ikimita

JF-Expert Member
Oct 23, 2010
300
195
Katika kukua kwangu nimekua nikisikia sifa tofauti tofauti kuhusu wa tz,baadhi ya sifa izo ni kuwa wapole,wasio penda purukushani,wasiojua kudai haki yao,waungwana,watu wa yes sir etc.

Hizo ndio gharama za amani ya Tanzania, hamna shida siye tubaki hivyo hivyo tu mkuu :)
 
Bwana PGO

JF-Expert Member
Mar 17, 2008
44,704
2,000
Katika kukua kwangu nimekua nikisikia sifa tofauti tofauti kuhusu wa tz,baadhi ya sifa izo ni kuwa wapole,wasio penda purukushani,wasiojua kudai haki yao,waungwana,watu wa yes sir etc.
Nikiwa ktk harakati zangu za kuangalia CNN wiki hii nzima kwa kiasi fulani nimefurahishwa na habri za uchaguzi wa ivory cost na mara moja habari hiyo imenifanya nikumbuke uchaguzi wetu wa Nov 31,ingawa kwa upande mwingine sifurahishwi na vitendo vya kuona maaskari(un+locals)wakiwa mitaani na mitutu na
 
Bwana PGO

JF-Expert Member
Mar 17, 2008
44,704
2,000
JK alipopata hizi taarifa kamcheka sana GABGABO kuwa kwanini ashindwe wakati ana dola, na silaha na kila kitu? kumbe jamaaa alimwalika ili aje aone uchakachuaji ulivyo bahati mbaya akawa busy na campaign sasa sijui atadai auziwe ikulu? maana naskia jamaa naye amemrudisha makusudi mafungio ili amuuzie pale kama kipindi kileeeee
 
kayumba

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
653
195
Nilikuwa napanga kuandika thread kuhusu hii mada Tz Vs Ivory Coast.

Mkuu, ufanano wa Tz na Ivory coast ya siku za nyuma ulikuwa mkubwa sana kuhusu suala la amani. Lakini angali Ivory coast katika miaka hii takribani 10 imekuwaje? Kama kawaida chanzo ni viongozi wa afrika kung'ang'ania madaraka. Nakumbuka mwandishi mmoja baada ya machafuko ya kwanza nchini Ivory coast alimalizia makala yake na maneno haya "At last Ivory Coast has proved to be part of Africa". Hii sentensi siku zote huwa iko akilini mwangu na naomba isitumiwe kuielezea tanzania uko tuendako! Mungu ibariki Tanzania.
 
bwegebwege

JF-Expert Member
Jul 30, 2010
1,055
1,250
Watanzania ni mabingwa wa kuongea; hakuna atakayethubutu kwenda na kupinga matokeo au kuizuia tume kutangaza matokeo!! Wabongo wamelala; wako usingizi mzito...Usingizoi wa PONO, ndiyo maana watawala wanawageuza watakavyo!! WATANZANIA WAAMKE!!

Nikukumbushe tu, Uchaguzi wa Bongo(SORRY, UCHAKACHUZI) haukuwa November 31 (kawaida Nov ina siku 30)......ulikuwa October 31
 
Bantugbro

JF-Expert Member
Feb 22, 2009
4,460
2,000
Wakuu,

Uchaguzi wa Pwani ya Pembe ya Ndovu hauna tofauti yeyote na Uchakachuaji wa Nov Bongo, maana tayari Kivaitu keshafanya kazi yake na sasa kamtangaza Gabgo kuwa ndiye mshindi halali. Habari ndio hiyoo..
 
niweze

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
1,008
0
Uchaguzi wa Ivory Coast ni Sawa Kabisa na Uchaguzi wa Tanzania. Kikubwa Kilichotokea ni Kwamba Pale Ivory Coast Kuwekuwa na Wanajeshi wa UN Kwa Sababu ya Vita na Walitakiwa Kuhusika Katika Uhasabiaji wa Kura. Hawa Wawakilishi wa UN Walihesabu Kura na Wametoa Kauli Kwamba Upinzani Wameshida. Kamati ya Katiba Imebadilisha Matokeo Kwa Sababu Raisi wa Chama Tawala Hajakubali Matokeo.

Hii ni Sawa Kabisa na Tanzania. Kikwete Alishindwa Uchaaguzi na Tume Ilimweleza JK Hilo na JK Akasema Hakikisheni Mnatangaza Nimeshinda na Kitu Ambacho CCM Ilifanya ni Kuhakikisha Wale Wasimamizi wa EU na Wapinzani Hawaingiii Kwenye Vituo vya Kuhesabia Kura. Kikwete Alishindwa Huu Uchaguzi na Madikteta Peke Yao Ndio Wanafanya Uhasi Kama Huu. Kitu Kingine ni Kuona Wananchi Tulikaa Kimya Bila Kupinga Kwa Nguvu Zote. Haya Ndio Matatizo ya Africa. Hakuna Demokrasia Africa Kabisa na Tukiangalia Kuanzia North Mpaka South Africa ni Udikteta Mtupu. Hii Ndio Kikwazo cha Maendeleo ya Inchi Zetu. Safari ni Kubwa ila Inatia Moyo. Hii Africa Union Sasa Ivunjwe Kabisa Mpaka Tupate Demokrasia Ipatikane. Katiba Peke Yake Ndio Solution ya Kuanzia.

"Maraisi Karibu Wote wa Africa Wamechaguliwa Kwa Demokrasia ya Wizi. "AU Sio Uwakilishi wa Demokrasia"
 
1954

JF-Expert Member
Nov 14, 2006
9,638
2,000
Yaani uchaguzi wa tanzania sawa na ule wa Ivory Coast?????? !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Sina haja na mjadala wa aina hii.
 
Nonda

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
13,372
2,000
Katika kukua kwangu nimekua nikisikia sifa tofauti tofauti kuhusu wa tz,baadhi ya sifa izo ni kuwa wapole,wasio penda purukushani,wasiojua kudai haki yao,waungwana,watu wa yes sir etc.
Nikiwa ktk harakati zangu za kuangalia CNN wiki hii nzima kwa kiasi fulani nimefurahishwa na habri za uchaguzi wa ivory cost na mara moja habari hiyo imenifanya nikumbuke uchaguzi wetu wa Nov 31,ingawa kwa upande mwingine sifurahishwi na vitendo vya kuona maaskari(un+locals)wakiwa mitaani na mitutu na habari zinazidi sema kuwa yawezekana kukazuka ugomvi.

Sasa basi baadhi ya matukio(see below) yaliyonifanya nifurahi zaidi na kuanza kufikiria je yawezekana tokea hapa Tz na je mtu/watu wanaogopa nini kufanya ivyo au ndio ktk kudumisha mila ya kua wa tz ni waungwana,ni kama ifuatavyo
1)kuona mtu akimpokonya live muhusika wa uchaguzi makaratasi ya matokeo mbele ya waandish alipokua akitangaza matokeo na kuya destroy kwa kuonyesha kuyapinga.Hapa nliwaza siku wahusika wa NEC walipokua wakitangaza ''cooked data/results''zao lingetokea hili tukio ingekuaje?na hapa nazidi somehow prove that maybe tu wastaarabu mana walioonewa waliishia kutoa tu kauli za kumstopisha mtangazaji matokeao hata hivyo kauli hizo hazikuzaa matunda yeyote,wengine waliishia andika tu kwenye magazeti na hakukua na any sort of strike hata kupinga hayo matokeo.
2)Tukio la kuona despite all odds na vituko vya raisi aliekua madarakani lakini bado upinzani wameshinda,ila kinachonichekesha eti nao wamepinga matokeo.hapa nili assume siku ya siku ikifika na CDM ikashinda am sure CCM watapinga nao matokeo,ss hao CCM sitaki kujiuliza kama ni waungwana wa kuweza kukemea tu kwa maneno(kaa ilivyo ada ya wa tz)au nao wataingia msituni/mtaani?jibu la hili swali nahisi hadi ikifika wakati ndio nitajua kwa ss sina la kusema.....

all in all tuzidi waombea hawa wenzetu wawe na amani,mana vita sio jambo jema hata kidogo.

Nawasilisha

Mkuu

Hili la nambari 2 lilishawahi kutokea Tanzania. Unless ikiwa kwako zanzibar si Tanzania. CCM baada ya kupata matokea na kujuwa wamepigwa na chini ,walipinga matokeo. Kama unakumbuka, kulikuwa na Mtu ana jina la Ali Ameir aliandika barua ya kukataa, kupinga matokea, siku moja au mbili hivi kabla ya matokeo kutangazwa kule Zanzibar.

Yalipotangazwa, ni baada ya Mwalimu kwenda kuweka mabo sawa kule Zanzibar, CCM wakapewa Ushindi, na Salmini Amour( Komandoo wa kutingisha kiberiti) akavikwa Urais wa Zanzibar.
Huo ulioitwa mpasuko, mgogoro kule Zenj ulianza hapo.

La kushangaza, Bw. Ali Ameir (aliwahi kuwa waziri wa mambo ya ndani ) alipoulizwa ilikuwaje CCM waliandika barua ya Kupinga matokea na leo baada ya kutangazwa washindi munayakubali?
Alibakia kujiuma uma tu.

Kwa taarifa yako tu, tokea uchaguzi wa 1995, kule Zanzibar CCM hawajawahi kushinda kwa kura. CCM inapigwa bao na CUF kila uchaguzi.Hili sio siri.

Kwa hiyo, hilo likitokea tena itakuwa si mara ya kwanza.

Chaguzi za Tanzania ni sawa na michezo ya kuigiza...La muhimu, wahimize CHADEMA, na vyama vyengine vya Upinzani vipiganie kuleta katiba mpya kabla ya chaguzi za 2015. Vyenginevyo bila ya Tume huru ya uchaguzi hakuna mpinzani "atakaeshinda". Ushindi uko guaranteed kwa CCM kupitia Tume ya Uchafuzi!

Haya shime, tudai katiba mpya.

Natumai umemsikia mama waziri mpya wa sheria anasema Tanzania haihitaji katiba mpya, tutaendelea kuweka viraka itakapolazimu, pia anasema hakuna mahela ya kuanza huo mchakato wa katiba mpya.

Nilisikia kuwa Upinzani ulishatengeneza rasimu ya katiba mpya, Waambie CHADEMA na Wadau wengine waifute vumbi,wanaweza kwa umoja wao kumkabidhi huyu mama,yeye kazi yake iwe ni kuipeleka tu bungeni ili waipitishe, kama kweli ana uchungu wa kuokoa mahela ya walalahoi;Na kama kuanza mchakato wa katiba mpya ni gharama kubwa kama anavyotaka tuamini. Wakiuza VX8 moja tu au mbili, hela zitatosha kutuletea katiba mpya au thamani ya katiba mpya ni damu ya Watanzania?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom