Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,181
Hoja ya serikali kupunguza siasa kwenye taasisi za kitaalamu kama TLS ina mashiko lakini siyo kwa ubabaishaji tunaouona hivi sasa.
Utawala waelekea umeshikwa na wenye uwezo mdogo na ndiyo maana wamejikita zaidi kwenye vitisho vya aidha kuifuta TLS au kupuuzilia mbali ushauri wao wa uteuzi wa majaji.
Ukweli ni kuwa vitisho vyote hivyo sana sana vinampaashia Tundu Lissu na wenzie kushinda uchaguzi na vitisho vya watawala kuthibitisha jinsi ambavyo wamekuwa wakiitumia TLS kubinya haki kila kona.
Mtu wa kawaida atajiuliza hivi hawa watawala yanawahusu nini yaendeleayo ndani ya TLS kama wao hawahusiki moja kwa moja na kunufaika na uongozi uliopo?
Ni kweli utaalamu ni chachu ya siasa lakini siasa ni hamira ya utaalamu.
Hamira hii kwetu hapa imechacha na haifai tena.
Utawala uache kujiingiza kwenye siasa ya vyama vilivyosajiliwa kisheria kwani kwa kufanya hivyo ni kujidhalilisha na ubavu wao wa ushawishi ni kondefu sana. Hata wao hili walijua fika na ndiyo maana wamezama kwenye kuwatisha wajumbe Wa TLS kuwa kutakuwa na athari endapo watawachagua mahasimu wao kisiasa kuwaongoza.
Badala ya kupepeta domo na kujishushia hadhi mbele ya jamii utawala urudi ofisini na kuja na muswada Wa sheria Wa kuwazuia wanasiasa kwenye aina za nyadhifa za aina zozote kwenye vyama vya siasa au serikalini kama madiwani, wabunge n.k kugombea nyadhifa kwenye NGO au vyama vya kitaalamu kama TLS.
Hivyo, mjadala wa uchaguzi Wa TLS kutekwa nyara na vyama vya siasa utaota mbawa siku za usoni.
Si kweli Tundu Lissu na Macha ni majibu ya TLS kuzimwa na watawala na hivyo kushindwa kutekeleza wajibu wao.
Zipo sheria nyingi ambazo zimewapa watawala nguvu ya kuigawa taaluma ya sheria na hivyo kuitawala watakavyo.
Pili siyo sahihi mtu au kikundi cha wanasiasa wachache wakajirundikia vyeo halafu huku wanaibeza katiba kwa kumrundikia Rais madaraka huku na wao wanaonyesha haiba hiyohiyo ya uroho na uchu Wa madaraka.
Utawala kunjua makucha kwa kurekebisha sheria acheni domo na vitisho ambavyo sanasana mnatuthibitishia kweli mmechokaaaaaa