Uchaguzi wa TFF: Wallace Karia achaguliwa kuwa rais mpya wa TFF

wilcoxon

JF-Expert Member
Jun 25, 2017
1,094
2,831
Uchaguzi TFF umeshafanyika jioni ya leo ambapo Rais, Makamu wa Rais na wajumbe kadhaa wamechaguliwa.

Rais mteule ni Wallace Karia, Makamu wa Rais ni Michael Wambura.

IMG_2596.JPG


Mchanganuo wa Kura kwa nafasi ya Urais:-
Jumla ya Kura zilizopigwa - 128
Kura zilizoharibika - 3

Wallace Karia - 95
Ally Mayay - 9
Shija Richard - 9
Iman Madega- 8
Mwakalebela- 3
Emmanuel Kimbe- 1

wallace-karia.jpg

Wallace Karia


Wajumbe waliochaguliwa ni kama ifuatavyo:

Zone 1: Saloum Chama
Zone 2: Vedastus Lufano
Zone 3: Mbasha Matutu
Zone 4: Sarah Chao
Zone 5: Issa Bukuku
Zone 6: Kenneth Pesambili
Zone 7: Elias Mwanjala
Zone 8: James Mhagama
Zone 9: Dunstan Mkundi
Zone 10: Mohamed Aden
Zone 11: Francis Ndulane
Zone 12: Khalid Abdallah
Zone 13: Lameck Nyambaya

======

STORY:

KUFUATIA Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) uliofanyika leo katika Ukumbi wa St Gasper Mjini Dodoma na kumalizika jioni ya leo, Mwenyekiti wa Kamati ya TFF, wakili Revocatus Kuuli ametangaza matokeo ya Uchaguzi huo Wallace Karia ameshinda nafasi hiyo kwa jumla ya kura 95 kati ya kura halali 125 zilizopigwa huku kura tatu zikiharibika na Michael Wambura akichaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho hilo..

Wagombea wengine wa Urais pamoja na kura walizopata ni Ally Mayay Tembele (9), Shija Richard (9), Iman Madega (8), Frederick Mwakalebela (3) na Emmanuel Kimbe (1).

Mohamed Abeid (Dodoma na Singida), Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Sarah Chao (Arusha na Manyara), Dustan Ditopile (Lindi na Mtwara), Elias Mwanjala (Mbeya na Iringa), Francis (Pwani na Morogoro), Vedastus Lufano (Mara na Mwanza), Lameck Nyangaya (Dar es salaam), Kenneth Pesambili (Rukwa na Katavi), Khalid Mohamed (Kilimanjaro na Tanga), Issa Mrisho (Kigoma na Tabora) na James Patrick (Njombe).

Rais wa Shirikisho hilo, Wallace Karia, Makamu wa Rais, Michael Richard Wambura pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji waliochaguliwa wameapishwa leo mjini Dodoma muda mfupi baada ya matokeo ya ushindi wao katika uchaguzi huo kutangazwa.

Akitoa hotuba yake muda mfupi baada ya kuapishwa kwake, Rais wa Shirikisho hilo (Wallace Karia) amesema kuwa amepigiwa simu na Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino pamoja na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmad Ahmad na wote wamelipongeza Shirikisho hilo kwa uamuzi ulioufanya na kuutakia uongozi mpya mafanikio mema.

Aidha Karia amesema TFF itawapa waandishi wa habari elimu ili kujua mambo gani ya kuzingatia kuweza kuinua soka la Tanzania, huku akitangaza kuanzia leo, soka la Tanzania halitakuwa na ubabaishaji.

Kwa upande wake, Waziri mwenye dhamana ya Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ameiagiza TFF kuweka utaratibu wa kuchapisha taarifa ya mapato na matumizi kwenye magazeti ili wananchi wajue.

=======

WASIFU WA WALLACE KARIA

Huyu ni MTanzania mwenzetu mpenda michezo mwenye kiu na maendeleo ya mpira wa Tanzania.

Karia ni aina ya viongozi wenye mapenzi mema na soka ndio maana sehemu nyingi alizopita ameacha alama nzuri katika soka.

Kaanza kuutumikia mpira kwa kuucheza akichezea timu ya Cost Kids ya Tanga, amecheza timu ya shule Popatral,timu ya Chuo cha Uhasibu Dar Es Salaam, timu ya Chui Tanga ambayo ilibadilishwa jina na kuitwa NIA, amecheza na kina Hussein Mwakuluzo, Razak Yusuph Careca,Joseph Razaro na wengi wengine na akiwa JKT amecheza JKT Ruvu.

UONGOZI

Kaanza kupata uzoefu kwenye ngazi za chini na kupanda kidogo kidogo mpaka amefika nafasi ya Makamu wa Rais na sasa ni Rais wa TFF

1990-Alikuwa mweka hazina Cost Union na baadaye akawa mweka hazina wa Chama cha soka Tanga.

Wakati Mh. Said Meck Sadick alipokuwa mkuu wa wilaya Tanga alimteua Karia kuwa Mjumbe kamati ya michezo wilaya na mweka hazina wa kamati.

Mh.George Huruma Mkuchika alipokuwa Mkuu wa mkoa Tanga alimteua Karia kuwa mweka hazina kamati ya michezo mkoa.

2004- Akashinda uchaguzi na kuwa muwakilishi wa kwanza wa vilabu Tanga na mjumbe mkutano mkuu TFF.

2008-Akashinda ujumbe kamati ya utendaji wilaya Tanga kabla ya kuhamishiwa kikazi kwenda KITETO ambako nako alishinda nafasi ya muwakilishi wa vilabu wilaya Kiteto na baadaye akawa muwakilishi wa vilabu mkoa wa Manyara.

Akiwa Manyara aliipandisha timu ya Morani FC kutoka ligi ya mkoa mpaka daraja la kwanza, akahamishiwa Dodoma ambako aliipandisha timu ya Polisi Dodoma ligi kuu akishirikiana na bwana Mwansasu na alipohamishiwa Morogoro akaipandisha Polisi Morogoro ligi kuu.

Akiwa mshauri wa fedha wa miji na majiji katika miji 7 na CDA alikuwa mmoja wa washauri wa kuanzishwa kwa timu ya MBEYA CITY akiwa na kina Juma Idd, Mapunda na Kimbe.

Akiwa mtumishi wa Halmashauri ya Tanga kwa juhudi zake alifanikisha TFF kupata uwanja uliopo ufukweni Tanga.


Amewahi kuwa Makamu mwenyekiti Coast Union wakati mwenyekiti akiwa Titus Bandawe na katibu Salim Bawazir lakini mbali na nafasi hiyo pia amekuwa kiongozi nafasi mbalimbali Coast ikiwemo kamati ya usajili.

Kwa jinsi asivyo na makando kando aliwahi kugombea nafasi ya uwakilishi wa vilabu kamati ya utendaji mpinzani wake mkubwa Abdul Sauko alipata kura 20 Karia alipata kura 106.

Alianzisha vuguvugu la kutaka ligi inayojitegemea akiwa na kina Ahmed Mgoyi na Yahaya Mohamed na ndipo Rais wa TFF Leodiger Tenga wakati huo alimteua kuwa mwenyekiti bodi ya ligi TPLB na akiwa nafasi hiyo akavipigania vilabu vipate haki ya kimkataba na mkataba wa VodaCom ukafanyiwa review na klabu na huo ukawa mkataba wa kwanza kujadiliwa na vilabu.

Akiwa mwenyekiti wa bodi ya ligi alifanikisha ujio wa Azam Tv ambayo ilipata haki ya kuonyesha ligi kuu (Tv Rights)

Mwenyekiti wa Shimisemita shirikisho la michezo mamlaka za serikali Mh Adam Mgoy(DC Kilosa) alimteua kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ambako anafanya kazi kubwa kuhamasisha michezo.

Amepitia kozi mbalimbali za uongozi za FIFA na ameshika nafasi mbalimbali za uongozi serikalini.

KAZI

Aliajiriwa wizara ya fedha mwaka 1990 akapangiwa Hazina Tanga ambako aliendelea kama mkuu wa idara ya fedha Manispaa Tanga, Jiji Tanga, Halmashairi Kiteto na manispaa ya Dodoma.

Ofisi ya Waziri mkuu Tamisemi akawa mshauri wa fedha manispaa Tanga ,Arusha ,Mbeya (Majiji), manispaa Mtwara, Kigoma, Dodoma na mamlaka ya CDA .

Amekuwa mkurugenzi Halmashauri Mvomero na manispaa ya Bukoba, muhasibu mkuu ofisi ya mkuu wa mkoa Kagera.

Sasa ni muhasibu mkuu serikali za mitaa ofisi ya mkuu wa mkoa Morogoro

Katika sehemu zote alizopita kuongoza kuanzia serikalini mpaka kwenye michezo hakuwahi kuwa na kashfa yoyote akiwa ni mwenye uadilifu wa kiwango cha juu.

ELIMU

-Ana MBA ya logistics Management kutoka COVENTRY UNIVERSITY huko UK

-Kozi mbalimbali za bodi ya Uhasibu kutoka Taasisi ya Uhasibu Arusha IAA.

-Alipata stashahada ya uhasibu Taasisi ya uhasibu Tanzania wakati huo DSA

- IFM stashahada ya uzamili ya uhasibu PGDA
 
Huko Kwny mpira kuna watu wengi sana wasiojitambua kabisa, hasa wapiga kura, ni ngumu sana kutoka kwa aina hii. Nashauri uongozi huu wa TFF usiwe wa kupigia kura bali kuomba kazi kama wakurugenzi tu. Kuna wapuuzi wengi sana huko Kwny michakato ya kupiga kura ambao hata shule walikataa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Karia na Wambura wote ni Simba damu.
Sasa matopeni chezeni mpira visingizio vya Malinzi havitakuwepo tena.

Kamati ya mashindano ilijaa watu wenu lakini kila kitu ilikuwa Malinzi hiki, Malinzi kile.

Kwa hiyo tutegemee kupindishwa sheria za soka Kwa vile viongozi ni simba damu?
 
Ningeshangaa sana kama wajumbe wangemchagua Ally Mayay. Kwanza kugombeagombea huku kunaweza kufukua siri zako, maana nakumbuka alipokuwa anacheza Yanga alifanya mtihani wa kidato cha sita akapata division zero. Watu wanaweza kuanza kufuatilia aliingiaje katika graduate and postgraduate studies
 
Uchaguzi TFF

Kura ziliopigwa-128
Zilizoharibika-3

Iman Madega- 8
Mwakalebela- 3
Emmanuel Kimbe- 1
Shija Richard- 9
Ally Mayay- 9
Karia- 95
 
Back
Top Bottom