joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,613
Baada ya Tanzania Kufanya vizuri katika kukabiliana na Corona licha ya kelele nyingi za kumpinga Magufuli kwa jinsi alivyopambana na Corona, Tanzania kwa nara nyingine tena imeidhirishia dunia kwamba inao uwezo mkubwa wa kufanya Mambo yake kwa ufanisi wa hali ya juu baada ya kufanya uchaguzi katika mazingira ya amani, usalama na uwazi wa hali ya juu.
Uchafuzi uliofanyika tarehe 28 October ni mfano wa kuigwa katika eneo zima la Africa kutokana na ukweli kwamba, kwa kiasi kikubwa ulifanyika katika mazingira ya wazi na ukweli, licha ya mapungufu machache ambayo hujitokeza katika chaguzi zote hapa Africa.
Matokeo ya uchaguzi huu, hayatofautiani kabisa na yale ya mwaka 2005, ambapo Kikwete alipata kura 80% na zaidi ya viti 254 vya Ubunge.
Ikumbukwe kwamba, katika chaguzi zote za Tanzania zilizofanyika, hakuna hata uchaguzi mmoja ambapo walioshindwa walikubaliana na matokeo ya uchaguzi, kiukweli katika Africa 90% ya wanaoshindwa hawakubali kushindwa panoja na ukweli kwamba kila kitu kipo wazi kabisa
Katika hili la kufanya uchaguzi wa wazi katika mazingira ya utulivu na amani, linaendelea kuiweka Tanzania katika ramani ya nchi zenye kuheshimika sana hapa Afrika, hasa ikizingatia kwamba, gharama za uchaguzi huu, zote zimelipwa na serikali ya Tanzania, hakuna hata senti moja ya msaada toka nje ya nchi, viva Magufuli, viva Tanzania