Uchaguzi wa Tanzania 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi wa Tanzania 2010

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Paul J, Oct 27, 2010.

 1. P

  Paul J Senior Member

  #1
  Oct 27, 2010
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu Watanzania wenzangu:

  Zikiwa zimebakia siku 3, tunayokazi kubwa tu ya kufanya; kuhakikiaha tunaleta mabadiliko ya kweli kwa kupiga kura kwa kiongozi mwenye dhamira ya kweli kuiondoa Tanzania ya sasa kutoka mikononi mwa mafisadi wachache kuipeleka mikononi mwa watanzania wote wenye kiu ya maendeleo ya taifa lao bila kujali itikadi zetu za vyama, dini, rangi na makabila yetu.Tunayemchagua anaye kazi kubwa ya kuijenga tanzania upya katika misingi ya haki, usawa, utu, udugu na umoja kama ilivyokuwa hapo awali mwaka 1967 baada ya Azimio la Arusha! Anayokaza pia ya kuhakikisha rasilimali tulizojaliwa na mwenyezi Mungu kwa ajili yetu sisi watanzania zinamnufaisha kila mmoja wetu aliyebarikiwa kuzaliwa Tanzania na kutunukiwa Utanzania na si kutumika kwenye care homes na baadhi ya atanzania wachache tu(mafisadi) wakati wazee wetu wa east africa wanapigwa mabomu ya machozi.

  Wapo watanzania ambao kwa njia moja au nyingine dhamira zao bado zi hai, hazijawa mfu na hivyo hawapendi kuendelea na ufisadi mbali na kwamba wanafaidika nao lakini kila wakifanya ufisadi bado dhamira zao zinawasuta maana bado zi hai. Hawa nao wasikilize dhamira zao siku hiyo ya tarehe 31 na kumchagua kiongozi makini hata kama wanaubia na ufisadi, kwa kuzisikiliza dhamira zao watakuwa wameziokoa nafsi zao maana Mwenyezi Mungu atakuwa amewarudisha katika kundi lililo jema.

  Wapo watanzania wachache (pure fisads) ambao dhamira zao zimekufa kabisa, wao kumuona mama mjamzito anapelekwa hospital kwa Bajaji wao wakiwa kwenye V8 (full AC,TV kila siti) ni sawa na mtu anapita Mikumi/Serengeti/Ruhaha/Katavi/na kwingineko akiwaangalia twiga tuliojaliwa na Mwenyezi Mungu bila kujali Mama na kiumbe alichonacho tumboni mwake na kudhihirisha hilo huaiadi kuongeza idadi ya Bajaji ili azidi kutalii/kutugeuza binadamu wenzake kama wanyama! Hawa dhamira zao ni mfu kabisa tuwaombee ili zifufuke na kuwa viumbe wapya hapo tarehe 31 huenda zikawasuta na kuwa watanzaia hai tukawanao.

  Mwenye mke, mwenye girl friend, mweyne mchumba, mjamzito na binadamu yoyote mwenye akili timamu sikiliza dhamira yako kutoka moyoni mwako, usiipuuze na hakikisha una piga kura yenye masilahi kwa Taifa na kwa Watanzania waliopo na wale ambao Mungu alishawapangia kuwa watanzania siku za mbele.

  Mungu wabariki wote wnye kuzisikiliza dhamira zao na kuziheshimu kwa kupiga kura, najua Mungu u mwenye huruma kwa viumbe wako lakini kwa binadamu asiyekuwa na huruma kwa binadamu mwenzie kipindi hiki basi muonjeshe uchungu ili naye aweze kumjali binadamu mwenzake kama anavyojijari.
   
 2. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  samahani mkuu,
  wewe ni paul james wa klauzi efem.?
   
 3. P

  Paul J Senior Member

  #3
  Oct 27, 2010
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapana mkuu
   
 4. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2010
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Samahani,

  wewe sio yule mtoto wa veteran wa CCM Paul Sozigwa?
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Hapana mzee!
   
 6. WABUSH

  WABUSH JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2010
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 285
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wewe sio yule mtoto wa veteran wa CCM Paul Sozigwa?


  Mzazi wake hapa anahusikaje!!!!!!
   
 7. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2010
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  samahani, wewe sio yule aliepewa zawadi na bush junior alipokuja kwetu tz?
   
Loading...