Elections 2010 Uchaguzi wa spika: CCM imevunja katiba ya nchi!

Fareed

JF-Expert Member
Apr 13, 2010
328
131
Kitendo cha Kamati Kuu ya CCM chini ya uenyekiti wa Dokta (asiye na PhD) Jakaya Kikwete kupitisha majina matatu ya wanawake pekee na kulazimisha Spika ajaye awe mwanamke kwa kutumia wingi za kura za wabunge wa CCM ni ukiukwaji wa haki za binadamu.

Katiba ya Tanzania na katiba ya CCM yenyewe zinatamka bayana kuwa binadamu wote ni sawa (kama alivyosema JF Senior Expert Member Kiranga kwenye mchango wake hapa JF.)

Hivyo basi, kitendo cha CCM kuwabagua wagombea wengine na kuwazuia wasigombee kwa kuangalia jinsia zao tu ni kinyume kabisa na katiba ya nchi inayotamka kuwa binadamu wote ni sawa.

Hata kama ni lengo ni zuri la "affirmative action" lakini huwezi kuvunja katiba na kunyima watu haki zao za msingi kwa kusingizia 'women empowerment'. CCM iwe jasiri na kueleza sababu halisi za uamuzi wake.

Makamba aliwaambia waandishi wa habari kuwa Spika wa Bunge aliyemaliza muda wake, Samuel Sitta, ni shupavu na mchapa kazi, lakini kosa lake ni moja tu - si mwanamke.

Hii dhambi ya jinsia ni sumu kama ubaguzi wa wagombea kwa kuangalia dini au kabila yao.

Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, katika moja ya hotuba yake maarufu alitoa mfano wa kiongozi mmoja mwenye sifa zote lakini akakataliwa kwa sababu moja tu -- kabila lake Mkara.

Hivyo basi CCM wanasema Sitta ana sifa zote safi za kuwa kiongozi, tatizo lake moja tu -- mwanaume.

Natoa wito kwa Wabunge wa CCM wapinge ubaguzi huu wa kijinsia na uvunjaji wa katiba uliofanywa na chama tawala kwa kumpigia kura mgombea wa upinzani awe Spika ili kuonesha hasira zao.
 

carmel

JF-Expert Member
Aug 24, 2009
2,837
257
Hawa CCM wameshazoea kuvunja katiba na hakuna anaye-question, kwani hukuona Shein kachaguliwa na kuapishwa kama rais wa Zanzibar kabla haja-rersign nafasi yake ya makamu wa rais bara?

Hao ndo CCM, wakiamka wanaamua kufanya watakavyo bila kujali katiba.
 

WABUSH

JF-Expert Member
Oct 14, 2010
286
4
Sababu iliyotolewa si halisi na haina mantiki. They simply looked for what would sound and appeal "sweety" to the public. The core reason is yet and shall never be disclosed.
 

nyondoloja

Senior Member
Nov 10, 2010
189
52
Wana macho hawaoni, wana masikio lakini hawasikii! Siku ya kufa nyani miti yote huteleza hawajielewi katika kutapatapa wanajikuta ndo wanaharibu zaidi
 

Ntemi Kazwile

JF-Expert Member
May 14, 2010
2,185
305
Hii imefanywa makusudi kumwondoa Sitta, hawakuwa na mbinu nyingine isipokuwa kuja na visingizio vya gender.

Ukifuatilia mtiririko wa matukio tangu maovu ya watawala yaanze kufumuliwa na Spika Sitta kuruhusu wabunge kuyajadili kwa uwazi, watawala walijaribu kumzuia Sitta asiruhusu hii mijadala kwani ilikuwa inawavua nguo na tangu hapo waliweka nadhiri ya kumwondoa kwa gharama yoyote ile, walitaka kumfukuza uanachama wakagundua kuwa hiyo ingewagharimu muno, wakajaribu kumwondoa kwenye kura za maoni wakashindwa kwani anapendwa mno jimboni mwake. Wakaweka mapandikizi kwenye mchakato wa uchaguzi ikashindikana pia.

Baada ya hapo wakabuni mbinu ya kuweka wagombea wasiositahili na ambao wako tayari kumshambulia waziwazi ili kuweka mazingira kuwa haelewani na wenzake hivyo anatakiwa kuwekwa kando, walijua pia kuwa hii peke yake isingeuzika, wakabuni mbinu nyingine ya genda ambayo ndiyo wanadhani itawasaidia kutimiza adhima yao (kumwondoa Sitta) bila gharama kubwa.

Hata hivyo hii pia inaweza kuja kuwagharimu kwani Spika akianza kuzuia mijadala ambayo awali iliruhusiwa wabunge wanaweza kumwondoa kwa kanuni za bunge na hilo likitokea gharama zake zitakuwa kubwa mno kwani linaweza kutokea karibia na uchaguzi wa 2015 na hawatapata nafasi ya kuuzima moto uliowashwa na Dr Slaa, na kuchochewa na wapiganaji pale mjengoni kama akina TL, HW, JMS, na wengine
 

Genekai

R I P
Feb 9, 2010
12,521
4,963
Sasa mkuu, kama kikao ndo kinaongozwa na huyo pamoja na vuvuzela unategemea itakuwaje?
 

Edson

JF-Expert Member
Mar 7, 2009
9,709
4,510
Kwa huwajui CCM ni watu wa majungu?

Hhata ukiangalia kipimo cha majungu (jungumeter) kinaonyesha wako kwenye peak
 

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,681
7,245
Kama walivunja katiba kwa kumwapisha Rais aliyeiba kura unaona ajabu nini kutamka huo upupu? Hao ndo chichiem bana
 

MzeePunch

JF-Expert Member
Jun 8, 2009
1,412
200
Walijua kwamba hizo sio sababu halisi ndio maana wakamtumia huyo Vuvuzela Makamba kutangaza kwa sababu sio mtu anayeweza ku-reason. Ukweli ni kwamba waliogopa Sitta angerejea kama Spika wasingefanikisha mipango yao ya kumuweka fisadi mwingine kugombea urais 2015.

Bunge hili litafichua madhambi makubwa zaidi kuliko yale ya Richmond, na ndio maana akina Rostam na Lowassa wamefanya kazi ya ziada kuhakikisha kuwa Sitta harejei kama Spika (Hii ni baada ya kushindwa kumng'oa kule Urambo Mashariki).

Tunasubiri kuona utendaji wa Spika mpya ANNA MAKINDA (Kama atamshinda MABERE MARANDO) ili tujiridhishe kama yeye ni chaguo la mafisadi au la. Tutalijua hilo kutokana na jinsi atakavyo-handle yale yatakayovurumishwa na akina TUNDU LISSU mjengoni.
 

emalau

JF-Expert Member
Apr 25, 2009
2,743
3,030
CCM hawana sifa ya kumtaka mtu aliye serious. Ukitaka upendwe ndani ya CCM uwe mtu wa maigizo. Huyo mama wanayetaka kumpa uspika nimeshamchunguza huwa ana tendency ya kuzuia mijadara mikali. Akifanya hivyo hili bunge litakuwa kama la Kenya la miaka ya 1992, yaani mgumi zitakuwa njenje.
 

kiraia

JF-Expert Member
Nov 20, 2007
1,717
983
Kweli JF kuna majibu ya kila swali, hii pia itawafumbua macho CCM then kesho makamba atakuja na majibu yake.
 

nginda

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
744
82
They are so intentional cuz anna ???kinda ni chaguo la chenge, rostam, lowasa na wengine ili kuzima moto wa ufisadi. read mwanahalisi.
 

mchillo

JF-Expert Member
Oct 13, 2010
493
211
Zipo sababu ziliyojificha ndani ya uteuzi wa CCM. Nazo ni kukwepa uteuzi wa spika atakayesimamia na kulinda maslahi ya taifa zaidi kuliko chama. CCM wanafahamu madhambi mbele ya wananchi, ndiyo maana wanahaha kumpata Spika atakayezima mijadala yenye maslahi kwa taifa ili kulinda maslahi ya wezi na mafisadi waliosheheni ndani ya CCM.
Hebu tujaribu kuwachunguza wateule wao mmoja mmoja, utagundua hakuna hata mmoja mwenye sifa ya kupigania maslahi ya taifa zaidi ya kujikomba kwa mafisadi waliokiteka chama.

Anna Makinda

Nani haelewi ukandamizaji wa Anna Makinda katika kuzima mijadala muhimu yenye maslahi kwa taifa ili kulinda maslahi ya chama chake. Waliokuwa wakifuatilia mijadala iliyokuwa ikiongozwa naye katika Bunge lililopita ni mashuhuda kwani kuna wakati alikuwa akiwaonya wabunge " Nadhani hujui madhara ya kukaidi maelekezo ya kiti" wakati ule alikuwa naibu Spika, je akiwa Spika itakuwaje?

Anna Abdallah

Huyu ni mtetezi namba moja wa mafisadi. Katika Bunge lililopita amekwaruzana mara nyingi na wabunge waliojipambanua dhidi ya ufisadi kwa ajili ya maslahi ya nchi wawe CCM wenzake au wapinzani, ni nani basi mwenye kuamini akishika madaraka ya kusimamia mijadala ya Bunge ataruhusu mijadala dhidi ya wanachama wenzake na chama chake kwa ajiliya maslahi ya taifa?

Kate Kamba
Huyu ni mwanasiasa wa siku nyingi aliyetumia karata zake vyema kutajirika enzi za Mkapa. Huyu kwa kushirikiana na Mama Mkapa waliihujumu nchi kwa kubinafsishiwa lililokuwa shamba la kuku la Taifa (NAPCO) lenye ukubwa wa makumi ya ekari likiwa na nyumba kadhaa, ofisi na vifaa kadhaa kwa bei ya kutupwa, kisha kuigeuza shule (Liku Secondary School) na sasa ni tawi la Kampala International University - Dar Es Salaam. Swali la kujiuliza hapa ni kwamba, Bepari, mfanyabiashara au fisadi anaweza kuendesha mjadala wa kupambana na ufisadi unaoitafuna nchi yetu?

Ombi kwa Wabunge waadilifu wa CCM
Wakumbuke wamechaguliwa na wananchi wenye kiu ya mabadiliko na uwajibikaji wa kweli, utakuwa ni usaliti na uhaini kumchagua Spika asiyefaa ili kulinda maslahi ya mafisadi waliosheheni ndani ya chama cha CCM. Wakifanya hivyo watakuwa wanakula hukumu yao wenyewe itakayohitimishwa miaka mitano ijayo. Kwa vile kura ni za siri tunawaomba watumie hekima yao kumchagua Spika asiye na hofu, jasiri na mwenye uchungu na ufisadi ambaye kwa sasa tunabaki na chaguo moja tu Mabere Marando wa CHADEMA.
Mkifanya hivi mtakiokoa hata chama chenu CCM kilichokwisha poteza dira sawa na gari lililo katika usukani likiwa katika mwendo kasi kabisa ambapo hatuelewi ni nani litampitia!
 

Lenana

JF-Expert Member
Oct 10, 2010
421
78
yetu macho na masikio vijijini wanalitambua hilo!? uongozi huanzia nyumbani familia ya makinda ikoje tunaweza anzie hapo kutambua bunge chini ya uongozi wake litafanana vipi?
 

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,829
4,164
Kitendo cha Kamati Kuu ya CCM chini ya uenyekiti wa Dokta (asiye na PhD) Jakaya Kikwete kupitisha majina matatu ya wanawake pekee na kulazimisha Spika ajaye awe mwanamke kwa kutumia wingi za kura za wabunge wa CCM ni ukiukwaji wa haki za binadamu.

Katiba ya Tanzania na katiba ya CCM yenyewe zinatamka bayana kuwa binadamu wote ni sawa (kama alivyosema JF Senior Expert Member Kiranga kwenye mchango wake hapa JF.)

Hivyo basi, kitendo cha CCM kuwabagua wagombea wengine na kuwazuia wasigombee kwa kuangalia jinsia zao tu ni kinyume kabisa na katiba ya nchi inayotamka kuwa binadamu wote ni sawa.

Hata kama ni lengo ni zuri la "affirmative action" lakini huwezi kuvunja katiba na kunyima watu haki zao za msingi kwa kusingizia 'women empowerment'. CCM iwe jasiri na kueleza sababu halisi za uamuzi wake.

Makamba aliwaambia waandishi wa habari kuwa Spika wa Bunge aliyemaliza muda wake, Samuel Sitta, ni shupavu na mchapa kazi, lakini kosa lake ni moja tu - si mwanamke.

Hii dhambi ya jinsia ni sumu kama ubaguzi wa wagombea kwa kuangalia dini au kabila yao.

Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, katika moja ya hotuba yake maarufu alitoa mfano wa kiongozi mmoja mwenye sifa zote lakini akakataliwa kwa sababu moja tu -- kabila lake Mkara.

Hivyo basi CCM wanasema Sitta ana sifa zote safi za kuwa kiongozi, tatizo lake moja tu -- mwanaume.

Natoa wito kwa Wabunge wa CCM wapinge ubaguzi huu wa kijinsia na uvunjaji wa katiba uliofanywa na chama tawala kwa kumpigia kura mgombea wa upinzani awe Spika ili kuonesha hasira zao.


Huu ni uthibitisho mwingine kuwa CCM kimejaa vilaza na kiko kibiashara zaidi
 

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,829
4,164
yetu macho na masikio vijijini wanalitambua hilo!?

Vijijini wanapata matangazo ya Sauti ya Ujerumani ambao wameelezea suala la Makinda kuwania nafasi ya Spika ni cha kihistoria.

Zaidi ya hapo watasikilizishwa RTD na kama kawa watanyweshwa sumu.

Haya mengine yanahitaji operation nyangumi kuyafikisha kwa wananchi wa vijijini.
 

Mzee Mnoko

New Member
Nov 7, 2010
2
0
Hii ni mara ya kwanza kwa chama tawala kuleta jambo la jinsia katika nafasi nyeti kama hiyo, lakini cha kujiuliza kwa nini wakati huu. Ukiangalia sana kamati ya mzee ruksa haikumaliza muda wake. Kwa kuwa spika Sitta alikuwa mtetezi wa maslahi ya nchi dhidi ya mafisani, CCM wakaona wamuondoe kuanza sura mpya ya chombo chetu kitukufu cha bunge. Hiyo yote ni njama za mafisadi. Nampongeza spika aliyemaliza muda wake maana alifanya kazi hiyo kwa weledi mkubwa.
 

sensa

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
397
20
Walichofanya ni kutimiza utaratibu tu,kwani inaonekana tangu mwanzo walishajua nani wa kumweka ndio maana pia wakasema unaibu spika utakuwa baada ya spika hata wale watakaokosa uspika wanaweza kujiunga kugombea nafasi ya unaibu.Maigizo kama kawaida!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom