Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Ugumu wa Maisha na #KaziNaBata

Chama cha ACT hakiko organized kabisa, ukipiga simu makao makuu hazipokelewi hivi mna matatizo gani, ? hakuna katibu mwenezi?
 
Zito ,kama ni kweli kuna maagizo hayo kutoka kwa viongozi wa ccm kwenda kwa watendaji kata ,hili swala ni hatari sana. Sidhani kama kuandika tu hapa inatosha ,lielezeni hili swala kwa uma kwa uwazi zaidi. Vinginevyo tutaingia kwenye shida kubwa sana.
 
Kabisa. Mipango advanced kabisa. Pia anaanzisha Mkoa mpya utakaochukua Wilaya za Biharamulo, Chato, Bukombe na Kakonko. Makao makuu ya Mkoa Chato na utaitwa Mkoa wa Chato-Burigi

Nimekuja geita hapa nimesikia watu kama watatu kwenye kupiga story kufanya chato kuwa mkoa hii nchi mpk 2035 itakua kila baada ya 10km mkoa duh
 
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Ugumu wa Maisha na #KaziNaBata



Zitto Kabwe, Mb



Jana siku nzima nilikuwa Vingunguti Dar es Salaam. Pamoja na viongozi wenzangu wa Chama cha ACT Wazalendo tulitembea kwa miguu kuzunguka kata nzima kufungua matawi ya chama. Tulifungua matawi 10 kwenye mitaa 6 ya Kata hiyo iliyopo kwenye jimbo la Segerea. Pia nilipata nafasi ya kutoa salaam kwa wanachama baada ya hotuba yenye maudhui makubwa ya Mshauri Mkuu wa Chama chetu Maalim Seif Shariff Hamad. Muhtasari wa salaam zangu ni kama ifuatavyo;



  1. Hakuna wa kufuta ACT Wazalendo na Wanachama kusajili kadi kwenye Matawi yao


Katika kata ya vingunguti tulikagua matawi 10 yenye jumla ya wanachama 714. Vile vile tulitoa kadi 251 kwa wanachama wapya. Niliwasihi wanachama waliochukua kadi za chama kusajili kadi zao kwenye matawi ya Chama. Maelekezo haya yanahusu wanaChama wote nchi nzima na hata walio Nje ya nchi; Kwamba MWANACHAMA kwenye TAWI. Haipaswi kuwa na mwanachama ana hang tu bila ya kuwa na Tawi. Hivyo kila mwanachama wa ACT Wazalendo aende kwenye tawi lake anapoishi au kufanya kazi kusajili nambari yake. Sheria mpya ya vyama vya Siasa inatutaka kutunza daftari la wanachama. Narudia tena kuwa popote walipo wanachama wetu nendeni kwenye matawi yenu kusajili kadi zenu za wanachama.

Kumekuwa na hofu ya chama chetu kufutwa kwa sababu kadhaa zilizotajwa na Msajili wa Vyama. Niliwaambia wanachama wetu kuwa wasiwe na hofu kwani tulijibu barua ya Msajili wa Vyama na hakuna mahala chama kimevunja sheria ya vyama vya Siasa. Tuendelee kufanya kazi ya kujenga Chama na kukiandaa kwa ajili ya chaguzi zinazokuja.



  1. Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 2019


Wanachama wa ACT Wazalendo wanapaswa kujiandaa kikamilifu na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Nimewaeleza Viongozi wa Dar es Salaam kuwa chama kitaweka wagombea kwenye kila Mtaa kwenye Mitaa yote 561 ya Mkoa wa Dar es Salaam. Chama tayari kimeandaa wanachama wake 3,366 kuwa wagombea wa Wenyeviti wa Mitaa na Wajumbe wa Kamati za Mitaa. Wanachama hawa watapewa mafunzo ya namna bora ya kuendesha mitaa na kutoa huduma Kwa wananchi kwa ufanisi na kwa misingi ya demokrasia na utawala bora. Nimewataka Viongozi wa Vingunguti yenye Mitaa 6 kuhakikisha kuwa ACT Wazalendo inashinda mitaa yote katika kata yao.

Hata hivyo kuna changamoto ya tishio kubwa la Uchaguzi kutokuwa huru na wa haki. Niliwapa Taarifa Viongozi na wanachama wa ACT Wazalendo nchi nzima kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM alikuwa na ziara huko Tarime mkoa wa Mara na kuwaita Watendaji wote wa Vijiji na Kata kuwapa maelekezo kuwa Wagombea wa vyama vya Upinzani wasiteuliwe kuwa wagombea kwa kutopokea fomu zao za uteuzi. Inawezekama kabisa kuwa hili la TARIME linafanyika nchi nzima. Nimewataka wanachama wa ACT Wazalendo wasikubali hilo kutokea kwa kuhakikisha kuwa fomu zinarejeshwa kwa wakati na wanachama wawasindikize wagombea kurejesha fomu.

Pia nimemtaka Waziri wa Nchi TAMISEMI Bwana Suleiman Jaffa kuuthibitishia Umma kuwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakuwa huru na wa haki. Tunataka CCM ipambane Nasi katika uwanja sawa badala ya kutegemea mbeleko ya Serikali. CCM inadai kuwa yenyewe ina wanachama wengi na pia imefanya mambo makubwa nchini, kwanini sasa iogope Uchaguzi? Kwanini ilete figisu kwenye Uchaguzi ?

Wanachama na viongozi wa ACT Wazalendo wasimame kidete kukataa kila aina ya uonevu. Wasikubali CCM kupora Uchaguzi huu kwa njia wanazotumia kupora Uchaguzi wa marudio hapa nchini. Nchi nzima isimame imara. Ninawasihi sana Watendaji wa Vijiji na Mitaa nchini kuepuka kabisa kufuata maelekezo haramu ya CCM na badala yake wafanye kazi kwa misingi ya Sheria na Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.



  1. Tunazo sababu za kuibwaga CCM mwaka 2020


Niliwaambia wananchi wa Vingunguti kuwa tuna sababu lukuki za kuiondoa CCM madarakani mwaka 2020. Lakini sababu kubwa ni mbili - Hali ngumu ya maisha ya wananchi wetu na ubinywaji wa Haki za msingi za raia. Sababu hizi zinaweza kuitwa sababu za UCHUMI - Hali mbaya ya uchumi na ugumu wa maisha ( vyuma kukaza ) na ukosefu wa ajira kwa Vijana wenye kufikia umri wa kufanya kazi. Sababu nyingine ni sababu ya HAKI- Uhuru wa watu kuminywa ( UDIKTETA ) na mauaji na utekaji wa wananchi mbalimbali. Sababu hizi zatosha kuiondoa Serikali iliyopo madarakani.



  • maisha ya wananchi yanazidi kuwa magumu kwa sababu Serikali imekuwa ikifanya maamuzi mabaya kiuchumi. Kwa mfano Serikali ya Rais Magufuli tangu iingie madarakani iligoma kutoa Fedha za kununua chakula cha akiba kuweka kwenye ghala la Taifa. Wakati Magufuli anaingia madarakani alikuta kuna akiba ya Chakula Tani 253,000 kwenye Ghala la Taifa ( NFRA ). Mwezi Mei 2019 Ghala la Taifa lina Tani 68,000 tu ya nafaka. Lakini Serikali hiyo hiyo inataka kuwauzia Kenya tani milioni 2 za Mahindi. Wanazitoa wapi wakati wao hawana. Wakati wa mavuno mwaka 2018 Serikali ilikataa kununua chakula ili kuwapa wakulima bei nzuri na pia ikazuia Wafanyabiashara kuuza chakula Nje ya Tanzania. Matokeo yake NFRA hawakuweka akiba na wakulima wakapata bei mbaya sana ya mahindi yao. Leo Mahindi yamepanda bei kwa asilimia 30 kutoka TZS 41,000 kwa gunia Mwezi Mei 2018 mpaka TZS 59,000 kwa Gunia Mwezi Mei 2019. Katika kupanda bei huko Serikali inataka kuuza Mahindi Kenya, Lakini Serikali haina Mahindi. Ina Tani 68,000 tu ambazo hata hapa Tanzania hazitoshi na bei zimeanza kupanda. Wakulima wa mahindi wametiwa umasikini mkubwa. Leo Mkoa wa Rukwa, Mkoa mzalishaji Mkuu wa Mahindi nchini, umekuwa Mkoa wa kwanza kwa umasikini nchini ambapo 45% ya raia wake wanaishi kwenye dimbwi la umasikini. Tukikumbuka na madhila ya wakulima wa Korosho kutolipwa, Soko la Mbaazi kuanguka na sasa tabu wanayopata wakulima wa Pamba, Kahawa na Tumbaku tutatambua kuwa Serikali ya CCM ya Awamu ya Tano imesababisha ugumu wa maisha ya wananchi. Hii ni sababu tosha ya kuwang’oa.
  • Tanzania inaingiza Vijana 800,000 kwenye soko la ajira kila mwaka lakini ni Vijana 70,000 tu wanapata ajira. Vijana 730,000 wanakaa mtaani bila kazi. Kazi zinazalishwa kwa kuwepo kwa shughuli za uzalishaji. Kwa hiyo lazima watu waweke mitaji yao nchini ili kuongeza shughuli za kiuchumi waweze kuajiri. Serikali ya Rais Magufuli tangu imeingia madarakani imechelewesha au kufuta miradi yenye thamani ya USD bilioni 52.8 sawa na TZS Trilioni 121 ambayo ingezishaji mamilioni ya ajira kwa Vijana wa Tanzania. Tunaona inatekelezwa miradi ambayo inatoa Fedha za ndani kwenda nje badala ya miradi inayoingiza Fedha nchini ili kuchochea uchumi wetu. Tunashuhudia pia miradi inayopendelea maeneo Fulani ya nchi yetu kama vile Chato: Uwanja wa Ndege, Hifadhi ya Taifa, Hospitali ya Rufaa na sasa nasikia panajengwa Chuo Kikuu kikubwa cha Wanafunzi 40,000. Kwanza hii ni kinyume cha Katiba kwani Katiba inataka maendeleo ya nchi yawe sawia na pasiwe na upendeleo wa baadhi ya maeneo Lakini pia inajenga chuki kwenye nchi miongoni mwa raia. Sababu hii inatosha kabisa kuiondoa Serikali ya Rais Magufuli madarakani.
  • Kubinywa kwa uhuru wa mawazo, Uhuru wa kufanya siasa, Uhuru wa Habari na hata vitendo vya utekaji na mauaji ni mbinu ya kuendesha Siasa kwa vitisho ili kutawala kwa Imla. Watanzania wengi wanaona kuwa hawana uhuru wa kuikosoa Serikali yao. 54% ya Watanzania wanasema uhuru wao umepotea katika kipindi cha utawala wa Rais Magufuli. Watanzania hawajazoea kuona watu wakitekwa na wengine kupotezwa kwa kiwango kinachoonekana sasa. Hii ni sababu tosha ya kuiondoa Serikali ya Rais John Magufuli.


  1. CCM hawana hoja na Watanzania wamechoshwa na utumwa wa Hapa Kazi Tu, Watanzania Kazi na Maisha


CCM watapata wakati mgumu katika kutafuta kura kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, hali hiyo inatokana na mwenendo wa Serikali ya Awamu ya Tano ambayo imejikita zaidi katika miradi mikubwa ya kitaifa inayotekelezwa vibaya na kusahau miradi midogo yenye kugusa wananchi moja kwa moja majimboni. Wabunge hawa hawana cha kuonyesha kwa wananchi. ‘Focus’ ya serikali hii imekuwa kwenye miradi mikubwa kama ununuzi wa ndege, ujenzi wa reli ya kisasa na miradi mingine. Sasa unaweza kuzungumzia siasa za ujenzi wa reli Morogoro au ndege – Dar es Salaam, Mwanza, Kilimanjaro na maeneo mengine wanakopanda ndege hizo. Unaweza kuzungumzia mradi wa umeme wa Stigler’s Gorge kwingine lakini si Kigoma, maana yake ni kwamba miradi hii mikubwa itakuwa na maeneo mahususi ya kufanyia siasa si kila jimbo la ubunge hapa nchini. Ilichofanya serikali ni fedha za miradi ya maendeleo kwa ajili ya miradi kupitia serikali za mitaa hazipelekwi kwa kiasi cha kutosha, pesa zinaelekezwa zaidi kwenye miradi mikubwa inayotekelezwa vibaya. Wananchi hawaguswi moja kwa moja na hayo. Wananchi wanataka kuona maisha yao yanaboreka.



Ukweli ambao haupingiki ni mmoja; kwamba watu wanahitaji kufanya kazi lakini wanahitaji pia chakula mezani, wanahitaji kupendwa, wanataka uhuru wao, kutimiza haja zao, kuwa na maisha mazuri na kuwa na uhakika wa maisha yao ya sasa na baadaye.Huu ndiyo ubinadamu. Huo ndiyo Utanzania. Kazi na Dawa ndio Kazi na Bata.



Watu wanahitaji kufanya kazi. Watu wanahitaji kufurahia maisha. ACT Wazalendo itaendesha Siasa ya kuwapa watu matumaini ( HOPE ) ili kujenga Tanzania ya Haki na yenye Demokrasia. Tanzania ambayo watu wanafanya kazi na kufurahia jasho la kazi yao. Kazi iendeshe maisha yao. #KaziNaBata



Vingunguti ni salama kwa ACT Wazalendo



Taifa kwanza Leo na kesho

29/7/2019

Kila la heri ACT, Lkn mjipange kujibu tuhuma za udini kwa Chama cha ACT. Hili litqtumika kuwabomoa
 
Zitto is a snitch.....haka kajamaa kana matatizo...nilipotezwa zamani nikifikiri amebadikika bada ya dem wake wa Congo kumuacha, kumbe bado.

Huyu anatuchelewesha sana.
 
Niletee na wako
Ni vizuri umeanza kujitokeza kujibu comments mbalimbali hapa jf, members walilalamika na umekuwa msikivu kwa hilo nakupongeza, ila kwa umaarufu wako ni ngumu kujibu kila comment, chagua chache zitazokujenga zaidi na chama chako kipya.
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom