Uchaguzi wa Serikali za Mitaa haukuwa Huru wala Haki!!!

makoye2009

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,642
2,000
Ni upuuzi na ujinga kuendelea kudanganyana kuwa huu uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaosimamiwa na Serikali ya CCM ati ni uchaguzi huru na wa haki! Haiwezekani chama Twawala CCM wao ndio wawe waratibu na wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Hii ni sawa na kocha wa Timu awe ndio Refa wa mchezo ambao Timu yake inashindana na Timu pinzani.Je, utategemea matokeo gani katika mchezo kama huo? Ni dhahiri mchezo huo hautakuwa ''A FAIR PLAY GAME''

Ili uchaguzi huu uwe Huru na Haki ilitakiwa tuwe na Tume Huru ya Uchaguzi ili iweze kuratibu na kusimamia uchaguzi huu. Kila Mtanzania ameshuhudia vurugu, wizi wa kura, mapingamizi yasiyo kichwa wala miguu kwa wapinzani, kutumika kwa risasi za moto na hata kupelekea vifo! Tumeona kila aina ya mbinu za kuhakikisha kuwa vyama pinzani hawashindi kwa namna yoyote ile ili kuihakikishia CCM kuendelea kutawala milele.

Ukweli utabaki ukweli kuwa CCM hawawezi kutamba kuwa wameshinda Uchaguzi huu hata kidogo. Kilichofanyika ni kwa Wasimamizi wa Uchaguzi(WAKURUGENZI WA MAJIJI NA HALMASHAURI)kuhakikishia kuwa CCM inashinda kwa maelekezo toka juu. Tulisikia kabla ya Uchaguzi kuwa kulikuwa na maelekezo toka Ofisi ya Waziri Mkuu kuwa lazima Wakurugenzi wahakikishe CCM inashinda na Mkurugenzi atakayeruhusu Wapinzani kupata ushindi ajihesabu hana Kazi!!!

Kwa hiyo ushindi wa CCM umetokana na kubebwa na Wasimamizi wa Uchaguzi ambao ni wateule wa Serikali iliyoko Madarakani kwa tiketi ya CCM wakishirikaina na Jeshi la Polisi. Huu ni ukweli ambao hata Rais Kiwete a.k.a Mzee wa Tezi Dume anaujua.

Poleni sana Watanzania kwa kunyang'anywa haki na uhuru wenu wa Kuchagua mnachokipenda.
 
Tetty

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
26,386
2,000
Usijalipamojanayo lakini mvua ya mawe imewanyeshea.:smow::smow::smow:
 
nyabhingi

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
14,374
2,000
ndio maana akapewa fisadi chenge awe mwandishi wa katiba akishirikiana na fisadi sitta.
 
Kwamhuzi

JF-Expert Member
Nov 15, 2014
1,766
1,250
Watanzania walio wengi ni mapoyoyo,sasa unategemea nini mkuu.Wanachaguliwa viongozi wanadhani wamechagua wao.They are being led to the slaughter house bila wao kujua.Frankly hawasaidiki.
Ni upuuzi na ujinga kuendelea kudanganyana kuwa huu uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaosimamiwa na Serikali ya CCM ati ni uchaguzi huru na wa haki! Haiwezekani chama Twawala CCM wao ndio wawe waratibu na wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Hii ni sawa na kocha wa Timu awe ndio Refa wa mchezo ambao Timu yake inashindana na Timu pinzani.Je, utategemea matokeo gani katika mchezo kama huo? Ni dhahiri mchezo huo hautakuwa ''A FAIR PLAY GAME''

Ili uchaguzi huu uwe Huru na Haki ilitakiwa tuwe na Tume Huru ya Uchaguzi ili iweze kuratibu na kusimamia uchaguzi huu. Kila Mtanzania ameshuhudia vurugu, wizi wa kura, mapingamizi yasiyo kichwa wala miguu kwa wapinzani, kutumika kwa risasi za moto na hata kupelekea vifo! Tumeona kila aina ya mbinu za kuhakikisha kuwa vyama pinzani hawashindi kwa namna yoyote ile ili kuihakikishia CCM kuendelea kutawala milele.

Ukweli utabaki ukweli kuwa CCM hawawezi kutamba kuwa wameshinda Uchaguzi huu hata kidogo. Kilichofanyika ni kwa Wasimamizi wa Uchaguzi(WAKURUGENZI WA MAJIJI NA HALMASHAURI)kuhakikishia kuwa CCM inashinda kwa maelekezo toka juu. Tulisikia kabla ya Uchaguzi kuwa kulikuwa na maelekezo toka Ofisi ya Waziri Mkuu kuwa lazima Wakurugenzi wahakikishe CCM inashinda na Mkurugenzi atakayeruhusu Wapinzani kupata ushindi ajihesabu hana Kazi!!!

Kwa hiyo ushindi wa CCM umetokana na kubebwa na Wasimamizi wa Uchaguzi ambao ni wateule wa Serikali iliyoko Madarakani kwa tiketi ya CCM wakishirikaina na Jeshi la Polisi. Huu ni ukweli ambao hata Rais Kiwete a.k.a Mzee wa Tezi Dume anaujua.

Poleni sana Watanzania kwa kunyang'anywa haki na uhuru wenu wa Kuchagua mnachokipenda.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom