Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019: Waziri wa TAMISEMI (Mh. Jafo) atoa Kanuni za Uchaguzi

sajo

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
2,996
5,213
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani S. Jafo ametoa Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019. Kanuni hizo zimechapwa katika gazeti la serikali la tarehe 26 Aprili 2019, kwa Tangazo namba 371 (Kanuni za uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kitongoji katika mamlaka miji midogo za mwaka 2019), Tangazo namba 372 (Kanuni za uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mtaa na wajumbe wa kamati ya Mtaa katika mamlaka za miji za mwaka 2019) na Tangazo Namba 373 (Kanuni za uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wa Halmashauri ya kijiji na Mwenyekiti wa Kitongoji za mwaka 2019).

Katika kanuni hizi, Waziri amefafanua kuwa kwa sasa mtu hatazuiwa kugombewa na hatapoteza sifa za kugombea ikiwa atakuwa anatumikia kifungo cha zaidi ya miezi sita kilichotokana na kushindwa kulipa faini tofauti na zamani ambapo mgombea alikuwa anapoteza sifa za kuwa mgombea ikiwa atatumikia kifungo cha zaidi ya miezi 6 kwa makosa ya jinai bila kujali kifungo hicho kimetokana na kuamriwa moja kwa moja kama kifungo au kikiwa ni mbadala wa kushindwa kulipa faini. Hii ina maana kuwa (mfano) mgombea amekutwa na hatia kwa shtaka linalomkabili na kuamriwa na mahakama kulipa faini ya kiasi fulani cha fedha ama kufungwa jela miezi nane (8) lakini mtu huyu akashindwa kulipa faini hiyo na hivyo kutimikia kifungo jela, bado atakuwa hajapoteza sifa za kugombea.

Kwa kanuni hizi Watendaji wa Mitaa, Vijiji na Kata hawataweza kuteuliwa kuandikisha au kusimamia zoezi la uandikishaji wa orodha ya wapiga kura ingawa wanaweza kuteuliwa kuwa wasimamizi wa uchaguzi huo. Pia kanuni hizo zimekataza watumishi wa Halmashauri kuwa wajumbe wa kamati ya Rufaa ambayo mwenyekiti wake atakuwa ni Katibu Tawala wa Wilaya (DAS) na wajumbe wengine watano ambao ni watumishi wa umma.

Muda wa Kampeni
Kampeni kwa nafasi zote za uchaguzi utakuwa ni siku saba (7) kabla ya siku ya uchaguzi. Kwa mujibu wa kanuni hizi vyama vya siasa havitalazimika kutoa taarifa polisi juu ya mikutano yake ya kampeni isipokuwa vitafuata ratiba iliyounganishwa na kuridhiwa na vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi huo. Ratiba hiyo itawasilishwa Polisi na msimamizi wa uchaguzi. Wajibu wa jeshi la Polisi iakuwa ni kuhakikisha ulinzi unatolewa katika mikutano yote ya kampeni na kuhakikisha amani inalindwa.

Siku ya Uchaguzi
Kura zitapigwa kuanzia saa 2:00 asubuhi mpaka saa 10:00 jioni. Vyama vya Siasa vitakavyoshiriki uchaguzi vitaruhusiwa kuwa na mawakala wakati wa uandikishaji wa orodha ya wapiga kura na pia wakati wa Upigaji kura (siku ya uchaguzi) na pia wakati wa kuhesabu kura zilizopigwa.

Upingaji wa Matokeo ya Uchaguzi
Baada ya matokeo, mgombea asiyeridhika na matokeo ya uchaguzi amepewa haki ya kufungua shauri katika Mahakama ya Wilaya ndani ya siku thelathini (30) kutoka siku ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi. Hii ni tofauti na ilivyozoeleka katika Uchaguzi mkuu ambapo mtu yeyote ambaye alishiriki uchaguzi huo au alikuwa na sifa za kushiriki uchaguzi huo huweza kufungua shauri kupinga matokeo ya uchaguzi, katika kanuni hizi ni mgombea tu ndiye anayeweza kufungua shauri hilo.

Mpaka sasa zimebaki siku themanini na nane (88) kufikia siku ya uchaguzi, tarehe 24 Novemba 2019.
 
Attachments

  • Kanuni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019.pdf
    12.8 MB · Views: 30
Kwa taarifa tu ni kuwa ccm kwa kutumia mabalozi, wenyeviti wa vijiji/mitaa na viongozi wengine wenye vinasaba vya ccm ndani ya halmashauri walishaanza kuandikisha orodha yao ya vitambulisho vya kupigia kura!
 
labdfa kw ashughuli nyingine ila nijuavyo serekali ya mita auandikishaji ufanyika upyaa
 
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani S. Jafo ametoa Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019. Kanuni hizo zimechapwa katika gazeti la serikali la tarehe 26 Aprili 2019, kwa Tangazo namba 371 (Kanuni za uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kitongoji katika mamlaka miji midogo za mwaka 2019), Tangazo namba 372 (Kanuni za uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mtaa na wajumbe wa kamati ya Mtaa katika mamlaka za miji za mwaka 2019) na Tangazo Namba 373 (Kanuni za uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wa Halmashauri ya kijiji na Mwenyekiti wa Kitongoji za mwaka 2019).

Katika kanuni hizi, Waziri amefafanua kuwa kwa sasa mtu hatazuiwa kugombewa na hatapoteza sifa za kugombea ikiwa atakuwa anatumikia kifungo cha zaidi ya miezi sita kilichotokana na kushindwa kulipa faini tofauti na zamani ambapo mgombea alikuwa anapoteza sifa za kuwa mgombea ikiwa atatumikia kifungo cha zaidi ya miezi 6 kwa makosa ya jinai bila kujali kifungo hicho kimetokana na kuamriwa moja kwa moja kama kifungo au kikiwa ni mbadala wa kushindwa kulipa faini. Hii ina maana kuwa (mfano) mgombea amekutwa na hatia kwa shtaka linalomkabili na kuamriwa na mahakama kulipa faini ya kiasi fulani cha fedha ama kufungwa jela miezi nane (8) lakini mtu huyu akashindwa kulipa faini hiyo na hivyo kutimikia kifungo jela, bado atakuwa hajapoteza sifa za kugombea.

Kwa kanuni hizi Watendaji wa Mitaa, Vijiji na Kata hawataweza kuteuliwa kuandikisha au kusimamia zoezi la uandikishaji wa orodha ya wapiga kura ingawa wanaweza kuteuliwa kuwa wasimamizi wa uchaguzi huo. Pia kanuni hizo zimekataza watumishi wa Halmashauri kuwa wajumbe wa kamati ya Rufaa ambayo mwenyekiti wake atakuwa ni Katibu Tawala wa Wilaya (DAS) na wajumbe wengine watano ambao ni watumishi wa umma.

Muda wa Kampeni
Kampeni kwa nafasi zote za uchaguzi utakuwa ni siku saba (7) kabla ya siku ya uchaguzi. Kwa mujibu wa kanuni hizi vyama vya siasa havitalazimika kutoa taarifa polisi juu ya mikutano yake ya kampeni isipokuwa vitafuata ratiba iliyounganishwa na kuridhiwa na vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi huo. Ratiba hiyo itawasilishwa Polisi na msimamizi wa uchaguzi. Wajibu wa jeshi la Polisi iakuwa ni kuhakikisha ulinzi unatolewa katika mikutano yote ya kampeni na kuhakikisha amani inalindwa.

Siku ya Uchaguzi
Kura zitapigwa kuanzia saa 2:00 asubuhi mpaka saa 10:00 jioni. Vyama vya Siasa vitakavyoshiriki uchaguzi vitaruhusiwa kuwa na mawakala wakati wa uandikishaji wa orodha ya wapiga kura na pia wakati wa Upigaji kura (siku ya uchaguzi) na pia wakati wa kuhesabu kura zilizopigwa.

Upingaji wa Matokeo ya Uchaguzi
Baada ya matokeo, mgombea asiyeridhika na matokeo ya uchaguzi amepewa haki ya kufungua shauri katika Mahakama ya Wilaya ndani ya siku thelathini (30) kutoka siku ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi. Hii ni tofauti na ilivyozoeleka katika Uchaguzi mkuu ambapo mtu yeyote ambaye alishiriki uchaguzi huo au alikuwa na sifa za kushiriki uchaguzi huo huweza kufungua shauri kupinga matokeo ya uchaguzi, katika kanuni hizi ni mgombea tu ndiye anayeweza kufungua shauri hilo.

Mpaka sasa zimebaki siku themanini na nane (88) kufikia siku ya uchaguzi, tarehe 24 Novemba 2019.
DAS wameingia.Good
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom