Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,556
- 29,640
Kuanzia mwezi Septemba 2019 hekahela za kinyang'anyiro cha uchaguzi wa serikali za mitaa nchi nzima zitakuwa katika peak.
Uchaguzi huu unatarajia kutupatia wenyeviti wa mitaa, vijiji na vitongoji pamoja na Halmashauri za mitaa kwa kipindi kingine cha miaka mitano hadi 2014. Kwa hali inavyoendelea sasa inaonyesha wanaharakati wamejipanga vilivyo kuibana serikali kuhusiana na utaratibu mzima wa chaguzi za serikali za Mitaa, vijiiji na Vitongoji nchi nzima. Hukumu ya hivi karibuni kuhusiana na usimamizi wa chaguzi zetu imeelekeza kutowatambua wakurugenzi wa Manispaa na Watendaji wa Serikali ambao siyo waajiriwa wa Tume ya Uchaguzi kusimamia chaguzi hizi. nimepata maswali mawili hapa ambayo natamani wenye ufahamu wa taratibu za chaguzi ama waliopo jikoni (NEC) kunipatia uelewa.
1. Je Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji unasimamiwa na sheria ya Tume Huru ya Uchaguzi au upo chini ya TAMISEMI?
2. Kama jibu la swali la kwanza ni kuwa NEC husimamia chaguzi hizi, utaratibu wa usimamizi wa Chaguzi za mwaka huu upoje? Namaanisha kuwa, Wakurugenzi wa wilaya na watendaji hawatahusika na usimamizi?
Ahsante