Diranqw
Senior Member
- Mar 13, 2016
- 160
- 72
Kwa takriban wiki ya pili sasa hekaheka kivumbi na jasho ni kuwania nafasi ya Urais wa serikali ya wanachuo wa chuo kikuu cha kumbukumbu ya sebastian kolowa ambapo vijana machachari wakiumana kwelikweli!,ni kijana Massau Justin a.k.a Kanda maalum na kijana kinda aitwaye Mwakalinga Joel.Uchaguzi ambao unavuta hisia kali ambapo mahasimu wa kuu wa siasa za Tanzania ;CCM VS CHADEMA wanaonekana wakiwa wanasuka mikakati mizito kuhakikisha wananyakua kiti hicho.Wakati timu Mwakalinga ikiwa Bumbuli,Tanga mjini na matawi mengine ya chuo hasimu wake Massau na mshindani mwingine Baraka Maugo wanazichanga karata zao kwenye ardhi ya magamba wakielekea kufunga kampeni hapo kesho tr.14 APRL 2016 kwa mdahalo mkali utakao endeshwa na tume ya uchaguzi ili kuweka wagombea kwenye mizani kwa ajili ya siku ya uchaguzi Ijumaa ya tar.15 Aprl 2016.Nitawaletea moja kwa moja yanayojiri kwenye uchaguzi huu p/se stay tune..........
Diranqw
Diranqw