Uchaguzi 2020 Uchaguzi wa October 2020, mtihani wa kwanza kwa Dk. Bashiru na Polepole

Nzelu za bwino

JF-Expert Member
Jan 12, 2020
376
450
Salaam wanajamvi, Oct 2020 kutakua na uchaguzi mkuu wa kuchagua madiwani, wabunge na Rais wa nchi. Uchaguzi huu ni wa kwanza kwa katibu mkuu na katibu mwenezi toka wateuliwe, ni uchaguzi huu utakaoonyesha uwezo wao wa kupangua na kupanga hoja kwenye mikikimikiki ya kampeni.

Tulizoea kuwaona akina Kinana na Nape walivyokuwa wanapambana. Je, Dkt. Bashiru na Polepole wataweza kuendana na mikikimikiki ya Uchaguzi Mkuu? Nawatakia kila le kheri kwenye Kazi yao.
 
Bashiru na Pole pole wao nguvu zao ni kwa polisi wao ...bila polisccm hakuna CCM nchi hii.
 
Bashiru na pole pole wao nguvu zao ni kwa polisi wao ...bila polisccm hakuna ccm nchi hii
Iko wazi hio, Bashiru alishasema watatumia vyombo vya dola kubaki madarakani. Alishasema hawawezi kufanya uzembe kama wa vyama vyengine vya ukombozi kutolewa madarakani. Nyenzo wanazo watazitumia.

CCM kupitia jumuiya ya vijana ndio TISS wenyewe, ndio Polisi hao na ndio Jeshi hao. Kuna hao vijana wapya wasiojuwa maadili ya kazi zao na waliajiriwa kutokana na UCCM wao.

Nchi imeharibiwa hii. Kwa hio Bashiru kuagiza kuwasha mitambo ya ushindi alikusudia kuwaambia hawa wafanye kazi yao.

Wapinzani jipangeni. Dola ni CCM na CCM ni dola.
 
Hakuna namna nyingine ya kuweza kuishinda ccm bila ya kutumia nguvu ya umma ...kama kuna wapinzani wanao amini kwamba wanaweza kuishinda ccm bila ya kufanya kama kile walichokifanya wa-misri mwaka 2011 basi watakuwa wana jiongopea mchana kweupe
 
Back
Top Bottom