Uchaguzi wa ndani CHADEMA Morogoro wazidi kupamba moto

MPANDA Jr

JF-Expert Member
Nov 27, 2011
1,295
157
Ni mwendelezo wa chaguzi za ndani ngazi ya majimbo na Wilaya za mkoa wa Morogoro. Leo Mwenyekiti wa Mkoa Mhe. Susan Kiwanga pamoja na timu yake akishirikiana na wajumbe wa Kanda ya kati ya Chadema wanasimamia uchaguzi katika Wilaya ya Mvomero.

Uchaguzi wa leo ni wa 5 kufanyika huku ule wa Wilaya ya Manispaa ya Morogoro ukipangwa kurudiwa kutokana na malalamiko yaliyotolewa na baadhi ya wagombea na hivyo msimamizi wa uchaguzi akauahirisha mpaka tarehe itakayotajwa kabla ya mwezi huu wa 8 kuisha.

Mpaka wakati huu, wagombea 43 wamejitokeza kuwania nafasi mbalimbali za wilaya hii. Idadi ya wagombea katika majimbo mengine ni kama ifuatavyo katika mabano Kilosa (31) Ulanga Magharib (34) Morogoro Manispaa (58) na Kilombero (62).

Zoezi hilo litakamilika ifikapo tarehe 27.08.2014

Picha zinaonesha matukio mbalimbali
 
Back
Top Bottom