Malata Junior
JF-Expert Member
- Nov 29, 2011
- 3,104
- 2,549
Kuna taarifa kwamba Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais mstaafu Jakaya Kikwete ataachia madarakani hivi karibuni japo kwa shingo upande.Kuna taarifa pia mwenyekiti mpya atapatikana mwezi Juni mwaka huu pale utakapofanyika mkutano mkuu maalumu wa chama hicho.
Cha kusikitisha hakuna mchakato wowote wa kidemokrasi ulioanza mpaka sasa hivi wa wanachama kutangaziwa kuwania nafasi hiyo,kuchukua fomu,kutafuta wadhamini,kufanya kampeni nk! Kuna tetesi kwamba nafasi hiyo anataka kupewa Rais Magufuli eti ni utamaduni wa chama hicho Rais kukabidhiwa uenyekiti wa chama Taifa.
Kwenye katiba ya CCM hakuna kipengele kinachozungumzia utamaduni,CCM wapeni haki wanachama wenu kugombea nafasi wanayoitaka acheni figisu figisu.