beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,879
- 6,356
Kuna shida kubwa Kilombero muda huu Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilombero...
Leo ndiyo siku uliopangwa kufanyika uchaguzi huo na hadi sasa Mbunge wa Kilombero Peter Lijualikali, dereva wake na dereva wa Mbunge Devotha Minja wamekamatwa na polisi.
Polisi ni wengi sana. Waandishi wa Habari wa baadhi ya vyombo vya habari, wamezuiwa kuingia wala kukaribia ukumbi unaotumika kupiga kura, isipokuwa wanaotoka Star Tv, TBC, Uhuru na Habari Leo.
Hakuna mwananchi anaruhusiwa kusogea. Halikadhalika wabunge wetu wamezuiwa kabisa kuvuka hata uzio uliowekwa. Polisi wamejaa kila mahali.
Upigaji wa kura unaendelea huko ukumbini.