UCHAGUZI WA MWENYEKITI CHUNYA: Madiwani wa CCM kikaangoni............... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UCHAGUZI WA MWENYEKITI CHUNYA: Madiwani wa CCM kikaangoni...............

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Dec 15, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 15, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,266
  Trophy Points: 280
  Madiwani 9 wahojiwa na TAKUKURU


  na Moses Ng'wat, Mbeya


  [​IMG] TAASISI ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (TAKUKURU), mkoa wa Mbeya, imewakamata na kuwahoji kwa saa 10 madiwani tisa wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Wilaya ya Chunya kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa. Miongoni mwa madiwani hao yumo pia Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Chunya, Kapale Chakupewa, ambaye ni diwani wa kata ya Galula na kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana zinadai kuwa ni miongoni mwa wagombea wa nafasi ya uenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo kwenye uchaguzi unaofanyika leo.
  Tukio la kukamatwa kwa madiwani hao linadaiwa kutokea jana baada ya kundi la madiwani hao, kusafiri kutoka wilayani Chunya Desemba 13 na kufikia katika nyumba mbili za kulala wageni walikokamatwa na TAKUKURU.
  Hata hivyo haikuweza kufahamika mara moja kilichosababisha madiwani hao kusafiri umbali wa kilomita 90 kutoka wilayani chunya na kuja mkoani Mbeya na kufikia nyumba mbili za wageni, ikiwa ni siku moja tu kabla ya kufanyika kwa zoezi la uchaguzi.
  Kamanda wa TAKUKURU mkoani Mbeya, Daniel Mtuka, alithibitisha kukamatwa kwa madiwani hao na baada ya kuwekewa dhamana na mmoja wa viongozi wa juu wa chama hicho mkoani humo na kudai kuwa idadi yao hawazidi 10 na kwamba mahojiano ya awali yalifanyika Desemba 14 kuanzia majira ya saa 3 hadi saa 10 jioni.
  “Kweli juzi kuna mzalendo mmoja alitupigia simu na kututaarifu kuwa kuna kundi la madiwani limetoka Chunya limekuja mkoani kwa lengo la kuwekwa sawa na mmoja wa wagombea na nafasi ya uenyekiti na tulipofuatilia tuliwabaini watu hao ni madiwani,” alisema Mtuka.
  Alisema kuwa madiwani hao walikutwa katika nyumba mbili za kulala wageni za Lucky Inn na Lake Nyasa ambazo zote ziko eneo la Soweto.
  Kamanda Mtuka, alipotakiwa kutaja majina ya madiwani hao na kufafanua vitu walivyokamatwa navyo, hakuwa tayari kutaja na kueleza kuwa sheria namba 23 hairuhusu na suala hilo bado linafanyiwa uchunguzi na ukikamilika taarifu zitatolewa katika vyombo vya habari.
  Alisema waliamua kuwahoji madiwani hao baada ya kubaini kuwepo dalili zinazoashiria vitendo vya rushwa kwa kuwa waliokamatwa ni madiwani ambao ni wapiga kura, pamoja na mmoja wa wagombea wa nafasi ya uenyekiti wa halmashauri.
  CCM leo inafanya uchaguzi wa ndani wa kupata wagombea wa nafasi ya umeya na uenyekiti mikoa yote nchini watakaopambana na wagombea wa vyama vya upinzani.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 15, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,266
  Trophy Points: 280
  SWALI NINALOJIULIZA NI ........................hivi CCM kweli itaweza kupambana na ufisadi wakati viongozi wake ni vinara wa ufisadi......na uongozi huupata kwa ufisadi?
   
 3. m

  matawi JF-Expert Member

  #3
  Dec 15, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Ndo maana Mwakyembe alipendekeza Dr Hosea aondolewe wadhifa lakini mpaka leo Kikwete hataki. Ccm na rushwa ni kama uji na mgonjwa ngumu kutenganisha
   
Loading...