Uchaguzi wa Mwenyekiti CHADEMA utafanyika lini?

Gangongine

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
3,856
2,000
Ni muda mrefu sasa Chama kinachojinasibu kuwa cha Demokrasia kimeendelea kuwa na Mwenyekiti asiye na Ukomo.

Matokeo yake Chama kinazidi kuporomoka kwa kasi ya ajabu kwa kuteua Katibu Mkuu asiye na uwezo na kuitupa Sera ya Kupinga Ufisadi na Kutetea Rasilimali za Nchi.

Kwa kukosa mwelekeo sasa Chama hakina Dira wala Mwelekeo zaidi ya kufanya Vurugu ndani ya Bunge na kukosoa hata yale ambayo yana tija kwa Taifa eti kwa kuwa yanafanywa na CCM.

Ndio maana nauliza hivi hakuna ukomo wa Uenyekiti katika Chama hiki ambacho kilikuwa tishio wakati wa Dr Slaa na kabla ya kuwapokea waliokataliwa na CCM?
 
Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Jan 3, 2012
4,595
2,000
16711977_10206681252908262_8080622556719525945_n.jpg
 
esitena tetena

JF-Expert Member
Aug 21, 2015
1,751
2,000
waacheni wenye chama chao ndio walalamike. muda ukifika watachagua mwenyekiti wao,kama ambavyo ccm walivyovunja katiba ya chama chao kwa "kumkabidhi kijiti" uenyekiti wa ccm taifa rais JPM kabla ya wakati (2017) kwa kisingizio cha "huu ndio utamaduni wa chama chetu."
 
Nyenyere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
13,492
2,000
Ni muda mrefu sasa Chama kinachojinasibu kuwa cha Demokrasia kimeendelea kuwa na Mwenyekiti asiye na Ukomo.

Matokeo yake Chama kinazidi kuporomoka kwa kasi ya ajabu kwa kuteua Katibu Mkuu asiye na uwezo na kuitupa Sera ya Kupinga Ufisadi na Kutetea Rasilimali za Nchi.

Kwa kukosa mwelekeo sasa Chama hakina Dira wala Mwelekeo zaidi ya kufanya Vurugu ndani ya Bunge na kukosoa hata yale ambayo yana tija kwa Taifa eti kwa kuwa yanafanywa na CCM.

Ndio maana nauliza hivi hakuna ukomo wa Uenyekiti katika Chama hiki ambacho kilikuwa tishio wakati wa Dr Slaa na kabla ya kuwapokea waliokataliwa na CCM?
Mbowe akizeeka
 
idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
24,198
2,000
Wanadai katiba mpya ya nchi wakati ya kwao hawana hata uelewa nayo.....

Mbowe onyesha ukomo kuhusu uenyekiti wako ndio uhoji uhalali wa katiba ya Jamuhuri.
 
kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
25,937
2,000
chadema ni chama cha wasanii na wapiga dili,pale hakuna uchaguzi na ole wako uulize uchaguzi wa Taifa ndio utajua nguvu za Mbowe
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom