Uchaguzi 2020 Uchaguzi wa mwaka huu ni mrahisi sana kwa Wapinzani. Chukua fomu kupitia chama chochote kisicho na mwakilishi hapo ulipo, hakika utashinda

PAZIA 3

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
1,070
1,842
Huwezi amini, mwaka huu Uchaguzi ni rahisi Sana kwa wapinzani wote waliochukua fomu kugombea nafasi mbalimbali, sema Kuna maeneo hayajapa wawakilishi hasa vyama chipkizi, nakushauri ndugu yangu, Kama unajiamini, chukua fomu, utashinda mapema tu, ninazo sababu kusema hivyo;

1: Chama chenye nguvu kinaingia kwenye uchaguzi mkuu kikiwa hakijui wapi kwenye serikali ya mtaa wana nguvu au la
2: Wanaingia uchaguzi mkuu wakiwa hawaaminiani, hasa hasila za wajumbe hazijulikani Kama watapoa au watakasilika zaidi
3: Kuna nguvu ya uamsho wa Uhuru na haki, wengi hawaelewi Kama falsafa hii Ina nguvu, ila huwezi amini ccm wanaielewa zaidi kuliko upinzani, hivyo wataiunga mkono kupitia upinzani
4: Wajumbe watapiga kura ya hasila bila kujali Nani kasimama na Nani wa CCM

Chukua fomu ndugu yangu usichelewe, fanya maamzi leo, weka historia maishani mwako, Kuna nafasi za bure upinzani, usiogope kwani baada ya uchaguzi utakuwa mtu mwingine kabisa.

cc Paschal Mayala etal

Fanyeni maamzi leo
 
Back
Top Bottom