Uchaguzi 2020 Uchaguzi wa mwaka huu ni mgumu sana kuwahi kutokea

Duuuu... Unatumia nin kuangalia idadi ya watu maana sote tunatazama kwa macho yote mawili...kampeni rahisi sana kwa ccm tofauti na miaka iliyopita
 
Kama kuna Uchaguzi Mkuu ambao nauona kuwa ndiyo utakuja kuwa Mgumu na huenda hata Kuipasua CCM na Tanzania ni ujao wa mwaka 2025.
Kwel mkuu, uchaguzi wa 2025 ndio utakuwa mgumu lkn huu wa 2020 sio mgumu kwa ccm mana ht 2015 watu walsema n uchaguzi mgumu lkn bd upinzani wakafa kifo cha mende
 
Nikianza kufuatilia trend ya matukio hapa nchini hasa Mh Tundu Lissu anapohusika nashiwishika kuwa kutakuwa na mabadiliko makubwa sana ya kiuongozi hapa nchini:

1. Tunakumbuka suala la UKUTA jinsi Lissu alivyolivalia njuga na ilikuwa bado kidogo tu nchi iandike historia mpya. Hilo likakwama.

2. Likaja suala la makinikia Lissu alisimama kidete kupinga namna suala hilo lilivyochukuliwa kishamba na kipuuzi. Bado tunakumbuka msamiati wa 'Profesorial rubbish'. Leo hii kila mtu ni shahidi jinsi mambo yalivyokwenda. Badala ya kupata $190 billion tumeamhilia $300 million ambazo mpaka sasa tumepata tu $100. Leo hii tujiulize makinikia yako wapi, si wamepewa wenyewe the so called mabeberu? Na hili lilipelekea kipigwa risasi. Lissu ni game changer.

3. Wakadhani dawa ni kumpiga risasi afe ili waendelee na mipango yao ovu. Mungu akasema hapana kuna kazi bado Lissu anatakiwa afanye.

4. Wakakataa kumpa haki yake ya matibabu kulingana na sheria, wakadhani atakuwa kusema maisha yoyote na hawezi kuwa tushio kwai, wapi Mungu akafungua mlango, huyo Ubelgiji. Akapona.

5. Wakadhani anatibiwa kwa mshahara wake wa ubunge, njama zikapangwa ili asipewe mshahara wake. Baada kuzuia kwa miezi 3 kelele zikapigwa, wakaachia.

6. Wakaona sasa ili asipate huo mshahara ni kumfuta ubunge, hilo wakalitekeleza kwa nguvu kubwa. Lakini mbeba maono hakutetereka.

7. Akatangaza kurudi nyumbani na kugombea urais wakadhani ni mzaha, mbeba maono akarudi. Huyo CHADEMA wakampitisha kwa kishindo na kusema NI YEYE. Bado hakuamini walichokuwa wanakiona nankukisikia.

8. Mara huyo ametinga Dodoma kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa, wakashindwa wamnyimeje. Akaanza kuzunguka kutafuta wadhamini, hapo kidogo machale yakaanza kuwacheza na kujua kuwa sio mzaha. Wakapanga njama za kuweka mapingamizi ili asiteuliwe. Mbeba maono kila walichokuwa wanapanga anakipata na kukiweka hadharani. Wakashindwa ikabidi wamteue hasa baada ya kuhisi nguvu kubwa ya umma iliyo nyuma yake.

9. Doh! Kampeni zikaanza, kama vile kidhaifu lakini kadri siku zinavyokwenda ndio anazidi ku gani momentum. Sasa amekuwa tishio, watanzania kwa maelfu wanaunga mkono hoja zake nzito ambazo ccm wameshindwa kuzijibu.

10. Sasa wamebakiwa na njia moja tu kumzuia Lissu asiwe Rais wa awamu ya 6nnayo ni njia ya hatari ya kucheza na kura za watanzania. Mungu ana mpango mkubwa sana kwa watanzania, na mpango huo ameuweka juu ya mabega ya Tundu Antipas Lissu.

Laiti hawa watu wangefuatilia hii trend yote wangejua kuwa sasa wanapambana na Mungu mwenyewe, sasa hiyo vita wataiweza kweli? Tundu Lissu ametumwa na Mungu kuja kuikomboa Tanzania kutoka katika shimo la uharibifu tuliloingizwa ndani ya miaka hii 5. Hili liko wazi na watanzania tujitokeze kwa wingi siku ya kupiga kura ili tukamilishe hiki ambacho Mungu amekiweka mbele ya macho yetu. Ndiyo Mungu analeta mabadiliko kupitia kwa watu. Na hilo liwe onyo kwa walio kwenye madaraka, kuzuia sauti ya wengi ikasikika, ni kupambana na Mungu mwenyewe na hakika hamtashinda.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
CCM haijwahi kushindwa. Nina polisi, nina jeshi, nina usalama wa taifa, nina wakurugenzi, media zote ni za kwangu, coverage ya uchaguzi kwenye TV ni nayo, wasanii ninao, nimejenga miradi mingi kwa mda mfupi, nimeweka watu wangu wote kwenye sehemu nyeti zote sasa wapinzani mna kitu hapo kweli. Upinzani utachukua mda mrefu kutawala nchi hii. Kuangusha huu mti unahitaji Supernatural Power. Lisu kuwa raisi wa nchi hii ni hapo Mungu tu aamuwe mwenyewe kuangusha mti ulioshinda wengi. Kwa maana hiyo lazima kuwe na Supenatiral Power ya kumwezesha Lisu kuwa madarakani.
What type of arsenal can you use to fight peoples' wish? History has proved any usable arsenal useless.
 
Back
Top Bottom