Uchaguzi 2020 Uchaguzi wa mwaka huu ni mgumu sana kuwahi kutokea

Prof Koboko

JF-Expert Member
Aug 15, 2020
350
2,549
Uchaguzi wa mwaka huu ni mgumu sana kuwahi kutokea kwa sababu hizi chache tu;

1. Tundu Lissu ni Mwanasheria mbobevu na makini kiasi kwamba utampa haki yake kiuhalali kabisa.

2. Mpaka sasa CCM pamoja na kutumia wasani wengi na mabango kila kona, bado kampeni zao na ujazaji wa watu uwanjani unafanana na pengine kuzidiwa na CHADEMA.

3. Kwa sababu Wasimamizi wote wa uchaguzi kuanzia Mwenyekiti wake mpaka wasimamizi wasaidizi ni wateule wake woye, bila shaka anafikiria hawawezi kumuangusha. Hapa ndio mwanzo na matatizo yote, tuliona ilivyokua MALAWI tusilichukulie poa hili, Lissu ni mwana siasa mjanja na jeuri siyo sawa na LOWASSA CCM wasijidanganye. Dola haijawahi kushinda umma hilo wafahamu.

4. Miradi mingi aliyoianzisha Magufuli haijamalizika, anafikiri labda atatumia kila njia kuhakikisha anashinda. Hama experience na Umma uliokamilika, asubiri ashinde kwa uhalali maana akishindwa hatarudi tena Ikulu.
 
Kama kuna Uchaguzi Mkuu ambao nauona kuwa ndiyo utakuja kuwa Mgumu na huenda hata Kuipasua CCM na Tanzania ni ujao wa mwaka 2025.
 
Mkuu umenena kweli kabisa, mimi ninahisi baada ya uchaguzi kutakua na patashika, either matokeo yarudiwe kuhesabiwa au vinginevyo lakini kwa jinsi nainavyomjua Lissu, sio mwepesi Magu ajipange sana maana Lissu atamsumbua vya kutosha
 
Katika hali ya kawaida, Ccm hawakutakiwa kutumia nguvu kubwa kupiga kampeni. Lakini kutokana na ujinga wa viongozi wake, wamejikuta kwenye wakati mgumu na kutumia nguvu kubwa kuliko hata wapinzani kwenye kutafuta ridhaa.

Halafu hawajifunzi. Imagine tangu 1961? Halafu bado hawajui Watanzania wana taka nini.
 
Binafsi labda Zanzibar, ila bara labda baadhi ya majimbo tu kama Kawe,Mbeya city,Iringa mjini,Ubungo etc,ila kwa Urais labda Lissu angekuja 2025
 
CCM haijwahi kushindwa. Nina polisi, nina jeshi, nina usalama wa taifa, nina wakurugenzi, media zote ni za kwangu, coverage ya uchaguzi kwenye TV ni nayo, wasanii ninao, nimejenga miradi mingi kwa mda mfupi, nimeweka watu wangu wote kwenye sehemu nyeti zote sasa wapinzani mna kitu hapo kweli. Upinzani utachukua mda mrefu kutawala nchi hii. Kuangusha huu mti unahitaji Supernatural Power.

Lisu kuwa raisi wa nchi hii ni hapo Mungu tu aamuwe mwenyewe kuangusha mti ulioshinda wengi. Kwa maana hiyo lazima kuwe na Supenatiral Power ya kumwezesha Lisu kuwa madarakani.
 
Yani ukiwambia chadema waseme vigezo vya uchaguzi huu kuwa mgumu watakwambia mambo yafuatayo.

1. CCM inatumia wasaa na kusomba watu kwenye kampeni
Majibu ya hii hoja ni kwamba ipo tangu chadema ianze kushiriki uchaguzi kwa mara ya kwanza. Sasa sijui kipya kwa sasa hivi ni kipi?

2. Lissu ni jasiri
Hivi ujasiri wa Lisu unasaidia nini kama hana kura za kumtosha? Kwani huyu Lisu si alikuwepo miaka yote ya uchaguzi? Huo ujasiri wake aliufanyia nini sasa?

3. Lissu ni mwanasheria mahiri
Kwahiyo ushindi unakuja tu kisa wewe ni mwanasheria mahiri? Huna mtaji wa jura nje ya chama chako cha chadema, sasa huo umahiri wako wa sheria utakusaidia kitu gani huku huna kura za kuibiwa?


Lisu atatia aibu kuliko wagombea wote waliowahi kugombea chadema kwa kupata kura kidogo.
 
Back
Top Bottom