Uchaguzi wa mwaka huu ajenda kuu ziwe zipi?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,283
33,887
Hivi watanzania wameshaandaa ni nini wanataka wanasiasa wawatendee wakichaguliwa kuwa viongozi wao? Ajenda kwenye mambo haya ziwe zipi?

  1. Kilimo
  2. Ajira
  3. sayansi na teknolojia
  4. Elimu
  5. Mahusiano ya Kimataifa
  6. Uchumi na biashara
  7. Ulinzi na usalama
  8. Usawa wa kijinsia
  9. Maendeleo ya jamii
  10. Miundombinu na usafirishaji
  11. Haki za raia
  12. Nishati na madini
Au watanzania tunasubiri wanasiasa waje na mipango yao na kutukaririsha kama kasuku?
 
Ngoja nikujibu haraka na kwa kifupi sana, lakini jibu likiwa ndio msingi wa yote uliyoweka hapo juu na mengi mengine ambayo hukuyaweka.

Hatutaki uongozi tunaouchagua utufanye sisi tuliowaweka hapo kuwa kama mali yao wanayoweza kuitumia na kuifanyia yoyote wanayotaka wao hata kama sisi hatuyataki.

Hatutaki uongozi tunaouweka madarakani ndio utufanye kuwa MATEKA wake, tusiweze hata kuuadabisha unapokosea.

Hatutaki uongozi tunaouweka madarakani na kuukabidhi vyombo vyetu vya dola, uvitumie vyombo hivyo kutukandamiza

Tunataka uongozi unaoheshimu katiba yetu, sheria zetu na taratibu tulizojiwekea.
Uongozi huo ukifuata hayo, hayo mengine hapo juu tutayatimiza sisi wenyewe kwa kushirikiana nao.
 
Raisi Magufuli na Team yake wanajua, sisi tunafwata tu!
We! Hizo za kukaa miaka mitano bei za vyakula zinapanda mishahara no? Kazi zinafanywa hakuna kupanda madaraja eti shauri ya daraja la Mfugale?
Au mambo ya kufukuza kazi watu kwa vile kuingia form one alitumia jina la mtu kusoma hadi masters lakini wale waliofeli sekondari kwa vile wanapendwa wanapeta tuu?
Sera za kutunyang'anya korosho zetu kwa kutumia jeshi na kutuacha njia panda huku shangazi zetu wakitishiwa fyoko!
Mwambieni asisumbuke angeaga tuu na kuondoka kwa heshima maana tunakuja na Slogan ya #MwagaPombeKunywaChai

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema yao inajulikana ,hoja ni ruksa ya kufanya mikutano na maandamano kila siku

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app

Maandamano na mikutano wanafanya ccm kila siku, cdm wanaandamana tu haki zinapokiukwa, na wanafanya mikutano kwa ratiba maalum kama haki ya chama cha siasa. Labda useme maandamano ya cdm ni nongwa dhidi ya wakoloni weusi.
 
Raisi Magufuli na Team yake wanajua, sisi tunafwata tu!

Kwa ww ni sawa, mtu yoyote mwenye mawazo ya kijamaa huwa ameondolewa uwezo wa kufikiri, na uwezo wa kufikiri huwa wanakabidhiwa viongozi. Lakini sisi wenye uwezo wa kufikiri tunakuwa na mawazo yetu, na viongozi wanasimamia tu utekelezaji bora wa mawazo yetu. Tabia za kiijinga za kuabudu viongozi zinafanywa na watu wenye uwezo mdogo wa kufikiri.
 
Wapinzani wanapaswa kuja na ahadi ya kushusha bei ya vifaa vya ujenzi vyote ili wananchi waweze kujenga nyumba bora.
 
10 hapa mtaani naona barabara znachongwa vumbi linaongezeka tu, Nikauliza vipi kunani.
Nikajibiwa. " Ni yule diwani wetu aliyepotea toka 2016 July. Hata skuuliza tena bado tupo nyuma Sana ila angalau wananchi nw wameshtukia upuuzi wa wagombea
 
Wewe njoo na ajenda moja tu
(1 ) TWENDE TWENDE (2020) TUKAPIGE CHINI JIWE !
Hapo ndio Litajijua na wasiojulikana wenzake( team pombe)
 
Hivi watanzania wameshaandaa ni nini wanataka wanasiasa wawatendee wakichaguliwa kuwa viongozi wao? Ajenda kwenye mambo haya ziwe zipi?

  1. Kilimo
  2. Ajira
  3. sayansi na teknolojia
  4. Elimu
  5. Mahusiano ya Kimataifa
  6. Uchumi na biashara
  7. Ulinzi na usalama
  8. Usawa wa kijinsia
  9. Maendeleo ya jamii
  10. Miundombinu na usafirishaji
  11. Haki za raia
  12. Nishati na madini
Au watanzania tunasubiri wanasiasa waje na mipango yao na kutukaririsha kama kasuku?
Tunasubiri matusi ya zamani na kubezana
 
Nadhani kwenye madini upande wa masoko wamejitahidi tumeona masoko yako mengi ila kilichoko nyuma ya pazia wauzaji na wachimbaji ama wadau watujuze
 
Tunaambiwa kuwa kilimo ni uti wa mgongo lakini hatuoni vyama vikiweka hadharani nini mipango yao kuhusu Kilimo.
Vyama hata kama vitaweka hadharani mipango yao ya kilimo km sera zetu siyo za kudumu nitatizo 'sera zikibadilshwa majukwaani kwakifupi nyuma ya mikamera hazina tija kwasababu huwezi kupanga ''you can not plan with policies of uncertainty' tumeshudia kwenye wizara ya kilimo upande wa uvuvi wanatumia sera mpya lakini sheria ni za zamani huwezi kufikia malengo
 
Benny Haraba kwa nini kisitokee chama kitakachosema chenyewe kitasimamia sera zake na hakitaruhusu zivurugwe majukwaani kwa kutaka tu sifa za kisiasa??
 
Ngoja nikujibu haraka na kwa kifupi sana, lakini jibu likiwa ndio msingi wa yote uliyoweka hapo juu na mengi mengine ambayo hukuyaweka.

Hatutaki uongozi tunaouchagua utufanye sisi tuliowaweka hapo kuwa kama mali yao wanayoweza kuitumia na kuifanyia yoyote wanayotaka wao hata kama sisi hatuyataki.

Hatutaki uongozi tunaouweka madarakani ndio utufanye kuwa MATEKA wake, tusiweze hata kuuadabisha unapokosea.

Hatutaki uongozi tunaouweka madarakani na kuukabidhi vyombo vyetu vya dola, uvitumie vyombo hivyo kutukandamiza

Tunataka uongozi unaoheshimu katiba yetu, sheria zetu na taratibu tulizojiwekea.
Uongozi huo ukifuata hayo, hayo mengine hapo juu tutayatimiza sisi wenyewe kwa kushirikiana nao.
Hongera sana. Sio wao wageuke kuwa ndio Katiba hata kama wana uhaba wa hekima.
 
Back
Top Bottom