Uchaguzi wa mitaa, chadema yafanya kweli kigoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi wa mitaa, chadema yafanya kweli kigoma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbala-mwezi, Oct 26, 2009.

 1. M

  Mbala-mwezi Member

  #1
  Oct 26, 2009
  Joined: Sep 27, 2009
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna chaguzi ngumu kwa vyama vya upinzani kushinda kama hizi za mitaa. Hata hivyo, katika hali inayoonesha mwanga mpya, majimbo matatu ya mkoa wa Kigoma yanaonesha kukubalimabadiliko ya kweli na Uhuru wa kweli...haya sio mengine..
  kwanza ni jimbo la Kigoma mjini ambalo CHADEMA inaongoza kata7 kati ya 13, ambako kuna mitaa68, mitaa4 uchaguzi umevurugika. CHADEMA imeshinda mitaa33, CUF1.UMD1,CCM29...Mwaka 2004, jimbo hili lilikuwa na mitaa 200, ambapo CCM ilishinda mitaa 110, CHADEMA90....hayo ndio mabadiliko makubwa katika jimbo hilo ngome ya CHADEMA, ambayo mpaka sasa haijajulikana wazi nani anajipanga kuiongoza kupitia CHADEMA 2010, ingawa kuna mpambano mkali ndani ya CCM ambapo zaidi ya watu4 wameshaanza kupambana kila mmoja akitaka awe yeye kupitia CCM 2010.

  Pili, ni jimbo la Kigoma kaskazini, ambalo lipo chini ya Zitto Kabwe, ambalo mwaka 2004, CHADEMA ilishinda vijiji2 tu kati ya 33...Leo, matokeo yaliyopatikana mpaka jioni hii, CHADEMA imeshinda vijiji12, CCM16, na vijiji 5 vilivyopo ukanda wa ziwa Tanganyika matokeo bado hayajapatikana kutokana na ukosefu wa mawasiliano ya simu, na zaidi ni usafiri mgumu kwani boti linachukua takribani masaa8 na zaidi..Haya ndio matokeo ya CHADEMA katika jimbo hili, ambalo Mh Zitto hakuweza kufanya kampeni hata siku moja, japo alichangia gharama za kampeni na kuamuru wanakijiji wapambane na kila aina ya mbinu chafu za CCM na serikali yake katika uchaguzi....
  Tatu ni jimbo la Kigoma kusini ambalo mwaka 2004, upinzani ukiongozwa na CHADEMA, ukifuatiwa na NCCR na CUF kwa mbali ulifanikiwa kushinda vijiji27 kati ya 43....mpaka sasa vijiji 8 vilivyopo ukanda wa ziwa na ambako ni ngome ya CHADEMA matokeo hayajapatikana kutona na usafiri na mawasiliano duni...mpaka sasa CHADEMA imeshinda vijiji8, NCCR8,CUF2...hili ni jimbo ambalo kwa sasa kutoka upinzani linawaniwa na vijana wawili, Afisa Habari wa CHADEMA David Kafulila26, na Mdhamini wa chama, kijana wa kiasia, Muslim Asanary26....kutoka vyama vingine bado hakuna fununu kabisa hasa baada ya ngome ya NCCR iliyopo kata ya Nguruka kuwa nyuma ya David Kafulila..
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Kwa mbaali watz wantaka kutoka usingizini.
   
 3. M

  Malila JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Nawapa tano ndugu zangu wa Kigoma.
   
 4. M

  MkuyuMkubwa Member

  #4
  Oct 26, 2009
  Joined: Sep 27, 2009
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM inapaswa kujuta kujenga barabara mbili za rami ndani ya jimbo la zitto, huku majimbo mengine hayajapata barabara tangu uhuru...hapa wamefanya kosa kisiasa...nilikuwa kigoma kikazi wiki mbili zilizopita...hoja ni hiyo tu!....wanataniana...kitendawili....tega! serikali imejenga barabara ya kwanza ya rami mkoani wapi?....ukisema kigoma kaskazini, unaambiwa umekosa! ukisema kwa zitto kabwe...ndo umepata! hawa ni watoto kabisa wa shule ya msingi....barabara hizi za rami kwa zitto ni pigo kubwa kwa ccm2010....
   
 5. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Haya mawazo ndio yale ya kina Sumaye kuwa yeyote anayekuwa mwanachama wa upinzani ni kuuwa hata biashara zake. Nilidhani wewe unaishi kwa mizizi hadi leo, lkn nikashangaa uliposema ulikuwa huko Kigoma kikazi. Niliishauri kama kweli hukwenda kutafuta mizizi! lakini mbona unajua kusoma na kuandika na zaidi hata kutumia mtandao? hapa kuna walakini.
   
 6. M

  MkuyuMkubwa Member

  #6
  Oct 26, 2009
  Joined: Sep 27, 2009
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kumradhi NONO...unajua sikulenga huko...nimesema ni kosa walofanya kisiasa kwasababu CCM walidhani kwa kujitahidi kufanya baadhi ya mambo ndani ya jimbo hilo labda ingekuwa hoja ya wao kujipendekeza kwa watu wa jimbo hilo....lakini wananchi wameichukua tofauti ingawa ndio usahihi, kwani wanasema "ili serikali ilete maendeleo tuchague upinzani" kwaiyo karata ya CCM ni garasa
   
 7. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  CCM wako madarakani na kuwapelekea maendeleo wananchi ni haki ya wananchi hao bila ya kujali itikadi zao . Najua yes CCM watakuwa wamedhani wanamuumiza Zitto na waitumie kama kigezo lakini why Chalinze iwe zaidi ya Kigoma ? Hongera wana Kigoma wipe CCM off the map if you can please.
   
 8. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2009
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Pumba completely
   
 9. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mie nashangazwa na wasomi na wakazi wa Dar eti wanaichukia CCM lakini hawasaidii Upinzani kuchukua uongozi unafiki bwana .

  Tarime ikoje kule ?

  Arusha mabomu yametembea kama kawaida kuhakikisha CCM inashinda .
   
 10. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Du, Chama Cha Majambazi...kimeanza sasa...Mkuu kuna Lt. Makamba nini uko...anaongoza vita?
   
 11. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #11
  Oct 26, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Mkuyu Mkubwa,

  Mimi nadhani hii ni credit kwa chama chochote kitakachopata nafasi ya kuongoza serikali na ndio kujijengea uhalali wa kuendelea kuwepo. Hii ni mishale japo michache kuwa tunaweza kuvumiliana na kufanya kazi pamoja kama watanzania. Hii imewapa wanakigoma nafasi ya kuvipima vyama vya siasa kuwa nani wampe nafasi badala ya ule ubabe wa kina Mkapa na sumaye ambao waliwaadhibu wananchi wasiokuwa na hatia kwa sababu tu waliwachagua upinzani.

  Jambo kubwa wanalotakiwa kutekeleza ccm ni kupiga marufuku na kuachana vitendo vya kununua viongozi waliochaguliwa kutoka vyama vya upinzani, ili kuipa Tanzania afya yake ndani ya miaka michache ijayo. Ninatoka jimbo tulilomchagua mbunge wa upinzani wakati wa uchaguzi wa mwanzo wa vyama vingi, ninafahamu adhabu mkapa aliyoitoa kwa miaka 10 ya utawala wake, zaidi tulishuhudia katika chaguzi zilizofuata wakiwanunua madiwani na wenyeviti wa vijiji, kweli ccm ilifilisika na kupoteza haki ya kuwa chama cha waTanzania.
   
 12. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #12
  Oct 26, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Safi sana sana hayo mabadiliko yangeambukizwa kwingine Tanzania ingekombolewa.
   
 13. M

  Malila JF-Expert Member

  #13
  Oct 26, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Taratibu tutafika.
   
 14. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #14
  Oct 26, 2009
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Jamani nanimwenye data za Ubungo? Nnahamu sana ya kujua mijitokeo ya hii sehemu.....kwangu huko mazee
   
 15. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #15
  Oct 26, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Umewapa ushauri wa bure lakini CCM hawawezi kusikiliza maana walisha zoea kukwapua kura na ndiyo maana wanaibiana hata wenyewe kwa wenyewe na wanalia .So hawawezi kuelewa hawa .Wacha wananchi waamke wawabane kwa nguvu
   
 16. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #16
  Oct 26, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Hiyo niliyo bold inanifanya niwe na woga, Hapo ilitakiwa kuwa "Imeshinda", kwani ni nani asiyejua kuwa matokeo ya mwisho yatatoka makao makuu ya nchi?, kuwa msiwape ushindi au wapeni. Mnakumbuka chaguzi ndogo?, Biharamulo et al, kilifanyika nini?
   
 17. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #17
  Oct 26, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni lazima CCM ikubali mabadiliko na wabadilike. Hongera sana Kigoma kwani CCM walibweteka
   
Loading...