Uchaguzi wa Meya Manispaa ya Kigoma waahirishwa

Zitto

Former MP Kigoma Urban
Mar 2, 2007
1,562
10,879
Katika hatua ya kushangaza kabisa, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji ameahirisha uchaguzi wa Meya. Katika Halmashauri hii CHADEMA ina madiwani wengi zaidi ya CCM na nafasi ya Meya na Naibu Meya ni ya chama chetu.
Mkurugenzi wa Manispaa amesema kapigiwa simu na Waziri wa TAMISEMI na kumwagiza aahirishe. Nimewasiliana na Waziri wa nchi TAMISEMI mhe Mkuchika na amesema yupo Newala na hajatoa agizo hilo na kwamba Serikali inaendeshwa kwa maandishi.
CCM wamegoma kuja kikaoni. Mkurugenzi kakimbia kikao na ofisi. CHADEMA imetimiza quoram lakini kikao hakifanyiki.
This is democracy at its best.
 
Mh!mbona tulipata habari kuwa Chadema hawawezi kuongoza halmashauri hiyo mbaka washirikiane na NCCR MAGEUZI!!Mambo yamebadilika tena!tafdhani tunaomaba ufafanunuzi mheshimiwa Zitto!!
 
Kigoma mjini inanishangaza sana. 2005 CHADEMA ilipata madiwani wengi lakini wakakosa ubunge. Mwaka huu tena hayo yamejirudia, kuna nini huko?
 
Mhh kweli Mh.Zitto hii ndiyo demekorasia tunayopigania kuijenga? Tuna safari ndefu katika kuifikia demokrasia ya kweli. Katika hali ya kawaida kama mna madiwani wachache kuliko chama kingine ni obvious matumaini ya ushindi hayapo nafikiri sasa wanataka kutafuta ushindi wa mezani. Sasa hata hilo baraza la madiwani haliwezi kuzinduliwa na hivyo madiwani hawawezi kuanza kutkeleza rasmi majukumu yao kwasababu ya uroho wa madaraka wa watu wachache.

Kweli Tanzania ni zaidi ya uijuavyo!
 
Tumeamua kuwa hatutatoka katika kikao mpaka uchaguzi ufanyike. CCM wanafanya mchezo wa kijinga sana. Tumewazidi madiwani. Hawataki kutupa Council yetu. Wanakaa kwenye vikao RC, DC na wengine kuhujumu. Wajue tu huu mji ni wa CHADEMA na labda watuue, Umeya ni wetu.
 
Kwanini halmashauri ambazo CCM uwezo wa kupata Meya ni mdogo kuna kuwa na mizengwe mingi? Maana tumeona Mwanza,Arusha nk hali ni tete?
 
Katika hatua ya kushangaza kabisa, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji ameahirisha uchaguzi wa Meya. Katika Halmashauri hii CHADEMA ina madiwani wengi zaidi ya CCM na nafasi ya Meya na Naibu Meya ni ya chama chetu.
Mkurugenzi wa Manispaa amesema kapigiwa simu na Waziri wa TAMISEMI na kumwagiza aahirishe. Nimewasiliana na Waziri wa nchi TAMISEMI mhe Mkuchika na amesema yupo Newala na hajatoa agizo hilo na kwamba Serikali inaendeshwa kwa maandishi.
CCM wamegoma kuja kikaoni. Mkurugenzi kakimbia kikao na ofisi. CHADEMA imetimiza quoram lakini kikao hakifanyiki.
This is democracy at its best.

Nashukuru kusikia haya kutoka kwako Zitto, mengi sana yamesemwa kwenye vyombo vya habari lakini nadhani njia pekee ya kujibu na kuwaziba midomo wote wanaotilia shaka uanachama wako wa Chadema ni kusimamia masilahi ya Chama mpaka kieleweke
 
Kigoma mjini inanishangaza sana. 2005 CHADEMA ilipata madiwani wengi lakini wakakosa ubunge. Mwaka huu tena hayo yamejirudia, kuna nini huko?

Hata mimi huwa inanishangaza sana!labda wagombea ubunge mara kwa mara huwa hawakubaliki!!Au Peter Serukamba amejizatiti sana!!
 
Mh!mbona tulipata habari kuwa Chadema hawawezi kuongoza halmashauri hiyo mbaka washirikiane na NCCR MAGEUZI!!Mambo yamebadilika tena!tafdhani tunaomaba ufafanunuzi mheshimiwa Zitto!!
Kigoma kuna Halmashauri 4, halmashauri ya Kibondo pekee ndio CCM wana majority. Halmashauri ya Wilaya Kasulu NCCR wanaongoza kwa msaada wa CHADEMA, Halmashuri ya wilaya Kigoma inaongozwa na CHADEMA kwa msaada wa NCCR na Manispaa ya Kigoma inaongozwa CHADEMA peke yake.
 
Wanasiasa wa siku hizi mnashangaza sana, hamkawii kutumia neno 'kuuliwa' au 'kumwaga damu'

Hivi Zitto wewe uko tayari kufa kwa ajili ya umeya kwa chama au ni maneno tu ya kisiasa?
 
Yaleyale ya kutangaza matokeo katika uchaguzi mkuu sehemu ambazo wamebwagwa. Wajue kabisa kuwa kama wanafanya kitu kupunguza idadi ya madiwani wa CDM basi wajue kila mmoja atakayepungua wa CDM wao watatu watapungua. Huu ni upumbavu wa kulewa madaraka. Kweli katiba mpya ni muhimu. Mambo yote haya yanapaswa kuzingatiwa katika katiba mpya
 
Nashukuru kusikia haya kutoka kwako Zitto, mengi sana yamesemwa kwenye vyombo vya habari lakini nadhani njia pekee ya kujibu na kuwaziba midomo wote wanaotilia shaka uanachama wako wa Chadema ni kusimamia masilahi ya Chama mpaka kieleweke

Acha kuchemka mkuu!yaani kwa kuandika hii posts basi umeridhika kabisa na uanachama na utiifu kwa Chadema!au ndiyo unafiki kwa kuwa yupo hapa!!kuwa mkweli!MIMI BINAFSI SINA IMANI NA ZITTO KAMA NILIVYOKUWA NINAIMANI NAYE SIKU ZA NYUMA!NILIHISI KWA KUWA HUYU NI KIJANA MWENZETU BASI UKOMBOZI WA KWELI UNAKUJA.lAKINI KWA BAHATI MBAYA MATUMAINI YANGU YAMEYEYUKA KAMA THERUJI.
 
ccm wanachotaka watu waingie mtaani wapate sababu ya kumaliza hasira zao...wananchi wamewachoka hamuelewi nini?
 
Kigoma kuna Halmashauri 4, halmashauri ya Kibondo pekee ndio CCM wana majority. Halmashauri ya Wilaya Kasulu NCCR wanaongoza kwa msaada wa CHADEMA, Halmashuri ya wilaya Kigoma inaongozwa na CHADEMA kwa msaada wa NCCR na Manispaa ya Kigoma inaongozwa CHADEMA peke yake.

Nashukuru sana kwa ufafanuzi mzuri mkuu!!
 
Tumeamua kuwa hatutatoka katika kikao mpaka uchaguzi ufanyike. CCM wanafanya mchezo wa kijinga sana. Tumewazidi madiwani. Hawataki kutupa Council yetu. Wanakaa kwenye vikao RC, DC na wengine kuhujumu. Wajue tu huu mji ni wa CHADEMA na labda watuue, Umeya ni wetu.
Kinachotokea kinatukumbusha machungu na maumivu tuliyoyapata kwenye uchaguzi Mkuu pale tulipokuwa tunadai Matokeo ya Wabunge wetu wa Chadema ila ninachoamini nikwamba kwa Matokeo ya Umeya uchakachuaji hauwezekani nyie simameni Kidete kuhakikisha HAKI inachukua mkondo wake.
 
Katika hatua ya kushangaza kabisa, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji ameahirisha uchaguzi wa Meya. Katika Halmashauri hii CHADEMA ina madiwani wengi zaidi ya CCM na nafasi ya Meya na Naibu Meya ni ya chama chetu.
Mkurugenzi wa Manispaa amesema kapigiwa simu na Waziri wa TAMISEMI na kumwagiza aahirishe. Nimewasiliana na Waziri wa nchi TAMISEMI mhe Mkuchika na amesema yupo Newala na hajatoa agizo hilo na kwamba Serikali inaendeshwa kwa maandishi.
CCM wamegoma kuja kikaoni. Mkurugenzi kakimbia kikao na ofisi. CHADEMA imetimiza quoram lakini kikao hakifanyiki.
This is democracy at its best.

Limenikuna hilo.....nafurahi bado uko chamani...
 
Tumeamua kuwa hatutatoka katika kikao mpaka uchaguzi ufanyike. CCM wanafanya mchezo wa kijinga sana. Tumewazidi madiwani. Hawataki kutupa Council yetu. Wanakaa kwenye vikao RC, DC na wengine kuhujumu. Wajue tu huu mji ni wa CHADEMA na labda watuue, Umeya ni wetu.

Huo ndio uamuzi unaofaa komaeni mpaka kieleweke wanachi wenyewe walishawapa hiyo halmashauri hakuna wakuwapoka
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom