uchaguzi wa Mayor wa London na Watanzania.

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,571
mwezi huu siku ya sikukuu ya wafanyakazi Jiji la London waliweza kuchagua Mayor wao japo siku hiyo ilikuwa ni siku ya wafanyakazi ila chama cha wafanyakazi/Labour kilishindwa kuitumia siku hiyo vizuri ili kujipatia ushindi na kujikuta kinaangukia pua .

Kwa wale waliokuwa wanafuatilia kwa ukaribu uchaguzi huu kuna jambo la kuangalia kwa kina hapa na kujiuliza ulikuwa wapi ushiriki wa watanzania waishio London?

Naambiwa kuwa wananchi wa nchi nyingine za kiafrika waishio humo london waliweza kujikusanya na kumuunga mkono mgombea wa kundi ama chama kimojawapo ila hilo kwa wenzangu watanzania waishio londoni halikuweza kufanyika .

Kama watanzania hawataki kuwa sehemu ya mafanikio ama hata ya kushindwa wakiwa huku huko ugaibuni kuna tatizo gani?

Nimejaribu kuuliza na kuambiwa kuwa waGhana waishio Londoni waliweza kukutana na wagombea wote wawili wa Labour na mstahiki meya aliyeshinda Borris na kuwauliza ni mambo gani watawafanyia .

Wananchi wa Nigeria na haswa wale waishio miji ya Enfield,Reading na kwingineko nao waliweza kujikusanya na na wagombea hao na kuwauliza wananini kipya kwa ajili yao kama wakiwapa kura .

Ila kwa watanzania hakuna hata mmoja ambaye alitaka kujihusisha na kundi mojawapo kuna tatizo gani kwa watanzaia wenzangu?

Nimejiuliza maswali haya baada ya kufanya utafiti wa kina na kuona jinsi ambavyo watanzania waishio london walivyonyuma na kujihusisha na mambo ya kila siku .

Kujihusisha kungewawezesha kujulikana na hata kupata recognition kuwa kumbe na wao wapo hapo london,la ajabu ni kuwa wanaishi wenyewe wenyewe tuu je?ni kuwa wanaishi humo kiharamu ama kihalali?
 
Watanzania wa hapa London ni wanafiki tuu kwani wao wanajua zaidi kujipigia makelele kwenye JF na wao kulaumu vyama huko Tz TUU ila wao wenyewe ni kama gunia la chumvi.

Najua wapo watakaonishambulia sana ila ndio ukweli huo, mlishindwa kukiunga hata mkono chama cha Green?
 
Lawama zingine ni kama kufurahisha genge, hivi mna uhakika gani kwamba Watanzania hawakushiriki kwenye uchaguzi huo?

Sio kila mtu anawezakuwa activist wa vyama na pia idadi ya Watanzania wazoefu London ni ndogo sana ukilinganisha na hayo makundi mengine.

Watanzania wengi tu wanapiga kura. Ondoeni hilo kundi kubwa la vijana Watanzania ambao wengi hao wanahangaika na shule na maisha, hata huo muda wa kujishughulisha na mambo ya vyama unafikiri watatoa wapi? Inatakiwa tuwe realistic tunapojadili haya mambo.

Watanzania wengi walimpigia Ken lakini ndio hivyo kura hazikutosha.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom