Uchaguzi wa marudio: Mbowe kunguruma leo muheza-tanga


Mbelwa Germano

Mbelwa Germano

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2011
Messages
789
Likes
2
Points
0
Mbelwa Germano

Mbelwa Germano

JF-Expert Member
Joined May 7, 2011
789 2 0
Leo Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA Mhe. Freaaman Mbowe atawahutubia wakazi wa kata ya Genge na Tengeni wilayani Muheza katika mwendelezo wa kampeni za uchaguzi wa marudio unaotarajiwa kufanyika jumapili ya tarehe tarehe 16/06/2013. Wakazi wa kata hizi wanamsubiri kwa hamu Kamanda Mbowe ambapo anatarajiwa kuwasili na helicopter muda si mrefu.

Katika kuhakikisha kwamba CHADEMA inashinda katika uchaguzi wa Udiwani katika kata mbili jimbo la Muheza, Katibu wa Kanda ya Kaskazi Ndugu. Amani Golugwa ameweka kambi Muheza kuongeza nguvu za mashambulizi akiongozana na Makamanda wengine wa Kanda ya Kaskazini. Hii ni kuhakikisha kwamba CHADEMA inaibuka na ushindi katika kata zote zenye uchaguzi kanda ya Kaskazini.

Ushindi wa kata hizi ni itakuwa ishara ya CHADEMA kuendelea kukubalika katika maeneo mengi na kuthibitisha kwamba hakuna ngome ya CCM kwenye nchi hii. Kwa muda mrefu CCM imekuwa ikijigamba kwamba Mkoa wa Tanga ni ngome yao na hata wakati Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga Ndugu. Henry Daffa Shekifu akichangia bungeni kujigamba kwamba Tanga ni ngome imara na madhubuti

KATIKA HATUA NYINGINE


Jaribio la Chama Cha Mapinduzi(CCM) kuwashawishi Wenyeviti wa vijiji kupitia CHADEMA Jimbo la Bumbuli kujiuzulu nafasi zao umeshindikana. Hii ni baada ya Mwenyekiti wa Kijiji cha Kwekitui kukana kuhusika kuandika barua ya kujiuzulu kwenda kwa Mtendaji wa Kijiji hicho. Barua hii ya kughushi iliandikwa kuwahadaa wananchi kwamba Mwenyekiti wa kijiji amejiuzulu.

Mwezi ulipita kulitokea utata baada ya Mwenyekiti huyu kutonekana kwenye eneo lake la kazi baada ya viongozi wa CCM kumshawishi na kutoa lugha za vitisho dhidi yake kujitoa katika nafasi yake na hivyo kujenga hasira kwa wakazi wa kijiji cha Kwekitui.

Aidha katika muendelezo wa tabia hii ya vitisho kwa Wenyeviti wa vijiji kujiengua katika nafasi zao vimefanyika katika kijiji cha Milungui jimbo la Lushoto baada ya Mwenyekiti wa kijiji hicho kupitia CHADEMA kutoa taarifa juu ya hila anazofanyika katika utendaji wa majukumu yake.
 

Forum statistics

Threads 1,275,229
Members 490,947
Posts 30,536,233