Uchaguzi wa marudio kesho tar.16.12.2014 nchi nzima.

Emmanuel J. Buyamba

Verified Member
May 24, 2013
1,073
2,000
Ndugu watanzania taarifa nilizozipokea hivi punde na kuthibitishwa na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Msalala mkoani ni Shinyanga ndio hizo.
Inasemekana kuna waraka toka TAMISEMI makao makuu kwenda wilaya zote umetumwa mchana wa leo.
Kiukweli hii Tamisemi haijawatendea haki wananchi hapa.Hii ni kwa sababu jana walisema marudio ni Jumamosi ijayo.
Wito:wafuasi hasa wa UKAWA jiridhisheni na hili na kama ni kweli basi fanyeni kila mbinu kuwafahamisha wapiga kura wetu.CCM na TAMISEMI kuna jambo wanalitaka ndio maana wametukurupusha iwe kesho.

Nawasilisha!!!.
======================

UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA WAFANIKIWA KWA ASILIMIA 98

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Mh. Hawa Ghasia akiri mapungufu katika Uchaguzi wa Serikali Mitaa uliofanyika jana, asema serikali itawachukulia hatua watendaji wake watakaobainika kufanya uzembe na hata kama ni yeye asema yuko tayari kuwajibika.

Uchaguzi kurudiwa Jumamosi na Jumapili katika baadhi ya maeneo.

Chanzo:IPP Media
 
murumbasi

Member
Dec 3, 2014
75
0
Tunakuomba Mhe. Rais umuajibishe Waziri - Ofisi ya Waziri Mkuu- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. Kwa kweli amekuangusha na kukuabisha mbele ya Wananchi unaowaongoza. Huyu Mama habebeki.
 
Kingmairo

JF-Expert Member
Apr 7, 2012
4,940
2,000
Kwa maana ingine serikali inasema walimu wasiende kufundisha, madaktari wasiende kutibu, makarani wasiende ofisini, mahakimu wasiende mahakamani katika maeneo hayo ili wakapige kura kwenye maeneo yao. Huu utakuwa ni ujinga uliopitiliza
 
Kaitampunu

JF-Expert Member
Nov 24, 2011
1,938
2,000
Kwa maana ingine serikali inasema walimu wasiende kufundisha, madaktari wasiende kutibu, makarani wasiende ofisini, mahakimu wasiende mahakamani katika maeneo hayo ili wakapige kura kwenye maeneo yao. Huu utakuwa ni ujinga uliopitiliza
Kwa utawala huu wa dhaifu kila kitu kinawezekana.
 
kinauche

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
7,682
2,000
Kama ni kwelinitnis extremely serious. Wengi jana hawakupoga kura kwa sababu ya ibada. Walishaambiwa wabadilishe siku ya kupiga kura hawataki. Sasa wanatoa taarifa ghafla. Kunani
 
Emmanuel J. Buyamba

Verified Member
May 24, 2013
1,073
2,000
Mods hebu tusaidieni kuwapata watu wa TAMISEMI sasa hivi watupe tamko.Tayari huku kwenye kata Kahama na Msalala wasimamizi wamepewa nakala kuwa uchaguzi kesho.
 
laticka

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
346
225
Hawa magamba wanasaka kila namna ya kuiba kufa ...na watahangaika sana shenzi zao
 
Not_Yet_Uhuru

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
1,304
0
Tunakuomba Mhe. Rais umuajibishe Waziri - Ofisi ya Waziri Mkuu- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. Kwa kweli amekuangusha na kukuabisha mbele ya Wananchi unaowaongoza. Huyu Mama habebeki.

Acha mzaha Murumbasi...wewe unafikiria kuwa makosa yanayofanyika ktk chaguzi ni ya bahati mbaya!, au tume na Tamisemi hawayajui?? Rais na PM Pinda wanayajua vyema...hakuna kificho hapo!
..Na hivyo Waziri huyu kilaza Hawa Ghasia anaongea tu ktk kutekeleza malengo ya genge zima la CCM na sio makosa yatakayomfanya eti awajibishwe hata kidogo.! Kwa lipi? hili ni kosa kubwa kuliko mengi makubwa ambayo Rais anagugumia kuyatolea maamuzi? ESCROW unaijua shuruba yake kitaifa na kimataifa? usiombe kujua kuwa hawaupati usingizi hawa jamaa...Ujangili je? Usafirishaji wa Unga je? Uangamizaji Albino je?
...Hili la kuvurugwa kwa Kura za Serikali za Mitaa sio almanusura...bali ni 'Special Project' na kuwa kuharibika ndio 'mission accomplished' hiyo ndiyo inayowawezesha kuchanganya mabox, watu kukata tamaa, na wenyewe kuweka kura zao watakavyo! ...hii inayooonyesha kuwa CCM haipo tena hewani ..'not reachabo'! inakufa sawia...inahemea kuiba, kuharibu, kuchakachua, visingizio na kuchukua njaa za wananchi kama mtaji wa kutawala, ila wanazidi kuerevuka...siku zao CCM zinahesabika!
 
fundi25

JF-Expert Member
Apr 16, 2013
10,202
2,000
Vijana tupo tayari kwa mapambao muda wowote hatuongwi tunakwenda moja kwa moja kuhamasishana kesho wawe tiari haswa kituo chamwenge ccm wanakiwinda hata kwa kumwaga damu kama noma na iwe nouma !!
 
MAGAMBA KILLER

Senior Member
Mar 22, 2013
148
195
mimi ninabaki nashangaa kwa maana hawa magamba wameamua kutumia mbinu ya kuahirisha jana ili ufanyike kesho kwa kujua kwamba hasa maeneo ya kata ya bugarama kuna wafanyakazi wengi na ambao kwa siku ya kesho watakuwa kazini ili wasipige kura. ninaendelea kuamini kwamba kweli ndani ya mbinu 400 za kuiba kura hii ni mojawapo pia.
 
The Red Pen

JF-Expert Member
Sep 26, 2014
518
225
Acha mzaha Murumbasi...wewe unafikiria kuwa makosa yanayofanyika ktk chaguzi ni ya bahati mbaya!, au tume na Tamisemi hawayajui?? Rais na PM Pinda wanayajua vyema...hakuna kificho hapo!
..Na hivyo Waziri huyu kilaza Hawa Ghasia anaongea tu ktk kutekeleza malengo ya genge zima la CCM na sio makosa yatakayomfanya eti awajibishwe hata kidogo.! Kwa lipi? hili ni kosa kubwa kuliko mengi makubwa ambayo Rais anagugumia kuyatolea maamuzi? ESCROW unaijua shuruba yake kitaifa na kimataifa? usiombe kujua kuwa hawaupati usingizi hawa jamaa...Ujangili je? Usafirishaji wa Unga je? Uangamizaji Albino je?
...Hili la kuvurugwa kwa Kura za Serikali za Mitaa sio almanusura...bali ni 'Special Project' na kuwa kuharibika ndio 'mission accomplished' hiyo ndiyo inayowawezesha kuchanganya mabox, watu kukata tamaa, na wenyewe kuweka kura zao watakavyo! ...hii inayooonyesha kuwa CCM haipo tena hewani ..'not reachabo'! inakufa sawia...inahemea kuiba, kuharibu, kuchakachua, visingizio na kuchukua njaa za wananchi kama mtaji wa kutawala, ila wanazidi kuerevuka...siku zao CCM zinahesabika!

Well Said...!!!!!!!!
 
RockSpider

JF-Expert Member
Feb 16, 2014
6,864
1,500
Hawa Ghasia amepanic anahisi kutemwa kwenye uwaziri... Tayari wameliboronga na kuna mwelekeo wa kuboronga Zaidi....
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom