Uchaguzi wa marudio: CCM wanajiandaa kutekeleza utapeli wa karne

simplemind

JF-Expert Member
Apr 10, 2009
16,418
9,206
Hivi kwa nini ZEC inasisitiza kutotoa majina ya wagombea wa CUF kwenye karatasi za kupiga kura? Tangazo la Jecha tarehe 22 au 23 au machi- wanzabari asilimia 90 wamejitokeza kura ya marudio kinyume na matarajio ya wengi.Dkt Shein ameshinda kwa kupata asilimia 55 za kura. CCM imeshinda nusu ya majimbo Pemba pamoja kunyakua majimbo matatu unguja yaliyoshindwa na CUF uchaguzi wa awali. Nachukua nafasi kumpongeza Rais wa Muungano kwa msimamo wake madhubuti kuhusu mkwamo wa kisiasa Zanzibar. Pos nawapongeza wanzanzibari kwa kujitokeza kwa wingi kuchagua viongozi wao halali. Punde baada hii TBC inataangaza Rais Magu apongeza Dkt Shein kwa ushindi kishindo na Wanzazibari kwa kuwa na imani kubwa na chama tawala! The writing is on the wall.
 
Na hapo ndipo Zanzibar italipuka kwa vilio na maombolezo badala ya vifijo na nderemo, busara za hali ya juu zinahitajika katika hili suala.
 
Uchaguzi wa Marudio mpambano bado ni Mkali sana mshindi hajulikani mpaka sasa acheni uchochezi
 
Uchaguzi wa Marudio mpambano bado ni Mkali sana mshindi hajulikani mpaka sasa acheni uchochezi

Wewe Pohamba vipi, mpambano na mshindi hajulikani wakati timu pinzani imegoma kuingia uwanjani! Naona unajitoa ufahamu kwa kitu kilicho wazi.

Vv
 
Wewe Pohamba vipi, mpambano na mshindi hajulikani wakati timu pinzani imegoma kuingia uwanjani! Naona unajitoa ufahamu kwa kitu kilicho wazi.

Vv

Timu zote zipo uwanjani na ndio maana picha na Majina yao yapo kwny karatasi za kupigia kura, walichofanya ni kushawishi mashabiki wao wasije kuwashangilia kitu ambacho hakiharamishi Pambano!!
 
Timu zote zipo uwanjani na ndio maana picha na Majina yao yapo kwny karatasi za kupigia kura, walichofanya ni kushawishi mashabiki wao wasije kuwashangilia kitu ambacho hakiharamishi Pambano!!
Umejivua akili lini ?
 
Cku ikifika kila kona ulikofanyika uchaguzi itakuwa wazi kuelezewa nn kilijiri na nani mshindi. Yetu macho na masikio Muda utakapofikia
 
Back
Top Bottom