Uchaguzi wa Marekani umemalizika, tumeona umuhimu wa kujenga taasisi imara sio watu imara

Hilo ni somo tosha!Nawashangaa watu wanaotumia Marekani kama mfano wa kuwa na wao hawana demokrasia,huwa hawaoni angle ambayo mleta mada umeiweka!

Jambi kubwa ni kuwa taasisi haziko kumtumikia mtawala,ziko kwa ajili ya interest za wananchi!
Wananchi ndiyo chanzo cha madaraka yote na kwao mamlaka zote huwekwa.Hayo yanapopuuzwa na watawala,Wananchi wawajibike.
 
Kwani hapa kwetu wafuasi wa Magu wakijaribu kushinikiza atangazwe tu hata kama hajashinda wataachwa tu wafanye watakalo?
Ndicho walichofanya October 2020 hata kabla hawajaamrishwa,wanajipendekeza haraka sana.
 
Kwani hapa kwetu wafuasi wa Magu wakijaribu kushinikiza atangazwe tu hata kama hajashinda wataachwa tu wafanye watakalo?

mara ngapi bashiri anasema watatumia dolla kushinda na hafanywi kitu na kwanamna hiyo haki haitakuwepo
 
Naona umejaribu kutafuta "angle" nzuri ya kupenyeza ajenda yako katika hili.

Inawezekana ni kweli hizo taasisi unazozisema zikawa na nguvu na kutekeleza majukumu yao kulingana na matakwa ya wananchi.

Lakini Marekani wana taasisi nyingi sana zenye majukumu mbalimbali hivyo tukio hili pia limetufunza kwamba katika masuala ya kiusalama ilitakiwa Donald trump apitie vinu vikali kabla ya jina lake kupendekezwa mgombea wa uraisi mwaka 2015.

Hilo ni kosa namba moja, kumwachia mtu kama Donald Trump ambae mpaka sasa anaonekana ana mapungufu kiakili, kushika ofisi kubwa duniani ya uraisi na kukalia vitufe vya makombora ya nyuklia.

Pili, kuhusu ghasia za Capitol ni kwamba hakukuwepo polisi wa kutosha kwenye first barrier of security hivyo kulipotokea breach ikawa ngumu kwa polisi wachache walokuwepo kukabiliana na uwingi wa wafanya vurugu.

Hivyo hakukuwepo mpangilio maalum au planning kwamba Capitol pana mjadala wa kumpitisha Biden hivyo security lazima ingekuwa "beefed up".

Na mwisho ni kushindwa kwa integensia kutambua kuwepo na mpango wa vurugu hizo ambazo zimesababisha vifo vya watu watano akiwepo askari polisi.

Yaani vyombo vya kijasusi vya Marekani NSA, FBI na vingine kushindwa kubaini mipango ya vurugu, hapo pia tuna la kujifunza kwa upande wetu kama kainchi ka Afrika.

Ila vyombo vya usalama vya Tanzania pamoja na kauwezo vilivyo navyo vilijiandaa mapema kabla, wakati na baada ya uchaguzi na moja ya maeneo ya kuyaangalia kwa ukaribu ilikuwa ni mitandao ya kijamii na kuhakikisha Tweeter haitumiwi vibaya kusambaza taharuki.
Asante Richard kwa kuangalia angle hiyo, si kwamba intelijensia yao ilikuwa haijui bali kuna habari kuwa Trump alikuwa briefed lkn akawa mzito kutoa maamuzi ya kuongezwa ulinzi (askari) wakutosha kwa sababu zake hadi makamu Spence alipoingilia kati dk za mwisho. Na hilo ni kosa mojawapo atakaloshitakiwa kati ya mengi waliyopanga kumshitaki baada ya muda wake kwisha.
 
Wewe ndio ulishafeli. Kibaraka wenu aliwaambia mtoke muandamane mkaingia mitini. Sasa hapo nani kafeli ?
Mimi sina kibaraka kama ufikiriavyo na uwezo wa mdogo wa kusoma alama za nyakati hao hao unaowaita vibaraka wa mabeberu kuna muda utahitaji msaada wao lakini hutofanikiwa kwa sababu umependa ujinga na upumbavu.
 
Naona umejaribu kutafuta "angle" nzuri ya kupenyeza ajenda yako katika hili.

Inawezekana ni kweli hizo taasisi unazozisema zikawa na nguvu na kutekeleza majukumu yao kulingana na matakwa ya wananchi.

Lakini Marekani wana taasisi nyingi sana zenye majukumu mbalimbali hivyo tukio hili pia limetufunza kwamba katika masuala ya kiusalama ilitakiwa Donald trump apitie vinu vikali kabla ya jina lake kupendekezwa mgombea wa uraisi mwaka 2015.

Hilo ni kosa namba moja, kumwachia mtu kama Donald Trump ambae mpaka sasa anaonekana ana mapungufu kiakili, kushika ofisi kubwa duniani ya uraisi na kukalia vitufe vya makombora ya nyuklia.

Pili, kuhusu ghasia za Capitol ni kwamba hakukuwepo polisi wa kutosha kwenye first barrier of security hivyo kulipotokea breach ikawa ngumu kwa polisi wachache walokuwepo kukabiliana na uwingi wa wafanya vurugu.

Hivyo hakukuwepo mpangilio maalum au planning kwamba Capitol pana mjadala wa kumpitisha Biden hivyo security lazima ingekuwa "beefed up".

Na mwisho ni kushindwa kwa integensia kutambua kuwepo na mpango wa vurugu hizo ambazo zimesababisha vifo vya watu watano akiwepo askari polisi.

Yaani vyombo vya kijasusi vya Marekani NSA, FBI na vingine kushindwa kubaini mipango ya vurugu, hapo pia tuna la kujifunza kwa upande wetu kama kainchi ka Afrika.

Ila vyombo vya usalama vya Tanzania pamoja na kauwezo vilivyo navyo vilijiandaa mapema kabla, wakati na baada ya uchaguzi na moja ya maeneo ya kuyaangalia kwa ukaribu ilikuwa ni mitandao ya kijamii na kuhakikisha Tweeter haitumiwi vibaya kusambaza taharuki.
Watu wangapi wameuwawa Zanzibar pamoja na kujiandaa kote huko unakokusema?
 
Nani kapindua matokeo hapa kwetu ? Toka kampeini zilipoanza hapa kwetu mgombea uraisi wa upinzani ni kutoa matusi tu bila hoja za msingi. Unategemea angeshinda uraisi huyo ? Pinga pinga popote duniani mwisho wao ni huwa ni shaba tu kama ilivyotokea kwa hao wanaojiita wanademokrasia ( USA ).
USA aliyeuwawa kwa Risasi ni mmoja tu,tena baada ya kuonekana anatoa silaha!Ameuwawa pia askari mmoja na wengine watatu ni medical condition so acha upotoshaji wako hapa!
 
Marekani ndio waje wajifunze kwetu maana ni aibu kubwa kwa Taifa kama lile kufanya uchaguzi kwa kelele.
Ni wazi viongozi wa Marekani wamekosa Political torelance.
No democracy in U. S wao ndio waje wajifunze kwetu.
😁😁😁😁😁,wakija kujifunza huku basi Trump angeendelea kutawala kwa awamu nyingine hata kama kashindwa!
 
Wao ndio wanachakujifunza kutoka Kwetu Haiwezekani wahuni waandamane waongie kwe ye ofisi za Bunge, sisi Tumefanikiwa kuwatoa vibaraka waliotakwa kuuza nchi yetu, na taasisi zetu Imara zilihakikisha hakuna vurugu za kudumu muda mlefu
Taasis gani imara hapa bongo?Zote ziko kwa ajili ya kumtumikia mtawala na matakwa yake hata kama si halali!

Trump angekuwa Tanzania angeamrisha tume ifute matokeo ya uchaguzi,kule alizuia mpaka kukimbilia mahakamani lakini Mahakama ikapuuza hoja zake!
Huku kwetu tunakumbuka 2015 baada ya Maalim Seif kushinda Zanzibar,ikatoka amri kuwa ZEC ifute uchaguzi na ikafanya hivyo huku jeshi likizingira ZEC!Wakafanya yao!

Kama unamaanisha Trump aje kujifunza mbinu za Kijecha basi sawa,ila sasa hizo mbinu kwa Marekani haziwezi kufanya kazi maana hakuna taasisi ambayo ipo kumtumikia!
 
Marekani ndio waje wajifunze kwetu maana ni aibu kubwa kwa Taifa kama lile kufanya uchaguzi kwa kelele.
Ni wazi viongozi wa Marekani wamekosa Political torelance.
No democracy in U. S wao ndio waje wajifunze kwetu.
Waje Afrika kujifunza demokrasia ya kung’ang’ania madaraka?
 
Wao ndio wanachakujifunza kutoka Kwetu Haiwezekani wahuni waandamane waongie kwe ye ofisi za Bunge, sisi Tumefanikiwa kuwatoa vibaraka waliotakwa kuuza nchi yetu, na taasisi zetu Imara zilihakikisha hakuna vurugu za kudumu muda mlefu
Donald Trump ndiye aliwashawishi watu waandamane, huku akiwaita ni watu mhimu sana. Siku hii ya jana katika hotuba yake anasisitiza kuwa Marekani inaendeshwa kwa mujibu wa sheria na Katiba, na watu wote waliofanya maandamano na kusababisha MADHARA watachukuliwa HATUA

Trump akili zake sometime kama za Bashiru wa ccm
 
Maana ya kuwa na taasisi imara siyo jeshi kujichukulia sheria mkononi na kutumia nguvu kumnyamazisha anayepinga.
 
Ukiwa na mahaba sana kumbe unakuwa kipofu?

Hujaona kama kuna watu zaidi ya 4 wamekufa sababu ya huo uchaguzi?

Msichokijua ni kwamba hata huko ukileta ujinga unakula shaba kama hivyo. Nyie hapa mkila virungu mnakimbilia kwa kina Amsterdam.

Naomba pia niulizie kwa Pompeo kama atatoa tamko juu ya vifo hivyo.
Trump mwenyewe ameshatoa kauli kulaani kitendo hapa kwetu je?
 
Uchaguzi wa Marekani umemalizika rasmi leo usiku kwa Rais mteule Joe Biden kuthibitishwa na mabunge yote mawili kuwa rais wa nchi hiyo baada ya rais Trump kwa kipindi cha miezi miwili kuhangaika kupinga matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika Novemba mwaka jana.

Tulichojifunza zaidi ni jinsi uchaguzi huu ulivyofanyika na mapungufu yake yalivyofanyiwa kazi na vyombo husika chini ya mihimili mitatu ya nchi hiyo na jinsi utawala wa sheria ulivyoheshimiwa na demokrasia kuachwa ichukue mkondo wake.

Baada ya matokeo kutangazwa Trump alipeleka malalamiko yake Mahakamani akipinga matokeo ya baadhi ya majimbo, mahakama ikasema malalamiko yake hayakuwa na msingi wowote kwa vile hayana ushahidi.

A district court in Nevada shot down the Trump’s claims, finding “that there is no credible or reliable evidence that the 2020 General Election was affected by fraud.”

Jumamosi 2/1/2021 simu ya Trump ilidukuliwa akimpigia Afisa Tume ya uchaguzi wa Georgia Brad Raffensperger akitaka atafute kura 11,780 za ushindi akakataliwa.

“I just want to find 11,780 votes, which is one more than we have. Because we won the state," said Trump on call.

“President Trump, we’ve had several lawsuits, and we’ve had to respond in court to the lawsuits and the contentions," Raffensperger told Trump on the call. "We don’t agree that you have won."

Siku chache kabla ya Bunge la Congress kukutana kuthibitisha ushindi wa Biden, Makamu wa rais Mike Pence alikataa shinikizo la boss wake Trump la kumtaka kuingilia kati matokeo ya kura Electral College Votes na kuzuia kuthibitishwa kwa Rais mteule Jo Biden, Pence alimwambia hana uwezo huo.

"Our Founders were deeply skeptical of concentrations of power and created a Republic based on separation of powers and checks and balances under the Constitution.”

"The Presidency belongs to the American people, and to them alone," Pence told Trump.

Huu ni uthibitisho kuwa viongozi wengi walisimamia haki, utawala wa sheria, imagine makamu wa rais wa Tanzania au nchi yeyote ya Afrika angekataa maelekezo ya rais aliye madarakani.

Baada ya Trump kuona ugumu wa kuitumia mihimili ya Mahakama, Ofisi ya rais White House na Bunge, suluhisho la mwisho lilikuwa ni kuwatumia wafuasi wake na baadhi ya wabunge wa chama chake kuvamia bunge na kujaribu kuzuia mjadala wa kumthibitisha Biden kwa nguvu jaribio ambalo nalo halikufanikiwa.

Mitchell McConnell wa chama cha REPUBLICAN chama anachotoka TRUMP ndani ya Congress alisema;

"I will vote to respect the American people’s decision & defend our system of government. My full remarks".

Kwa Tanzania ni mbunge gani wa chama tawala anaweza kumwambia hivyo rais aliye madarakani.

Pamoja na wafuasi wa Trump kuvamia na kuingia hadi kwenye ukumbi wa bunge na ofisi ya Spika hatukuona polisi kutumia nguvu kupita kiasi kuwatawanya, najiuliza ingekuwa Dodoma watu wamevamia bunge kiasi hicho wakati huu tungekuwa na vifo vingapi na gereza la Isanga lisingetosha.

Pamoja na hayo yote leo Trump amekubali kukabidhi madaraka ifikapo 20/1/2021. Bila taasisi imara leo Trump asingekubali kutoka madarakani.

Tujifunze kuheshimu taasisi zetu, katiba na sheria tulizojitungia na tuache uhuru wa wananchi kufikisha hisia zao kwa vyombo vinavyohusika. Tutumie uchaguzi wa Marekani kuwa kama somo kwetu hasa kwa watawala wa nchi zetu za ki Afrika wanaojiona wao kama miungu watu, kuwa hakuna aliye juu ya sheria hata kama ni rais.
WEWE NI MMOJA WA WANAOLINDWA NA MODERATORS NDIYO SABABU POST ZAKO ZA NCHI ZA NJE ZINALINDWA! ZA WENZAKO HAZICHUKUI DAKIKA ZINATUPWA KULE.
 
Back
Top Bottom