EllySkyWilly
JF-Expert Member
- Aug 28, 2020
- 2,204
- 2,083
Marekani ndio waje wajifunze kwetu maana ni aibu kubwa kwa Taifa kama lile kufanya uchaguzi kwa kelele.Uchaguzi wa Marekani umemalizika rasmi leo usiku kwa Rais mteule Joe Biden kuthibitishwa na mabunge yote mawili kuwa rais wa nchi hiyo baada ya rais Trump kwa kipindi cha miezi miwili kuhangaika kupinga matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika Novemba mwaka jana.
Tulichojifunza zaidi ni jinsi uchaguzi huu ulivyofanyika na mapungufu yake yalivyofanyiwa kazi na vyombo husika chini ya mihimili mitatu ya nchi hiyo na jinsi utawala wa sheria ulivyoheshimiwa na demokrasia kuachwa ichukue mkondo wake.
Baada ya matokeo kutangazwa Trump alipeleka malalamiko yake Mahakamani akipinga matokeo ya baadhi ya majimbo, mahakama ikasema malalamiko yake hayakuwa na msingi wowote kwa vile hayana ushahidi.
A district court in Nevada shot down the Trump’s claims, finding “that there is no credible or reliable evidence that the 2020 General Election was affected by fraud.”
Jumamosi 2/1/2021 simu ya Trump ilidukuliwa akimpigia Afisa Tume ya uchaguzi wa Georgia Brad Raffensperger akitaka atafute kura 11,780 za ushindi akakataliwa.
“I just want to find 11,780 votes, which is one more than we have. Because we won the state," said Trump on call.
“President Trump, we’ve had several lawsuits, and we’ve had to respond in court to the lawsuits and the contentions," Raffensperger told Trump on the call. "We don’t agree that you have won."
Siku chache kabla ya Bunge la Congress kukutana kuthibitisha ushindi wa Biden, Makamu wa rais Mike Pence alikataa shinikizo la boss wake Trump la kumtaka kuingilia kati matokeo ya kura Electral College Votes na kuzuia kuthibitishwa kwa Rais mteule Jo Biden, Pence alimwambia hana uwezo huo.
"Our Founders were deeply skeptical of concentrations of power and created a Republic based on separation of powers and checks and balances under the Constitution.”
"The Presidency belongs to the American people, and to them alone," Pence told Trump.
Huu ni uthibitisho kuwa viongozi wengi walisimamia haki, utawala wa sheria, imagine makamu wa rais wa Tanzania au nchi yeyote ya Afrika angekataa maelekezo ya rais aliye madarakani.
Baada ya Trump kuona ugumu wa kuitumia mihimili ya Mahakama, Ofisi ya rais White House na Bunge, suluhisho la mwisho lilikuwa ni kuwatumia wafuasi wake na baadhi ya wabunge wa chama chake kuvamia bunge na kujaribu kuzuia mjadala wa kumthibitisha Biden kwa nguvu jaribio ambalo nalo halikufanikiwa.
Mitchell McConnell wa chama cha REPUBLICAN chama anachotoka TRUMP ndani ya Congress alisema;
"I will vote to respect the American people’s decision & defend our system of government. My full remarks".
Kwa Tanzania ni mbunge gani wa chama tawala anaweza kumwambia hivyo rais aliye madarakani.
Pamoja na wafuasi wa Trump kuvamia na kuingia hadi kwenye ukumbi wa bunge na ofisi ya Spika hatukuona polisi kutumia nguvu kupita kiasi kuwatawanya, najiuliza ingekuwa Dodoma watu wamevamia bunge kiasi hicho wakati huu tungekuwa na vifo vingapi na gereza la Isanga lisingetosha.
Pamoja na hayo yote leo Trump amekubali kukabidhi madaraka ifikapo 20/1/2021. Bila taasisi imara leo Trump asingekubali kutoka madarakani.
Tujifunze kuheshimu taasisi zetu, katiba na sheria tulizojitungia na tuache uhuru wa wananchi kufikisha hisia zao kwa vyombo vinavyohusika. Tutumie uchaguzi wa Marekani kuwa kama somo kwetu hasa kwa watawala wa nchi zetu za ki Afrika wanaojiona wao kama miungu watu, kuwa hakuna aliye juu ya sheria hata kama ni rais.
Ni wazi viongozi wa Marekani wamekosa Political torelance.
No democracy in U. S wao ndio waje wajifunze kwetu.