Uchaguzi wa Marekani umemalizika, tumeona umuhimu wa kujenga taasisi imara sio watu imara

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,269
Uchaguzi wa Marekani umemalizika rasmi leo usiku kwa Rais mteule Joe Biden kuthibitishwa na mabunge yote mawili kuwa rais wa nchi hiyo baada ya rais Trump kwa kipindi cha miezi miwili kuhangaika kupinga matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika Novemba mwaka jana.

Tulichojifunza zaidi ni jinsi uchaguzi huu ulivyofanyika na mapungufu yake yalivyofanyiwa kazi na vyombo husika chini ya mihimili mitatu ya nchi hiyo na jinsi utawala wa sheria ulivyoheshimiwa na demokrasia kuachwa ichukue mkondo wake.

Baada ya matokeo kutangazwa Trump alipeleka malalamiko yake Mahakamani akipinga matokeo ya baadhi ya majimbo, mahakama ikasema malalamiko yake hayakuwa na msingi wowote kwa vile hayana ushahidi.

A district court in Nevada shot down the Trump’s claims, finding “that there is no credible or reliable evidence that the 2020 General Election was affected by fraud.”

Jumamosi 2/1/2021 simu ya Trump ilidukuliwa akimpigia Afisa Tume ya uchaguzi wa Georgia Brad Raffensperger akitaka atafute kura 11,780 za ushindi akakataliwa.

“I just want to find 11,780 votes, which is one more than we have. Because we won the state," said Trump on call.

“President Trump, we’ve had several lawsuits, and we’ve had to respond in court to the lawsuits and the contentions," Raffensperger told Trump on the call. "We don’t agree that you have won."

Siku chache kabla ya Bunge la Congress kukutana kuthibitisha ushindi wa Biden, Makamu wa rais Mike Pence alikataa shinikizo la boss wake Trump la kumtaka kuingilia kati matokeo ya kura Electral College Votes na kuzuia kuthibitishwa kwa Rais mteule Jo Biden, Pence alimwambia hana uwezo huo.

"Our Founders were deeply skeptical of concentrations of power and created a Republic based on separation of powers and checks and balances under the Constitution.”

"The Presidency belongs to the American people, and to them alone," Pence told Trump.

Huu ni uthibitisho kuwa viongozi wengi walisimamia haki, utawala wa sheria, imagine makamu wa rais wa Tanzania au nchi yeyote ya Afrika angekataa maelekezo ya rais aliye madarakani.

Baada ya Trump kuona ugumu wa kuitumia mihimili ya Mahakama, Ofisi ya rais White House na Bunge, suluhisho la mwisho lilikuwa ni kuwatumia wafuasi wake na baadhi ya wabunge wa chama chake kuvamia bunge na kujaribu kuzuia mjadala wa kumthibitisha Biden kwa nguvu jaribio ambalo nalo halikufanikiwa.

Mitchell McConnell wa chama cha REPUBLICAN chama anachotoka TRUMP ndani ya Congress alisema;

"I will vote to respect the American people’s decision & defend our system of government. My full remarks".

Kwa Tanzania ni mbunge gani wa chama tawala anaweza kumwambia hivyo rais aliye madarakani.

Pamoja na wafuasi wa Trump kuvamia na kuingia hadi kwenye ukumbi wa bunge na ofisi ya Spika hatukuona polisi kutumia nguvu kupita kiasi kuwatawanya, najiuliza ingekuwa Dodoma watu wamevamia bunge kiasi hicho wakati huu tungekuwa na vifo vingapi na gereza la Isanga lisingetosha.

Pamoja na hayo yote leo Trump amekubali kukabidhi madaraka ifikapo 20/1/2021. Bila taasisi imara leo Trump asingekubali kutoka madarakani.

Tujifunze kuheshimu taasisi zetu, katiba na sheria tulizojitungia na tuache uhuru wa wananchi kufikisha hisia zao kwa vyombo vinavyohusika. Tutumie uchaguzi wa Marekani kuwa kama somo kwetu hasa kwa watawala wa nchi zetu za ki Afrika wanaojiona wao kama miungu watu, kuwa hakuna aliye juu ya sheria hata kama ni rais.
 
Hilo ni somo tosha! Nawashangaa watu wanaotumia Marekani kama mfano wa kuwa na wao hawana demokrasia,huwa hawaoni angle ambayo mleta mada umeiweka!

Jambo kubwa ni kuwa taasisi haziko kumtumikia mtawala,ziko kwa ajili ya interest za wananchi!
 
Ukiwa na mahaba sana kumbe unakuwa kipofu?

Hujaona kama kuna watu zaidi ya 4 wamekufa sababu ya huo uchaguzi?

Msichokijua ni kwamba hata huko ukileta ujinga unakula shaba kama hivyo. Nyie hapa mkila virungu mnakimbilia kwa kina Amsterdam.

Naomba pia niulizie kwa Pompeo kama atatoa tamko juu ya vifo hivyo.
 
Ukiwa na mahaba sana kumbe unakuwa kipofu?

Hujaona kama kuna watu zaidi ya 4 wamekufa sababu ya huo uchaguzi?

Msichokijua ni kwamba hata huko ukileta ujinga unakula shaba kama hivyo,. Nyie hapa mkila virungu mnakimbilia kwa kina Amsterdam.

Naomba pia niulizie kwa Pompeo kama atatoa tamko juu ya vifo hivyo.
Wamekufa majambazi wa rais Trump level moja na akina bashite hawajafa waungwana wa nchi bali wale waliokuwa wanataka kutapeli uchaguzi halali wa rais.
 
Wamekufa majambazi wa rais Trump level moja na akina bashite hawajafa waungwana wa nchi bali wale waliokuwa wanataka kutapeli uchaguzi halali wa rais.
Ok. Ni kama wale majambazi waopigwaga virungu huku kwetu kwa kujaribu kupinga matokeo?

Hapo nmekuelewa. Na wengine hadi wamekimbia nchi.
 
Hilo ni somo tosha!Nawashangaa watu wanaotumia Marekani kama mfano wa kuwa na wao hawana demokrasia,huwa hawaoni angle ambayo mleta mada umeiweka!
Jambi kubwa ni kuwa taasisi haziko kumtumikia mtawala,ziko kwa ajili ya interest za wananchi!
Hii ndiyo hoja kubwa ambayo kuna watu huwa hawataki kuiona. Taasisi za Marekani ni mfano wa kuigwa. Kikubwa hapa ni taasisi IMARA na HURU.

Watanzania hapa tuzungumzie taasisi HURU siyo taasisi zinazosikiliza nani anasema nini.
 
Mkuu leo ukipita Pale KTM mbagala pembeni kulikua kuna malori lukuki siku hizi hayapo,,ukipita kisemvule kuna kiwanda cha cement leo yamebaki magofu, ukipita Quality center hivyo hivyo, Dangote nae kafunga, sababu tu ni sifa za watu wachache kiukweli serikali hii ni ya hivyo kuliko zote.

Ni vigumu sis Watanzania kuwa na taasisi imara kwani asilimia kubwa ya raia wake wanapenda sifa hivyo kuwa kiongozi mkuu wa nchi wajibu wake ni kuabudiwa na kusifiwa.
 
Ukiwa na mahaba sana kumbe unakuwa kipofu?

Hujaona kama kuna watu zaidi ya 4 wamekufa sababu ya huo uchaguzi?

Msichokijua ni kwamba hata huko ukileta ujinga unakula shaba kama hivyo,. Nyie hapa mkila virungu mnakimbilia kwa kina Amsterdam.

Naomba pia niulizie kwa Pompeo kama atatoa tamko juu ya vifo hivyo.
Hao wanne waliokula shaba unajua ni wa upende wa Trump? Nchi zetu za Africa hilo linawezekana? Jaribu kuiangalia hoja ya mleta mada kwa upana wake zaidi, kuliko kujikita kwenye hoja ya watu wanne waliouawa na polisi wakati wa kuzuia wafuasi wa Trump wasiingie kwenye ukumbi wa bunge.
 
Ok. Ni kama wale majambazi waopigwaga virungu huku kwetu kwa kujaribu kupinga matokeo?

Hapo nmekuelewa. Na wengine hadi wamekimbia nchi.
Huku hakuna taasisi imara ni maagizo kutoka juu mara moja yanatekelezwa kama ingekuwa kwetu kitendo cha rais Trump kupinga matokeo jeshi la polisi lingemsapoti,mahakama ingemsapoti,chama chake kingemsapoti,makamu wa rais angemsapoti,usalama wa taifa wangemsapoti na Biden mpaka wa leo angalikuwa korokoroni upo.
 
Hao wanne waliokula shaba unajua ni wa upende wa Trump? Nchi zetu za Africa hilo linawezekana? Jaribu kuiangalia hoja ya mleta mada kwa upana wake zaidi, kuliko kujikita kwenye hoja ya watu wanne waliouawa na polisi wakatai wa kuzuia wafuasi wa Trump wasiingie kwenye ukumbi wa bunge.
Kwani hapa kwetu wafuasi wa Magu wakijaribu kushinikiza atangazwe tu hata kama hajashinda wataachwa tu wafanye watakalo?
 
Huku hakuna taasisi imara ni maagizo kutoka juu mara moja yanatekelezwa kama ingekuwa kwetu kitendo cha rais Trump kupinga matokeo jeshi la polisi lingemsapoti,mahakama ingemsapoti,chama chake kingemsapoti,makamu wa rais angemsapoti,usalama wa taifa wangemsapoti na Biden mpaka wa leo angalikuwa korokoroni upo.
Huo ni mtazamo wako!
 
Mwambie. Labda kwa mifano hiyo anaweza kukuelewa.
 
Achana na ujinga wa hao wamarekani, uchaguzi umeonyesha madhaifu ya hiyo wanayoita demokrasia. Uchaguzi toka mwaka jana mtu ameshindwa anapigia tu kelele. Ndio maana sisi tuna taasisi imara kama jeshi la polisi, ukishindwa umeshindwa unakaa kimya.

Kwa uimara wa jeshi letu hakuna hata mjinga mmoja aliyesogeza pua yake nje eti kuandamana kupinga matokeo, hao wamarekani mpaka watu wanaingia kwnye jengo la bunge ni upuuzi tu, ni muhimu huku kwetu polisi waimarishwe zaidi na kupewa meno, ili wajinga wachache na vibaraka wa mabeberu watakaotaka kuiga hayo ya wamarekani waadabishwe wapugwe mpaka wachakaee.
 
Kwani hapa kwetu wafuasi wa Magu wakijaribu kushinikiza atangazwe tu hata kama hajashinda wataachwa tu wafanye watakalo?
Polisi wapi watajaribu kuwasumbua? Kuna mambo mengine jisikilize hata wewe mwenyewe utapata majibu. Hebu fuatilia hii mada uone kama kuna mwingine mwenye mtazamo kama wako. Penye ukweli watu wanaona ndugu.
 
Obama alisema "Afrika haitaji maraisi wazuri bali taasisi bora na imara" sas nakubali alichosema huyo nguli wa siasa na utawala bora duniani. Kilicho mfanya Trump kusema Pooo ni mifumo.

Kila aliyempa maelekezo aliyakaa mpk makamu wake kasema MZEE SIWEZ PINDUA MAAMUZI YA WAMAREKANI. Sisi Wauni wanapindua maamuz yetu na tunacheka. Cku yaja haiko mbali hata kama kwa miaka itafika tutaheshimiana.
 
Obama alisema "Afrika haitaji maraisi wazuri bali taasisi bora na imara" sas nakubali alichosema huyo nguli wa siasa na utawala bora duniani. Kilicho mfanya Trump kusema Pooo ni mifumo. Kila aliyempa maelekezo aliyakaa mpk makamu wake kasema MZEE SIWEZ PINDUA MAAMUZI YA WAMAREKANI. Sisi Wauni wanapindua maamuz yetu na tunacheka. Cku yaja haiko mbali hata kama kwa miaka itafika tutaheshimiana.
Crimea aione hii.
 
Back
Top Bottom