Uchaguzi wa Marekani 2020: Watu wanne wamefariki baada ya wafuasi wa Trump kuvamia Bunge

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
Polisi imethibitisha kuwa mwanamke mmoja aliyepigwa risasi wakati wa vurugu zilizotokea baada ya wafuasi wa Trump kuvamia bunge, amefariki dunia kwasababu ya majeraha aliyopata.

Bado maafisa hawajataja jina la mwanamke huyo lakini polisi wanasema alikuwa raia wa kawaida.

Aidha, mtu mwingine amepigwa risasi wakati wa vurugu zilizotokea ndani ya bunge la Marekani, kulingana na shirika la habari la Associated Press.

Lindsay Watts, mwanahabari wa shirika lenye kuhusishwa na Fox News, ameandika ujumbe kwenye Twitter kuwa wahudumu wa afya wa Washington DC walisema juhudi za kumuokoa mwanamke mmoja aliye kwenye hali mahututi zinaendelea baada ya kupigwa risasi kifuani.

Wafuasi wa Trump waliokuwa na hasira waliandamana huku wakiimba, "Tunamtaka Trump" huku mmoja wao akipigwa picha akiwa ameketi kwenye kiti cha rais wa bunge la Seneti.

Polisi Washington imesema kuwa ni wazi waandamanji hao walikuwa tayari kutumia nguvu yoyote ile kuingia katika majengo ya bunge.

Inasemekana hadi kufikia sasa watu 13 na silaha tano zimenaswa na polisi wakati ghasia zinaendelea bungeni.

Maafisa polisi wa Washington DC wamesema wamepata bunduki tano ikiwemo za mkononi na ndefu.

Mkuu wa polisi Robert Contee amewaambia wanahabari kuwa waliokamatwa sio wakazi wa eneo la DC.

Baada ya uvamizi huo uliochukua saa kadhaa, afisa anayesimamia mipangilio ya bungeni alitangaza kuwa sasa jengo hilo limenusuriwa na vikosi vya usalama.

Wakati mmoja Bwana Trump alilazimika kurekodi ujumbe kwenye video na kuutuma katika mtandao wa Twitter akitoa wito kwa wafuasi wake kuondoka katika majengo ya bunge lakini naye akawa anaendelea madai yasiokuwa na ushahidi wowote kuwa Democrats waliiba kura.

Lakini kukawa na ishara kidogo zinazoonesha kwamba waandamanaji hao wanatii wito wa Trump unaowataka warejee nyumbani licha ya kwamba mji huo wote unatekeleza hatua ya kutoka nje kuanzia saa kumi na mbili jioni hadi kumi na mbili asubuhi.

"Najua machungu yenu, najua mumevunjika moyo," Trump alisema. "Lakini lazima sasa murejee nyumbani, lazima tuwe na amani ... hatutaki yeyote ajeruhiwe."

Bwana Biden kwa upande wake amesema maandamano hayo "yamesababishwa na uchochezi na ni lazima hilo likome sasa", amesema.

Wanajeshi na maafisa wa polisi pia wamepelekwa katika majimbo jirani huku maafisa wa shirika la ujasusi FBI wakipelekwa katika majengo ya bunge kusaidiana na maafisa wa polisi.

Pia amethbitisha kuwa baadhi ya maafisa wanapata matibabu baada ya kujeruhiwa.

Wafuasi wa Donald Trump wenye hasira wamevuka mipaka ya usalama iliyowekwa na kusimama kandokando ya bunge huko Washington, wakati wabunge wanakutana kumuidhinisha rais mteule Joe Biden kama mshindi wa uchaguzi uliofanyika Novemba mwaka jana.

Katika matukio ya kutatanisha, waandamanaji walizunguka jengo la bunge huku wabunge nao wakisindikizwa kutoka bungeni humo na polisi.

Bwana Biden alisema huo ni "uasi", huku Bwana Trump kwa upande wake akatoa ujumbe kwa njia ya video akiwataka wafuasi wake kutoka bungeni na kurejea nyumbani.

Kikao cha pamoja cha bunge kuidhinisha ushindi wa Bwana Biden kimeahirishwa na bunge limelazimika kwenda mapumzikoni.

Kuna taarifa kuwa watu walitumia bunduki kwenye jengo hilo .Pia mabomu ya kutoa machozi yametumika kutawanya waandamanaji.
 
Uchaguzi umekwisha na mshindi amepatikana, tatizo lililotokea sasa mgombea mmoja hataki kushindwa! Ameenda mahakamani nalo ameshindwa licha ya yeye kuwa ndiye aliyeko madarakani!...
Kumbe hata wanao jiita vinara wa demokrasia duniani wanaandamana kupinga matokeo.

Maana yake nikwamba labda hapakuepo na uhuru,uwazi na haki.
Kweli dunia duara
 
"Wafuasi wa Trump waliokuwa na hasira waliandamana huku wakiimba, "Tunamtaka Trump" huku mmoja wao akipigwa picha akiwa ameketi kwenye kiti cha rais wa bunge la Seneti."

Kumbe Marekani wanajua kuzungumza Kiswahili fasaha hivi?🤔
 
Kumbe hata wanao jiita vinara wa demokrasia duniani wanaandamana kupinga matokeo.

Maana yake nikwamba labda hapakuepo na uhuru,uwazi na haki.
Kweli dunia duara
Samahani siwezi kuendelea na Post hii baada ya Moderators kuiondoa na kuunganisha na kitu kingine.
 
Kumbe hata wanao jiita vinara wa demokrasia duniani wanaandamana kupinga matokeo.

Maana yake nikwamba labda hapakuepo na uhuru,uwazi na haki.
Kweli dunia duara
Niliwahi kusema uendeshaji wa demokrasia duniani ni uleule bali sura ya demokrasia ya sehemu husika uonwa kwa mtizamo tofauti na sehemu nyingine! Nikaongeza kuwa demokrasia ya US hapishani sana na ya kwetu!!! Kwa maelezo haya nilishambuliwa kweli kweli na wanaojinasibu wabobezi wa maduala ya demokrasia.

La uchaguzi wa mwaka uliopita wa US na matukio yaliyoendelea jana liwafunue nyuso wale walionishambulia na kuelew msingi wa hoja yangu!
 
Sikuwahi kumkubali Trump.

Bora angeshinda Yule mama Hillary

Mimi wote sikuwahi kuwapenda,, maana kila anaeingia anaingia na sera zake, zaidi kuwakandamiza na kuwauwa waislamu na kuwaibia rasilimali zao. labda kidogo Bill clinton hapo sawa.


Ndio maana sinaga time ya kuwafatiria wendawazimu kama hawa wasio na utu.,,, mi nadhani tuwaachie wenzetu wa upande wa pili waendelee kuwashobokea hawa manaswara wenzao.
 
Watu wa haki za binadamu wanasemaje au ndio wamekaa kimya,mabalozi wa nchi za magharibi wapo kimya.
 
Mimi nazungumzia hao wanne waliokufa,sijawasikia human rights kukemea hiko kitendo au US hawapo.
Mashirika ya haki za binadamu sanjari na viongozi mbalimbali barani Ulaya wamekwisha kemea.

Pengine wewe, ulitaka wakemee kwa namna gani?
 
Back
Top Bottom