Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,467
- 113,582
- Thread starter
- #81
Kwenye hili la mgombea binafsi, nakubaliana na wewe, ila mashujaa wa kweli, siku zote hupambana by giving it a try na sio kuwa only a barking dogs seldom bite!.Hayo unayoyasema ni kweli na ndivyo inavyopaswa iwe! , lakini Aliyemteua Jecha ndiye aliyeteua hao majaji.
Kama aliamuriwa avunje sheria ya Zec kwa kufuta matokeo unilaterally with impunity, usishangae na hao wengine pamoja na kuujua ukweli wakashinikizwa wa rule otherwise, na kwa gharama yoyote!
Historia iko wazi, kwa matokeo ya kesi ya mgombea binafsi, jinsi ilivyohukumiwa ni somo
CUF wangejaribu, dunia ingewaelewa!. Hicho kimya chao ndicho kimepelekea hili igizo la uchaguzi wa marudio kufanyika, na kwa sheria zetu mbovu, baada tuu ya kutangazwa mshindi, the end justify the means!, kwa sasa no one can do anything else!, the goal posts zimehamishiwa 2020.
Kuna kanuni inasema uwongo ukisemwa sana na ukaachwa bila kukanushwa hugeuka ndio ukweli wenyewe!, vivyo hivyo haramu ikiachwa kubaki haramu, hugeuka ni halali, kwa sababu hakuna yeyote aliyechukua hatua yoyote kuizuia hiyo haramu, hivyo igizo la uchaguzi huo ni huru na wa haki na limetupatia viongozi halali!.
Pasco