Msambichaka Mkinga
JF-Expert Member
- Oct 22, 2015
- 1,649
- 2,908
Hivi kunapokuwa na wagombea wa chama kimoja, unasubiria matokeo gani?Wanabodi,
Kwa jinsi nilivyoshuhudia uchaguzi wa marejeo wa Zanzibar, kwa mujibu wa ITV, uchaguzi huu ulikuwa ni huru na wa haki, hivyo tuyasubiri matokeo na kuyapokea na kuyakubali kwa moyo mmoja!.
Kwa mujibu wa sheria yetu ya uchaguzi, kote bara na visiwani, kujiandikisha kupiga kura ni kwa hiyari, pia kutokujiandikisha pia ni hiyari, vivyo hivyo kujitokeza kupiga kura siku ya uchaguzi pia ni hiyari, na kutokujitokeza pia ni hiyari hivyo wote waliojiandikisha lakini hawakujitokeza, wameamua kuitumia demokrasia yao kwa kutokujitokeza kupiga kura.
Kijitokeza kwao, au kutokujitokeza kwao, hakubadilishi matokeo ya uchaguzi kwa sababu sisi tunafuata mfumo wa simple majority kumpata mshindi. Hata kama jimbo lina wapiga kura laki moja, lakini waliojitokeza kupiga kura ni watu 3, hizo kura tatu zitahesabiwa, aliyepata kua mbili ndiye mshindi halali, na uchaguzi huo utaelezwa ni uchaguzi huru na wa haki!.
Ingekuwa ili mtu uwe mshindi ni lazima angalau upate lets say theluthi moja ya kura zote halali, then hao waliosusa, wangesababisha hiyo theluthi isipatikane hivyo kuathiri zoezi zima la uchaguzi, lakini huku kususa kusiko na impact yoyote, ni wastage of time, ndio maana nikauliza hao CUF wanasusa ili iweje?!.
Uchaguzi wa Zanzibar sasa umemalizika, tusubiri matokeo, tuwapongeze washindi na kuwapa pole washindwa!, tusubiri kuapishwa kwa rais mpya wa Zanzibar na maisha yaendelee, maana kiukweli kelele zilizidi mno!. Tena afadhali uishe ili wale wale MCA wailete ile hukua waliyoizuia ili tuitumie kusonga mbele!.
Pasco