Uchaguzi wa Marejeo Zanzibar ni Huru na Haki! Tuyasubiri Matokeo, Tuyakubali!

Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
29,758
Points
2,000
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2008
29,758 2,000
Hayo unayoyasema ni kweli na ndivyo inavyopaswa iwe! , lakini Aliyemteua Jecha ndiye aliyeteua hao majaji.
Kama aliamuriwa avunje sheria ya Zec kwa kufuta matokeo unilaterally with impunity, usishangae na hao wengine pamoja na kuujua ukweli wakashinikizwa wa rule otherwise, na kwa gharama yoyote!

Historia iko wazi, kwa matokeo ya kesi ya mgombea binafsi, jinsi ilivyohukumiwa ni somo
Kwenye hili la mgombea binafsi, nakubaliana na wewe, ila mashujaa wa kweli, siku zote hupambana by giving it a try na sio kuwa only a barking dogs seldom bite!.

CUF wangejaribu, dunia ingewaelewa!. Hicho kimya chao ndicho kimepelekea hili igizo la uchaguzi wa marudio kufanyika, na kwa sheria zetu mbovu, baada tuu ya kutangazwa mshindi, the end justify the means!, kwa sasa no one can do anything else!, the goal posts zimehamishiwa 2020.

Kuna kanuni inasema uwongo ukisemwa sana na ukaachwa bila kukanushwa hugeuka ndio ukweli wenyewe!, vivyo hivyo haramu ikiachwa kubaki haramu, hugeuka ni halali, kwa sababu hakuna yeyote aliyechukua hatua yoyote kuizuia hiyo haramu, hivyo igizo la uchaguzi huo ni huru na wa haki na limetupatia viongozi halali!.

Pasco
 
Bobwe2

Bobwe2

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Messages
2,171
Points
2,000
Bobwe2

Bobwe2

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2014
2,171 2,000
Mtoa mada,imethibitishwa pasi na shaka sasa tanganyika initawala zanzibar kwa nguvu za kijeshi.
 
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
29,758
Points
2,000
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2008
29,758 2,000
China Yasema Uchaguzi wa Zanzibar Ulikuwa Huru na Wa Haki.....Yaahidi Kuendelea Kutoa Misaada na Kushirikiana na TanzaniaBalozi wa China nchini Tanzania Dkt. LU Youqing amefanya mazungumzo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mh. January Makamba Ofisini kwa Waziri huyo Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo yao Balozi wa China amesema kuwa Serikali ya China inaamini kwamba uchaguzi wa Zanzibar uliofanyika mwishoni wa wiki iliyopita ulikuwa huru na haki.

Balozi Youqing amesema kuwa Makamu wa Rais wa China ametuma salamu za pongezi kwa Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein kwa kuchaguliwa kwake na kwa watu wa Zanzibar kwa kuendesha uchaguzi huo katika misingi ya haki na uhuru.

“Alikuwepo shuhuda wetu katika kushuhudia uchaguzi huo na alituambia kuwa ulikuwa wa haki na uhuru,” alisema Balozi huyo.

Katika mazungumzo hayo Balozi Youqing alisema Serikali ya China itaendelea kutoa misaada na kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwani huo ni wajibu wa mataifa makubwa kwa nchi zinazoendelea.

Alimhakikishia Mheshimiwa Makamba kwamba China ina mipango mingi ya ushirikiano na Tanzania, ikiwemo kwenye sekta ya umeme na itaendelea kutoa ushirikiano kwa Tanzania, ikiwemo kupitia makampuni ya China, ili kuhakikisha malengo ya Tanzania kwenye sekta ya umeme yanatimia.

Kwa upande wake, Mheshimiwa Makamba alimshukuru Balozi Youqing pamoja na Serikali ya China kwa ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo mbili.

“Ujumbe na salamu ulizotoa leo umetupa faraja Watanzania. Urafiki baina ya nchi zetu, na baina ya vyama vyetu vya CCM na CCP, ni wa muda mrefu, ni wa majira yote, na umejengwa kwenye misingi ya kuheshimiana na hauna budi kuendelezwa”, alisema Mheshimiwa Makamba.

Pia Waziri Makamba na Balozi Youqing walikubaliana kutembelea Pemba na Unguja kwa pamoja mwezi Aprili ili kukagua na kutengeneza miradi ya maendeleo kati ya China na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Vilevile, walikubaliana kuhusu kutengeneza mradi mkubwa wa ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muugano wa Tanzania na China kwenye teknolojia zitakazosaidia kupunguza matumizi ya mkaa, hivyo kuhifadhi mazingira.

Waziri Makamba pia amemueleza Balozi Youqing kuhusu hitaji na umuhimu wa ushirikiano katika kuiwezesha Tanzania kumiliki teknolojia ya uzalishaji wa nishati kwa kutumia taka ngumu zinazozagaa katika miji ya Tanzania ambapo Balozi Youqing aliahidi kulifuatilia suala hilo.

IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI,
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
.................................
Wanabodi,

Kwa jinsi nilivyoshuhudia igizo la uchaguzi wa marejeo wa Zanzibar, kupitia ITV, igizo la uchaguzi huu, limekidhi vigezo vyote vya uchaguzi huru na wa haki, hivyo ulikuwa ni uchaguzi huru na wa haki, hivyo sasa tuyasubiri matokeo tarajiwa na kuyapokea na kisha kuyakubali kwa moyo mmoja!.

Vigezo vya kimataifa vya free and fair elections ni hivi

 • Free and fair elections require:
° Universal suffrage for all eligible men and women to vote — democracies do not restrict this right from minorities, the disabled, or give it only to those who are literate or who own property.
° Freedom to register as a voter or run for public office.
° Freedom of speech for candidates and political parties — democracies do not restrict candidates or political parties from criticizing the performance of the incumbent.
° Numerous opportunities for the electorate to receive objective information from a free press.
° Freedom to assemble for political rallies and campaigns.
° Rules that require party representatives to maintain a distance from polling places on election day — election officials, volunteer poll workers, and international monitors may assist voters with the voting process but not the voting choice.
° An impartial or balanced system of conducting elections and verifying election results — trained election officials must either be politically independent or those overseeing elections should be representative of the parties in the election.
° Accessible polling places, private voting space, secure ballot boxes, and transparent ballot counting.
° Secret ballots — voting by secret ballot ensures that an individual's choice of party or candidate cannot be used against him or her.
° Legal prohibitions against election fraud — enforceable laws must exist to prevent vote tampering (e.g. double counting, ghost voting).
° Recount and contestation procedures — legal mechanisms and processes to review election processes must be established to ensure that elections were conducted properly.

 • Voting methods — varying by country and even within countries — include:
° Paper ballots — votes are marked on or punched through paper.
° Ballots with pictures of candidates or party symbols so that illiterate citizens may cast the correct vote. Uchaguzi halisi ulikuwa ni October, ambao ulikidhi vigezo vyote hivi!.

Kwa bahati mbaya sana, kususia uchaguzi, au kutokujitokeza kupiga kura, hakupelekei kubatilisha uchahuzi kugeuka sio free and fair na kwa mujibu wa sheria yetu ya uchaguzi, kote bara na visiwani, kujiandikisha kupiga kura ni kwa hiyari, pia kutokujiandikisha pia ni hiyari, vivyo hivyo kujitokeza kupiga kura siku ya uchaguzi pia ni hiyari, na kutokujitokeza kuoiga kura ni huyari na hata kususia uchaguzi pia ni hiyari hivyo wote waliojiandikisha lakini hawakujitokeza, wameamua kuitumia demokrasia yao kwa kutokujitokeza kupiga kura.

Kijitokeza kwao, au kutokujitokeza kwao, hakubadilishi au kubatilisha matokeo ya uchaguzi kwa sababu uchaguzi ni process, na sisi tunafuata mfumo wa simple majority kumpata mshindi. Hata kama jimbo lina wapiga kura laki moja, lakini waliojitokeza kupiga kura ni watu 3 tuu, hizo kura tatu zitahesabiwa ndizo kura halali, aliyepata kura mbili ndiye mshindi halali, na uchaguzi huo utaelezwa ni uchaguzi huru na wa haki!.

Ingekuwa ili mtu uwe mshindi ni lazima angalau upate asilimia fulani ya kura, lets say theluthi moja ya kura zote halali, then hao waliosusa, wangesababisha hiyo theluthi isipatikane hivyo kuathiri zoezi zima la uchaguzi, lakini huku kususa kusiko na impact yoyote, ni wastage of time, money and resources, na kitu kikubwa zaidi kuwanyima mamia kwa maelfu the right of choice, to choose their leaders, ndio maana nikauliza hao CUF waliosusa, wameendelea kususa ili iweje?!.

Uchaguzi wa Zanzibar sasa umemalizika, tusubiri matokeo, tuwapongeze washindi na kuwapa pole washindwa!, tusubiri kuapishwa kwa rais mpya wa Zanzibar na maisha yaendelee, maana kiukweli kelele zilizidi mno!. Tena afadhali uishe ili na wale MCA wailete ile hulua waliyoizuia ili tuitumie kusonga mbele ambapo Zanzibar nayo inao mgao wake asilimia 4.5%!.

Kwa wale ambao ni wageni na mimi, nimeandika sana humu kuhusu uchaguzi wa Zanzibar,
Imethibitishwa pasi na shaka Maalim Seif Alishinda, Zanzibar!
Zanzibar Issue: Kwanini watu wanapiga kelele tu bila kuchukua
Kuna haja ya kuhofia kurudiwa Uchaguzi Zanzibar? |
CUF kushiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar si hiyari,
Hatimaye CUF 'Wameridhia' Rasmi, Kushiriki Uchaguzi Wa Marejeo

Pasco
 
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
29,758
Points
2,000
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2008
29,758 2,000
Jecha alipofuta uchaguzi ni nani alikuwa amejaza fomu ya malalamiko?
Paschal jiongeze, kama kusoma hujui basi hata picha huoni?.
Paskali jibu hili swali
Unapigwa na pacha mmoja unaenda kumshtakia kwa pacha mwenzie?
Mkuu Gamba la Nyoka, msimamo wangu kuhusu kilichotokea Zanzibar uko wazi kabisa, Jecha hakuwa na mamlaka yale ya kujiugeuza ZEC, alichofanya Jecha ni kitendo haramu, lakini ili haramu iwe ni haramu kweli, lazima iharimishwe, haramu isipoharimishwa hugeuka halal!. Kwa vile ile haramu ya Jecha haikuharimishwa, hivyo ikahalalishwa na uchaguzi wa marudio.

Pia nikatolea mfano wa kubakwa. Kubaka ni kosa la jinai, lakini ili liwe kosa, lazima anayebakwa alalamike, mwanamke akibakwa asipolalamika, na akabakwa tena na tena, atahesabika ameridhia, hivyo Wazanzibari katika umoja wao, wameridhia unakaji huu wa demokrasia Zanzibar, kwa sababu hakuna yoyote aliyelalamika rasmi, kulalamikia kwenye media sio utaratibu rasmi wa kuwasilisha , malalamiko.

Kuhusu hili la Zanzibar, mimi mwenyewe tuu nimepandisha nyuzi Zaidi ya 10 na hizi ni baadhi tuu.
 1. Zanzibar: Kama Maalim Kajitangazia Ushindi, kwa nini hajashitakiwa? Jecha Kapata Wapi Mamlaka ile?
 2. Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda
 3. Zanzibar Issue: Kwanini watu wanapiga kelele tu bila kuchukua hatua zozote
 4. Kuna haja ya kuhofia kurudiwa Uchaguzi Zanzibar?
 5. Zanzibar: Japo SMZ ya SUK sio de jure tena bali ni de facto, lakini ipo!, na hakuna aliyejiuzulu!
 6. CUF kushiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar si hiyari, Ni lazima! Vinginevyo, huo ndio mwisho wake
 7. Hatimaye CUF 'Wameridhia' Rasmi, Kushiriki Uchaguzi Wa Marudio Zanzibar!.
 8. Uchaguzi wa Marejeo Zanzibar ni Huru na Haki! Tuyasubiri Matokeo, Tuyakubali!
 9. Jee Kuna Uwezekano Siku Zote Huwa Hazitoshi, Bali Zinatosheshwa?!. Utosheshaji Ulipogoma, Ukafutwa?!
 10. Uhalali wa Rais Dr. Shein Wa Zanzibar ni Kutokana na Uchaguzi Halali, Huru na Wa Haki! .
 11. Ukweli Mchungu Zanzibar: Hakuna Mgogoro Wowote wa Kisiasa, Shein ni Rais Halali, Uchaguzi ni 2020!
 12. Pemba Chini ya CCM kuneemeka au Kujutia Kuichagua CUF Chaguzi Zilizopita?!
 13. Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!
Paskali
 
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
29,758
Points
2,000
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2008
29,758 2,000
Hivi unajifanya huelewi kuwa huwezi kushitaki mahakamani matokeo ya uraisi , tume itavyoamua ndio hivyo hivyo
Mkuu Gavana, ukipata muda karibu mitaa hii
P
 

Forum statistics

Threads 1,304,805
Members 501,517
Posts 31,527,680
Top