Uchaguzi wa Madiwani kata za Arusha Waahirishwa hadi Juni 30, 2013

Facilitator

JF-Expert Member
Oct 30, 2010
2,280
1,763
Kufuatia tukio la mlipuko jana jumamosi Arusha, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeahirisha chaguzi za madiwani katika kata zote nne (4) jijini arusha hadi jumapili ya tar 30/6/2013.

Poleni wote mlioguswa na tatizo hili.

-----------------------------

Tume ya taifa ya Uchaguzi imesimamisha kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa udiwani ktk kata nne jijini Arusha. Akizungumza kwa njia ya simu na Radio TBC FM,kutoka Zanzibari mwenyekiti huyo wa tume ya uchaguzi alisema kua wameamua kusimamisha uchaguzi huo ili kuwapa nafasi vyombo vya usalama kuchunguza swala hilo.

Alisema kua sheria inawapa mamlaka kufanya hivyo pale wanapogundua kuwa hakutakua na uhuru wa mpiga kura kwenda kupiga kura. Alisema haiwezekani uchaguzi ufanyike ktk hali kama hiyo huku kukiwa na wasiwasi.

Kwa wale waliokua wanasema ni uongo basi sio uwongo ni kweli.

Source: Radio TBC FM.

Tume ya Uchaguzi Tanzania imeahirisha uchaguzi uliokuwa umepangwa kufanyika leo hii katika kata 4 za Mkoa wa Arusha. Kata zingine 22 zitaendelea na uchaguzi kama kawaida. Hii inatokaana na mlipuko wa bomu wa hapo jana.Sasa utafanyika jumapili tarehe 30.6.2013
 
Haya sasa! Wameanza tena longolongo zao hawa mafisadi.

ccm hata wangepeleka mwakani hakika hapa hawapati hata kiti moja mafisadi wakubwa wehu!

Tunashukuru kwa habari hii Mkubwa!
 
Huo bila shaka ni uamzi mzuri kwani utapisha muda wa kuomboleza na kufanya mazishi kwa wapendwa wetu, lakini pia seikali ijaribu kufanya jitihada za makusudi kubaini wale wote waliohusika.
 
Poleni wafiwa, poleni wanachama na wapenzi wa CDM na Wa TZania wote kwa ujumla. Tulinde amani vyama visituletee vurugu na tukubali kushindwa , kwani asiyekubali kushindwa si mshindani.
 
Hapa ndo wanatuonyesha ni nini walichokuwa wamekipanga?! Haya matukio wanausika 100%..
Wameona ni jinsi gani walivyokataliwa na wana Ars! Wakaona waweke huo mlipuko wako. Sasa ndo tutawaonyesha Ars ikoje? Rangi zote lazima wazione....
 
Hata waharishe mara elfu kumi...magamba lazima yajampe pale A-town.....Aluta continue!!!
 
Ccm ba by Arusha,tulikupenda lakini haupendeki,tunajua dhambi zenu zilizovunda ndani ya manispaa hadi mwaamua kutuua!!!Kisa umeya???SASA MWAKOSA VYOTE BARA NA PWANI KWANI HAPA NDIPO PALIPOZALIWA AZIMIO LA ARUSHA."mtalijua jiji".
 
Kuweni makini Wanaarusha, upo uwezekano mkubwa ikawa ni uongo wa CCMwewe. Kama msimamizi wa uchaguzi hajatangaza then nendeni mkapige kura leo!
 
Haya sasa! Wameanza tena longolongo zao hawa mafisadi.

ccm hata wangepeleka mwakani hakika hapa hawapati hata kiti moja mafisadi wakubwa wehu!

Tunashukuru kwa habari hii Mkubwa!

Mnadhani baada ya kuwatoa watu makafara, tume ingewaachia tu.
 
Huo utakuwa uongo dhahiri ulioletwa na mleta uzi,ambaye anaonekana kuwa among kwenye ile timu ya Nape ya propagandists, under Lumumba strategic team,ili kuwafanya wana Arusha,wasijitokeze kwa wingi kuwapigia kura wagombea wao wa CDM.

Hivi Tume ya uchaguzi,JK na CCM,watakuwa hawajitaki kwa kiasi gani,kupanga uchaguzi huo wenye tension kubwa,tarehe 30 mwezi huu,sambamba na ujio wa Obama?!

Wana Arusha puuzeni kwa nguvu zote,uvumi wowote utakaoenezwa kuwa uchsguzi huo umeahirishwa,na badala yske jitokezeni kwa wingi sana vituoni na wapigieni kura kwa wingi sana wagombea wa CDM,ili kuwapa aibu ya mwaka hao waliokuwa wamepanga mpango wao huo nwovu,wa kusababisha umwagikaji damu wa raia wasio na hatia,ili mradi tu watimize ndoto yao ya kulitawala Taifa hili la TZ milele!!
 
Huyo mleta thread kabeba bk 7 yake saf kabisa!!wana a town mapambano yanaendelea na biashara ni asubuhi jion kulinda kura tu..Nenden vituon mka pewe hizo taarifa huko na sio jamvin!Wamalizen nyinyiem mapema kabisa kata zote nne then mchana turud taifa kujaribu kumchezea simba sharubu...!
 
Ni jambo jema ila likitafsriwa vibaya zaidi litajenga chuki mno miongoni mwa wananchi kwani wanasiasa hutafuta mwanya wa kuchopeka pendeleo zao za kisiasa na mlipuko huo utatumiwa sana na wanasiasa Arusha
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom