Uchaguzi wa Libya Mashakani kufanyika. Kamati zavunjwa siku 2 kabla ya Uchaguzi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Tume ya uchaguzi nchini Libya imeagiza kuvunjwa kwa kamati za uchaguzi nchini humo na kutilia mashaka uwezekano wa kuandaliwa kwa uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika mnamo Disemba 24.

Ijumaa ya Disemba 24, ndio siku ambayo huenda ingekuwa muhimu kwa Walibya kwani kwa mara ya kwanza wangepata nafasi ya kuchagua Rais wao. Hata hivyo, kuvunjwa kwa kamati hizo za uchaguzi moja kwa moja kunamaanisha kuwa uwezekano wa kufanyika kwa uchaguzi ni mdogo mno.

Muda mfupi baada ya tangazo la tume hiyo ya uchaguzi, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya UNSMIL ulitoa taarifa na kuonyesha wasiwasi wake juu ya hali ya usalama katika mji mkuu Tripoli.

Ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa nchini Libya umesema kujihami kwa baadhi ya makundi kunatishia kuleta mvutano na kusababisha uwezekano wa kuzuka upya kwa mapigano. Ujumbe huo umeongeza kuwa, mizozo ya kisiasa inapaswa kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo.

Picha zilizochapishwa mitandaoni zimeonyesha vifaru na malori ya kijeshi katika wilaya ya Fornaj huku watu waliojihami kwa silaha wakishika doria katika baadhi ya barabara. Wakaazi wamesema shule na vyuo vikuu mjini Tripoli vimefungwa kama tahadhari.

Kujihami kwa makundi hayo kunatokea wakati Walibya wenyewe wakisuburi tangazo rasmi la kuahirishwa kwa uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Ijumaa wiki hii.

Uchaguzi huo ulikusudia kuhitimisha mpango wa amani unaoongozwa na Umoja wa Mataifa uliolenga kurejesha utulivu na kuiingiza madarakani serikali iliyochaguliwa kidemokrasia na kumaliza mzozo wa muongo mmoja.

DW Swahili
 
images - 2021-12-22T154951.563.jpeg
huyu kijana jina lake limo kwenye wagombea? Penyenye zinasemaje kuhusu kukubalika kwake?
 
Back
Top Bottom